Friday, February 23, 2018

HILI NDIO LENGO LA MEYA WA BLANTYRE KUKUTANA MEYA WA DAR

           MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo amekutana na kufanya mazungumzo na Meya wa Jiji la Blantyre  Nchini Malawi Wild Ndipo ambapo pamoja na mambo mengine wamejadiliana namna watakavyoweza kubadilisha uzoefu katika kuendesha majiji.

Aidha ugeni huo wa Meya wa Jiji la Blantyre ulihusisha madiwani watatu, Balozi mdogo wa Maalawi Sai Kaphale ambapo wote walipata fursa ya kutembelea mradi wa mabasi yaendayo haraka (UDART).
Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kufanya mazungumzo hayo, Meya Mwita amesema lengo la ugeni huo ni kuendeleza urafiki ambao utawezesha kubadilishana ujuzi kwenye uendeshaji wa majiji hususani kwenye miundombinu  ya Elimu, barabara ,Utalii na huduma nyingine za kijamii.
Amesema kuwa wakiwa jijini hapa watajifunza namna ya kuendesha miundombinu hiyo hususani ya Barabara na Elimu ambapo kwa Jiji la Dar es Salaam limepata mafanikio makubwa kwenye utoaji wa huduma hizo.

Ameongeza kuwa mbali na miundombinu  hiyo,  lakini watapa fursa ya kujifunza namna ya ukusanyaji kodi na kuongeza mapato kwenye jiji ambapo kesho watashiriki kwenye baraza la Bajeti  litakalokaa siku mbili.
Kwaupande wake Meya wa Jiji la Blantyre Wild Ndipo amefurahia mapokezi waliyopata kutoka kwa Meya Mwita na kuahidi kushirikiana na jiji la Dar es Salaam katika masuala mbalimbali ya maendeleo
                                      ANGALIA HAPA KUJUA MENGI ZAIDI..
                      

No comments: