Tuesday, March 28, 2017

RASMI NAPE ATUA MZIGO KWA MH MWAKYEMBE LEO


Aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye leo amekabidhi ofisi kwa Waziri Mpya wa Wizara hiyo, Dk Harrison Mwakyembe.

 Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ofisi za Wizara Mjini Dodoma na kushuhudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo  Profesa Elisante Ole Gabriel.

Wengine walioshuhudia makabidhiano hayo ni Naibu Waziri Anastazia Wambura , Naibu Katibu Mkuu Nuru Millao na watendaji wa Wizara.

TANZANIA KWENYE HEADLINE ZA KIMATAIFA UVAMIZI WA CLOUDS MEDIA


Asasi za kiraia 33 barani Afrika zimelaani kitendo cha kuvamiwa kwa studio za televisheni ya Clouds na kulazimisha maudhui yasiyostahili yarushwe hewani.

Tamko la asasi hizo limetolewa ikiwa ni siku chache baada ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, (THBUB), Jukwaa la Wahariri (TEF) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kulaani kitendo hicho kinachodaiwa kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari.

BASATA WAJITETEA BAADA YA KUAMBIWA WAACHIE WIMBO WA MR NEY


Baraza la Sanaa Taifa ‘BATASA’ limerudi tena na kuufungilia wimbo ‘Wapo’ wa Nay wa Mitego kwa madai waliufungia ili kupisha uchunguzi wa kipolisi upite baada ya jeshi hilo kumshikilia rapa huyo kwa siku mbili kutokana na wimbo huyo.

Awali baraza hilo lilitangaza kuufungia wimbo huo kwa madai hauna maadili kabla ya Rais Magufuli kutoa tamko la wimbo huo kuendelea kupigwa kwa kuwa hauna tatizo lolote.

Monday, March 27, 2017

MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA JUMUIYA YA WANAWAKE WALIOJIAJIRI (SEWA) KUTOKA INDIA


Mh Makamu wa Rais akipokea taarifa ya ziara kutoka kwa Shree Kumar anayemuwakilisha Renana Jhabvala pamoja na Pushpa Rathod - SEWA Makamu wa Rais baada ya kuvishwa alama ya heshima kwa mila za Kihindi kutoka kwa Pushpa Rathod

JPM Atoa Agizo kwa CAG Kukagua Sekta ya Madini


Rais Magufuli amemuagiza CAG kufanya ukaguzi wa kina katika sekta ya madini na kubaini mianya yote ambayo inasababisha nchi kukosa mapato makubwa hususani katika misamaha ya kodi, mikataba mbalimbali na ulipaji wa kodi.

Ametoa agizo hilo leo wakati akipokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Bakwata Yatoa Tamko Kuhusu Masheikh Walioenda Kusali Kanisani kwa Gwajima Jumapili

MSANII BARNABAR ALIZWA NA WEZI


Usiku wa kuamkia leo Barnaba ameibiwa begi lake lililokuwa ndani ya gari lake likiwa na vitu vya thamani ambavyo ni pamoja na baadhi ya kazi zake ambazo hazijatoka zilizokuwa kwenye hard disc, kamera na laptop mbili.

Barnaba amepost ujumbe Instagram kuwaomba wasamaria wema kumrudishia na kutoa maelezo jinsi ya kuwasiliana naye na kati ya vitu vilivyopotea ipo pia hati yake kusafiria(passport).

Ameandika:


 “Za asubui Ndugu Zangu wapendwa Usiku wa kuamkia Leo Nimeibiwa Begi langu Dogo Tu si Kubwa Sana ambalo lilikuwa ndani ya Gari langu | lakini ndani Yake Kulikua Na Laptop πŸ’» za mac mbili moja Pro x moja Letina ya ukubwa Kidogo Theni Kuna external mbili moja Rangi Ya orange 🍊 moja Ya kijani Na Kuna File Zangu zilikua Na Mikataba Mbali Mbali lakini Kikubwa zaidi Ndani Yake Kuna PASPORT Yangu ambayo Ukifungua ndani Inasoma Jina La ELIASI BARNABASI INYASI and Kuna Vitu Vingi Sana Vidogo vidogo Vyenye Thamani Kubwa Kama Camera πŸŽ₯Na vingine Lakini Naomba sana Sana Waungwana Kama Kuna mtu Yotote atabaini au kujua Vilipo au hata kupelekewa Basi Naomba wasamalia Wema mnirudishie Au kuniletea Na Napatikana kwa No 0743505010 Mungu Awabariki Na naamini Aliyenavyo ajaiba Bali amepitiwa katika njia ya kutafuta Ridhiki Nami kwa jina la mungu nitamsamehe Na nimesamehe ila Kama Ana Rohoo nzuri Na ameguswa Basi Naomba waungwana mnipigie hata Kama Umeokota 😰😭” Alipost Barnaba

RIPOTI YA VINASABA YATHIBITISHA KIFO CHA FARU JOHN


Na: Lilian Lundo - MAELEZO

Tume iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza kifo cha Faru John imethibitisha kuwa Faru huyo alikufa katika eneo la Sasakwa Grumeti kutokana na kukosa matunzo, uangalizi wa karibu na matibabu alipoumwa.

Hayo yamesemwa leo Jijini, Dar es Salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele alipokuwa akikabidhi ripoti ya uchunguzi wa Kifo cha Faru huyo kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

“Sampuli zilizochukuliwa kwa ajili ya uchunguzi wa vinasaba ni mifupa ambayo ilichukuliwa katika mzoga wa Faru John uliokutwa eneo la Sasakwa Grumeti, Pembe zilizochukuliwa hifadhi ya Dar es Salaam na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), damu kutoka maabara ya NCAA na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), ngozi kutoka kwenye mzoga na kinyesi kilichokaushwa kutoka SUA,” alifafanua Prof. Manyele.

Aliendelea kwa kusema kuwa matokeo ya uchunguzi wa awali yameonyesha damu, pembe, mifupa na ngozi ni vya Faru John ambapo mpangilio wa vinasaba umeonyesho kuwa Faru huyo ni mweusi (Black Rhinoceros) mwenye jinsia ya kiume.

Aidha vielelezo hivyo vilitumwa Chuo Kikuu cha Pretoria, Afrika Kusini ambapo timu ya wataalam kutoka Tanzania chini ya Mkemia Mkuu wa Serikali walishiriki katika uchunguzi wa awali wa vinasaba na kujadili matokeo kabla ya kuyatuma kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ambapo Matokeo yameonyesha sampuli na vielelezo vyote ni vya mnyama pori Faru John.

Vile vile amesema, uchunguzi umeonyesha kuwa sababu za kifo cha Faru huyo ni kukosa matunzo, uangalizi wa karibu, kukosa matibabu alipoumwa, mazoea yanayotokana na kutofuata taratibu zilizowekwa kisheria pamoja na mapungufu ya kiuongozi kwa Wizara, Hifadhi na Taasisi zake.

Baadhi ya mapungufu yaliyobainishwa katika uchunguzi huo ni pamoja na kutokuwepo na kibali rasmi kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori cha kuruhusu kumhamisha Faru John kutoka NCAA kwenda Grumeti.

Prof. Manyele amesema kuwa hakukuwa na mkataba rasmi kati ya Serikali na mwekezaji unaoonyesha mnyama ametoka Serikalini kwenda kwa Mwekezaji.

Tume hiyo imeishauri Serikali kuchunguza viwanja vya ndege ndani ya hifadhi vinavyomilikiwa na wawekezaji kutokana na kuwepo na uwezekano wa viwanja hivyo kuwa njia ya majangili au matajiri kufanikiisha shughuli za ujangiri nchini.

Aidha kutokana na mapungufu ya kiutendaji yaliyofanywa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Wanyamapori nchini (kutokutoa kibali rasmi) na mapungufu ya kiuongozi yaliyofanywa na Mhifadhi wa NCAA kuruhusu Faru John kuondolewa bila kibali, Tume inashauri hatua za kiutawala zichukuliwe dhidi ya wahusika.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza timu hiyo kwa kazi nzuri waliyoifanya. Ameahidi kufanyia kazi maoni ya tume hiyo na kutolea maelezo ya hatua zitakazochukuliwa na Serikali muda mfupi ujayo.

Tume ya uchunguzi ya kifo cha Faru John iliundwa baada ya Waziri Mkuu kufanya ziara ya kikazi Ngorongoro Disemba 6, 2016, ambapo alibaini kuhamishwa kinyemela kwa faru huyo na kudaiwa kupelekwa Grumeti. 

Waziri Mkuu alitaka ukweli kuhusu upotevu wa Faru huyo na kuamua kuunda tume hiyo ili kubaini ukweli wa Faru huyo kama alikufa au alitoroshwa.


Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa kulia akipokea taarifa ya Tume aliyounda kuchunguza kifo cha Faru John kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele jijini  Dar es Salaam leo
Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa kulia akionyesha taarifa ya Tume aliyounda kuchunguza kifo cha Faru John kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele jijini Dar es Salaam leo

RAIS MAGUFULI AFURAHISHWA NA WIMBO WA NAY WA MITEGO 'WAPO' WAZIRI AAGIZA NAY AACHIWE HURU

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, ameliagiza Jeshi la Polisi kumuachia huru Msanii Ney wa Mitego aliyekuwa akishikiliwa na Jeshi hilo.
Waziri Mwakyembe ameishauri pia BASATA kuondoa zuio lake dhidi ya wimbo huo, na badala yake uendelee kupigwa tu kama nyimbo nyingine.
Akiongea na wandishi wa Habari leo mjini Dodoma, Dk. Mwakyembe amesema hata Rais Magufuli amefurahishwa na wimbo huo wa WAPO, na kumshauri Msanii huyo kama inawezekana aendelee kutaja watu wengine kama vile wakwepa kodi, wauza unga, wabwia unga, wezi pamoja na watu wengine wasio na maadili mema katika jamii.

Agizo la kuachiwa kwa msanii huyo limekuja baada ya Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kueleza kuwa wimbo wa Nay wa Mitego uliosambaa kwenye mitandao hivi karibuni ukiwa na jina la ‘Wapo’ una matusi na haufai.

Katibu Mkuu wa Basata, Godfrey Mngereza alieleza kuwa Baraza liliusikiliza wimbo huo na kubaini kuwa ni wimbo usiofaa kwa jamii na zaidi unachochea vurugu.

“Ule wimbo tumeusikiliza, kama Baraza tunasema ule wimbo hauna maadili, ni wimbo ambao una matusi, ni wimbo ambao unachochea vurugu, ni wimbo ambao haufai kwa jamii,” alisema.

Aliongeza kuwa vyombo vyote vya habari ambavyo vitaucheza wimbo huo vitakumbwa na mkono wa sheria kutoka kwa vyombo husika.
Nay wa Mitego alikamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro majira ya saa nane usiku, na alifikishwa Dar es Salaam kwa mahojiano na Jeshi la Polisi.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, Kamanda Ulrich Matei alithibitisha kukamatwa kwa msanii huyo usiku wa kuamkia jana.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, wakili Peter Kibatala alisema kuwa atasimamia kesi dhidi ya msanii huyo na kwamba tayari ameshamjulia hali katika kituo cha kati jijini Dar es Salaam.

Sunday, March 26, 2017

Huu ni ufafanuzi kutoka Mahakama ya Tanzania kuhusu uteuzi wa Kaimu Jaji Mkuu

Mahakama ya Tanzania imewathibitishia wananchi kuwa itaendelea kufanya kazi zake kwa mujibu wa Katiba na Sheria na kwa jitihada kubwa bila woga, hofu, huba wala chuki kwa wadau wote kama inavyopaswa.
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam kwa vyombo vya habari na Jaji Kiongozi, Ferdinand Wambali ilieza pia kwamba hakuna kosa la kikatiba lililofanywa na Rais John Magufuli kwa kumteua Kaimu Jaji Mkuu kama inavyopotoshwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Mbwana Samatta anamiliki mijengo sita Dar

Achana na uwezo wa Mbwana Samatta akiwa uwanjani. Mchezaji huyo siyo wa mchezo pia kiuchumi– ana mijengo takribani sita jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa gazeti la Mwanaspoti, mshambuliaji huyo wa Taifa Stars na klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji amewekeza zaidi katika kujenga nyumba ambazo zote hizo zipo Mbagala lakini katika maeneo tofauti tofauti.
Imedaiwa kuwa mijengo hiyo ya Samatta ipo Majimatitu, Kiburugwa Shimo la Mchanga, Mbande na Mbagala Saku (zote zipo Mbagala) ukiachana na ile ikulu yake anayoijenga huko kibada ambayo tayari imeisha japo kuna marekebisho madogo madogo yanaendelea.
Wakati huo huo rafiki wa karibu wa mchezaji huyo aliliambia gazeti hilo kuwa mchechezaji huyo anaishi katika nyumba yake aliyopanga (Apartment) iliyopo katika ufukwe wa bahari ya Hindi maeneo ya Kijichi.
“Anapokuja kwa mapumziko kwao huwa anakwenda kwa sababu ni nyumbani kwa ajili ya kusalimia na mambo mengine lakini hakai hapo, anaishi Kijichi kuna nyumba nzuri ya kifahari ipo ufukweni mwa bahari amepanga,”alisema.

COVENANT BENKI KUKISAIDIA KIKUNDI CHA FARASI KUNUNUA HISA ZA VODACOM NA KUWAPATIA BIMA YA AFYA KWA WANA KIKUNDI

Covenant ni benki inayowajali wananchi wa hali ya chini na idara binafsi. Leo kikundi hiki cha farasi kimeweza kutimiza mwaka mmoja. Kikiwa ni kikundi kilichoweka fedha zake katika benki hiyo na kuweza kupewa mwongozo jinsi ya kunufaika na huduma za benki hiyo. Wanachama wa kikundi hiko walianza wakiwa 20 na na kwa sasa wapo 40 na bado kuna wengine wanaomba kujiunga. Grace Boniphace Luwiku Mwenyekiti wa kikundi hiko alisema kuwa wanafurahia mafanikio ya mwaka mmoja wakiwa ndani ya Covenant kwa kuwa waliweza kutimiza malengo yao waliyo ya kusudia. walihitaji kuwa na biashara ya pamoja waliweza kufanikiwa na walihitaji kila mwanachama awe na biashara yake waliweza pia na waliona kitu muhimu ni afya waliweza kukatiwa bima ya afya  ya AAR.
Na kwa leo wanaweza kufurahia mafanikio waliyoyapata ndani ya mwaka mmoja.

MKURUGENZI MTENDAJI WA COVENANT BENKI SABETHA MWAMBENJA AKIONGEA NA VYOMBO VYA HABARI  KWA  KUKIPONGEZA KIKUNDI CHA FARASI KUTIMIZA MWAKA MMOJA.

Saturday, March 25, 2017

WABUNGE ZITTO NA LEMA USO KWA USO ARUSHA LEO
Mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema akipongezwa na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, mara baada ya kuhutubia mkutano mkuu wa kidemokrasia wa chama hicho uliolenga kuadhimisha miaka 50 ya Azimio la Arusha, mkutano uliofanyika jijini Arusha


VIDEO-COVENANT TZ KUKIPONGEZA FARASI GROUP.

VIDEO-COVENANT BANK KUSAIDIA VIKUNDI VIDOGO VIDOGO KUNUNUA HISA ZA VODACOM

LIPUMBA KUUNDA CUF MPYA TAYARI KWA MAPAMBANO YA KISIASA

Soma Hotuba Ya Zitto Kabwe aliyoitoa Muda mchache Uliopita Huko Arusha


  Hotuba ya Arusha

Nafasi ya Ujamaa wa Kiafrika katika Uchumi wa sasa
Kumbukizi ya Miaka 50 ya Azimio la Arusha
Ndg. Zitto Kabwe
25 Machi 2017

Hotuba ya Anna Mghwira maazimisho ya Azimio la Arusha


MKUTANO WA KIDEMOKRASIA, ARUSHA


MARCH 25, 2017
  
MADA:  UZOEFU WA KUNADI SERA ZA KIJAMAA KATIKA MAZINGIRA YA UBAPARI UCHWARA:

Mama Anna Elisha Mghwira,
Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo.


Ndugu wananchi wote
Wageni Waalikwa,
Viongozi wa ACT WAZALENDO,
Mabibi na Mabwana.

TASWE INTERNATIONAL TRADE FAIR 2017 MARCH 25 - 31, 2017

KAMATI YA BUNGE YAWATAKA WATUMISHI WA UMMA KUCHANGAMKIA NYUMBA ZINAZOJENGWA NA SERIKALI

 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),Mhandisi Elius Mwakalinga (wa tatu kulia), akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Fedha za Serikali (PAC), kabla ya kutembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za Bunju B jijini Dar es Salaam jana zinazojengwa na wakala huo. Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Josephat Asunga.

MAKAMANDA WA POLISI KUKUTANA DODOMA KUPANGA MIKAKATI YA KUPAMBANA NA UHALIFU


Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.

MAOFISA Wakuu wa Jeshi la Polisi  wanatarajia kukutana mkoani Dodoma kuanzia Jumatatu tarehe 27-29/03/2017 katika kikao kazi cha siku tatu kujadili na kupanga mikakati mbalimbali ya kukabiliana na uhalifu na wahalifu hapa nchini.


Hospitali ya Kimataifa ya Aga khan imeanzisha mfumo maalum wa utoaji wa tiba kwa akina mamaPichani ni  Meneja Masoko na Mawasiliano kutoka Aga Khan Olayce Lotha
NA KAROLI VINSENT
HOSPITAL ya Kimataifa ya  Aga khan kwa kushirikiana na Daktar bingwa wa masuala ya akina mama  kutoka Uengereza imeanzisha mfumo maalum wa utoaji wa tiba kwa akina mama wenye  uvimbe katika milango ya kizazi bila kuwafanyia upasuaji mkubwa ambapo zoezi hilo litakua endelevu lengo ni kuhakikisha huduma hiyo inawafikai wananchi wengi  .

CHADEMA WAMTAKA RAIS DK. MAGUFULI KUELEZA SABABU ZA KUTENGUA NAFASI YA UWAZIRI WA NAPE NNAUYE

 Makamu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu chama hicho kuwateuwa Lawrence Masha na Ezekia Wenje kugombea Ubunge wa Afrika Mashariki pamoja na mambo mbalimbali yayoendelea nchini. Kulia ni Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene.

Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Friday, March 24, 2017

VIDEO-MSIKILIZE BONIFACE JACOB MWANANCHI WA DAR ES SALAAM

KAMPUNI YA SIMU YA ITEL YATOA MISAADA KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI YA MUGABE SINZA DAR ES SALAAM

Kampuni inayotengeneza simu za mkononi za Itel lmetoa misaada kwa wanafunzi wenye mahitaji katika shule ya sekondari ya Mugabe iliyopo Sinza  jijini Dar es salaam. Misaada hiyo ikiwemo madaftari kalamu za wino na mabegi zaidi ya 100, misaada hiyo  na imepokelewa na makamu mkuu wa shule hiyo Bw. Elias Kambawala na kugawiwa kwa wanafunzi hao. Baada ya zoezi la ugawaji wa zawadi hizo pia kulikuwa na michezo tofauti tofauti kama mashindano ya mpira wa miguu, kushindana kuimba pamoja na kucheza miziki mbalimbali.

Afsa masoko wa Itel akiongea na vyombo vya habari jinsi walivyotoa misaada kwa wanafunzi shule ya mugabe
Saifoni Asajile ni meneja masoko wa kampuni ya Itel Tanzania amesema  kuwa zoezi hilo limekwenda vizuri kama lilivyopangwa na wanfunzi wamepokea kwa furaha kubwa sana huku pia alisisitiza zoezi hilo sio kama ndio limeanza kwa shule hiyo tu. Bali ni zoezi linafanyika kila mwezi katika shule mbalimbali lengo likiwa ni kuwapa fursa hata kwa wasio na uwezo kuona wanathaminiwa katika jamii.Kama mwezi uliopita waliweza kuwa shule ya msingi  air wing kwa wanafunzi wenye uhitaji maalum na zoezi bado linaendelea kwa mikoa yote nchi nzima.

Makamu mkuu wa shule bw. Elias Kambawala akielezea jinsi alivyoweza kupokea misaada hiyo
Makamu mkuu wa shule hiyo Bw Elias Kambawala amesema kuwa wamepokea misaada hiyo na imeweza kuwafikia walengwa ambao ni wanafunzi wenye uhitaji. Pia aliongezea kusema wanafunzi hao walikuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosa vifaa vya taaluma hiyo na kwa sasa wameweza kuipata misaada hiyo itawapa motisha ya kupenda kusoma. 

VIDEO-BALOZI MSTAAFU PATRICK CHOKALA AIUNGA MKONO TAASISI YA MAMAZ & PAPAZ

NAIBU MEYA WA MANISPAA YA ILALA, OMARY KUMBILAMOTO ATEMBELEA OFISI ZA MICHUZI MEDIA GROUP (MMG)

 Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto akisalimiana na Msimamizi wa Chumba cha Habari, Cathbert  Kajuna wakati alipotembelea ofsi za MMG leo.
  Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto, akisalimina na mwandishi mwandamizi na Msimamizi wa Habari za Mahakamani, Karama Kenyunko wakati alipofanya ziara katika ofisi za MMG.

MPIGA CHAPA MKUU ASISITIZA KAMPUNI KUENDELEA KUJISAJILI

Mpigachapa Mkuu  wa Serikali,Cassian Chibogoyo akionesha waandishi wahabari (hawapo pichani) katika moja ya mikutano yake  rangi sahihi  ya bendera yaTaifa, kulia ni Afisa Habari wa Idara Habari Maelezo, Frank Shija. (NA MPIGA PICHA WETU)

COCA-COLA YAZIDI KUHAMASISHA WANAFUNZI KUTAMBUA NA KUKUZA VIPAJI VYAO

Wafanyakazi wa Coca-Cola wakiwagawia wanafunzia wa Shule ya Sekondari ya Olorieni Vinywaji vya Coca-Cola katika eneo la shule hiyo.
Mwanafunzi wa Shule ya sekondari ya Olorieni akionyesha kipaji cha kucheza na Baiskeli kupitia promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya Onja msisimko katika shule mbalimbali.
Wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Olorieni wakionyesha kipaji cha kucheza na baiskeli kupitia promosheni inayoendeshwa na Coca-Cola ya Onja msisimko katika shule mbalimbali.

ZINGATIA KUNUFAIKA NA OFA MBALIMBALI ZINAZOTANGAZWA


Na Jumia Travel Tanzani
Ni mara ngapi umeshawahi kusikia ofa mbalimbali za mtangazo ya biashara kupitia vyombo vya habari? Je huwa unashawishika au kuvutiwa nayo mpaka kukupelekea kununua?

Kutoa punguzo la bei ni njia ya haraka zaidi inayotumiwa na wafanyabiashara wengi kuwavutia wateja. Tafiti zinaonyesha umakini wa mteja na ushawishi katika kutumia huduma fulani huja kwa ofa au punguzo la bei. Muda wowote ambao utamwambia mteja kwamba anaweza kuokoa pesa, ipo asilimia kubwa ya kuteka umakini wake na kukusikiliza. Zipo sababu kadhaa zinazowafanya wafanyabiashara kutoa matangazo ya punguzo katika bidhaa na huduma zao. Sababu hizo zinaweza kuwa kama vile kuwavutia wateja, kuongeza mauzo, kupunguza hifadhi ya bidhaa zisizohitajika dukani, kujijengea jina, kufikia malengo ya kibiashara, na kuokoa gharama nyinginezo za kuendesha biashara.Tukielekea msimu wa mapumziko ya sikukuu za Pasaka tunaamini utayasikia matangazo ya kila aina yanayokushawishi kutumia huduma fulani. Huduma kama vile za usafiri, mavazi, malazi, samani na kadhalika ni miongoni mwa zitakazokuwa kwenye mzunguko wa vyombo mbalimbali vya habari kukuvutia wewe mteja.   

Jumia Travel inaamini kwamba sio watu wote ambao wanatumia ofa hizi ambazo hutangazwa mara nyingi kwenye misimu ya sikukuu kama hii ya Pasaka ambayo inakuja. Inawezekana kukawa na sababu za mtu kuamua kutotumia ofa hizo lakini kuna manufaa mengi tu kama vile: 

Kuokoa gharama za matumizi yako ya kawaida. Ni kweli kabisa endapo utakuwa ukifanya manunuzi yako kipindi cha ofa utakuwa unafaulu katika hili. Kipindi pekee ambacho huwa na ofa nyingi ni cha sikukuu na mwisho wa mwaka. Na ni kutokana na uhitaji mkubwa kutoka kwa wateja kwa wakati huo ndio unaowalazimu kufanya manunuzi makubwa. 

Lakini pia ofa hurahisisha mahitaji yako kama mteja. Kupitia punguzo la bei unaweza kukuta pesa ambayo ilibidi ununue bidhaa moja unaweza kuongezea na zingine. Hivyo hapo utakuwa umerahisisha mahitaji yako kwa kutumia kiasi kilekile bila ya nyongeza yoyote. 


Kwa hali ya maisha ya sasa inabidi mtu kuwa makini sana na namna unavyotumia pesa kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Umakini huo ni pamoja na kufuatilia kwa ukaribu ili kuendana na tabia za wafanyabiashara na soko kwa ujumla.

Fuatilia kujua ni kipindi gani bei za bidhaa na huduma huwa ni za gharama ya juu na ni wakati gani hushuka. Kwa mfano, itakuwa haina maana kununua luninga kwa bei fulani wakati unaweza kuipata kwa nusu bei kipindi cha ofa.

Kwa wafanyabiashara wengi nchini na duniani kote kwa ujumla, hutoa ofa za bidhaa na huduma hasa kipindi cha sikukuu na mwisho wa mwaka. Kwa sababu kipindi hiko uhitaji miongoni mwa wateja huwa ni mkubwa na wako radhi kununua bidhaa au kutumia huduma. 

Jaribu kuanza kufuata utaratibu huu kuanzia sasa na uone ni kwa namna gani utakuwa na manufaa kwako. Mwaka bado mbichi, zipo sikukuu kadhaa zinakuja siku za usoni. Jaribu kutembelea Jumia Travel ujionee ofa zilizotolewa na hoteli mbalimbali kwa ajili ya msimu huu wa sikukuu.

VIJUE VIWANGO MAALUM VINAVYOLIPWA NA MMILIKI WA NYUMBA AU JENGO VINAFSI

Thursday, March 23, 2017

VIDE-SOBA HOUSE MPYA YAANZA DAR KWA LENGO LA KUSAIDIA VIJANA WA KITANZANIA

TAMTHILIYA YA KICHINA YA 'MFALME KIMA' ILIYOTAFSIRIWA KISWAHILI YAZINDULIWA NCHINI

 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante ole Gabriel (wa nne kutoka kushoto) na Naibu Waziri wa Masuala ya Utangazaji, Filamu na Habari wa China, Tong Gong (katikati), wakikata utepe kuzindua maonyesho ya kwanza ya tamthiliya ya China ya 'Mfalme Kima' iliyotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam. Wa pili kutoka kushoto ni Jiang Almin, ambaye ni Mkurgenzi wa Radio China Kimataifa, wa pili kutoka kulia ni Suzan Mungy (Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma na Matukio wa Shirika la Utangazaji Tanzania - TBC) na wa nne kulia ni Ma Li (Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Kimataifa wa China).

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante ole Gabriel,  akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya tamthiliya ya China ya 'Mfalme Kima' iliyotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili. 
 Ma Li, Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Kimataifa wa China, akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika leo hii jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa StarTimes, Guo Zingi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamthiliya ya 'Mfalme Kima' ambayo ni ya Kichina iliyotafsiriwa kwa Kiswahili.
 Suzana Mungy, Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma na Matukio wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamthiliya ya Kichina ya 'Mfalme Kima' iliyotafsiriwa Kiswahili. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurgenzi wa Radio China Kimataifa,  Jiang Almin, akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
 Meza kuu ya wageni wa heshima katika uzinduzi huo.
 Akinadada wa StarTimes wakiwa wamejiandaa kabla ya kukatwa kwa utepe kuashiria uzinduzi wa maonyesho ya kwanza ya Tamthiliya ya China ya Mfalme Kima iliyotafsiriwa kwa Lugha ya Kiswahili.
Wageni waalikwa wakifuatilia mambo yaliyokuwa yakiendelea.
 Wasanii wakitumbuiza kwenye uzinduzi huo.
 Wageni mbalimbali wakifuatilia.
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa StarTimes, wasanii wa wageni wa heshima.