Tuesday, December 15, 2015

G4S yaimarisha huduma za ulinzi Tanzania kwa kutambulisha Teknolojia mpya.

Henrik Krag kutoka Zonith akiwa na askari wa kampuni ya Q4S akielezea jambo kwa wageni waalikwa

Inj.Omar Bakar kutoka Tanzania Data Lab akiwasilisha mada kwenye hafla ya uzinduzi wa huduma mpya za Teknolojia ya ulinzi wa kisasa zenye kulinda watu na mali zao kutoka kampuni ya G4S Tanzania.

Sugandran wa Geo Tab akiwasilisha mada kwa wageni waalikwa


Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Jensen akizungumza na wageni waalikwa juzi jijini Dar Es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa huduma mpya za Teknolojia ya ulinzi wa kisasa zenye kulinda watu na mali zao kutoka kampuni ya G4S Tanzania.


·         G4S inatoa huduma za ulinzi zinazotumia teknolojia kusaidia taasisi na watu binafsi kulinda watu na mali zao.
Tarehe 8 Februari 2019, Dar es salaam. Wakati ambapo ni muhimu kupunguza gharama za uendeshaji, sio tu kwamba teknolojia itasaidia kufikia malengo haya lakini pia itaweza kutoa manufaa zaidi ya kuaminika na ufanisi.  Kwa kuongezea zaidi matuko mengi ya matumizi ya teknolojia inayostahili imeweza kuondoa maofisa wa ulinzi katika maeneo ambayo kuna hatari ya watu kuumia.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa teknolojia mpya ya ulinzi inayotolewa na G4S, Balozi wa Denmark Mhe. Einar H. Jensen alisema kwamba uimarishaji wa usalama wa watu na mali zao katika kanda hili umekuja katika wakati muafaka kwaajili ya kukabiliana na vitisho vilivyoshuhudiwa hivi karibuni.  'Dunia inabadilika kwa kasi sana na mahitaji ya kulinda watu na rasilimali hayajawahi kuwa makubwa kama hivi sasa. Mahitaji ya usalama kwa watu wa Afrika Mashariki vile vile yanazidi kuongezeka. Si muda mrefu tulikabiliana na uvamizi wa kikatili wa magaidi katika hoteli nchini Kenya, tunapaswa kuwa tayari kwa mashambulizi ya aina hiyo katika siku zijazo.  
Akitangaza uzinduzi wa bidhaa za kisasa mwaka 2019, Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa G4S Secure Solutions Tanzania, Andrew Lauwo amesema 'Mfumo wa Ulinzi wa ishara ya kengele ya video (A video alarm security system) (Videofied) iliyotengenezwa Ufaransa yenye uwezo wa kuhisi mtu anapoingia na kisha kutuma video ya haraka kwenye control room ya G4S na kwenye simu yako pale mtu anapoingia katika sehemu husika ni bidhaa nyingine iliyoko katika ofa: Mfumo huu unatumia betri na hauna waya na unaweza kufungwa nje au ndani.  Mfumo wa VIDEOFIED unatumika zaidi kulinda mali na pia unatumika katika mazingira ya nje kama vile sehemu za kuhifadhia boti, maeneo ya burudani ya nje, katika njia na sehemu nyingine ambako nishati ya umeme hakuna.'
'At the Gate' (Katika Mageti) ni mfumo wa kudhibiti waingiaji ambao unaruhusu ufuatiliaji wa nani anaingia na kutoka katika eneo lako kwa kuskani magari na taarifa za leseni za madereva wanapoingia na kutoka kupitia kifaa cha Android.  Kifaa hiki kinafanyakazi kwa kutumia mtandao wa simu au kuunganishwa na Wi-Fi na kutoa vipengele mbalimbali vinavyokutaarifu mgeni anapofika getini, picha nyingi za magari na walioko ndani, taarifa za laptop, silaha,simu za smart, tablets nk. zinazoingia na kutoka katika eneo nk.'. aliongeza.
Akitolea maoni kuhusu mfumo wa kufuatilia magari (Vehicle Tracking Management System) alisema, ‘Geotab kutoka Canada: ni mfumo wa kufuatilia magari na kufuatilia tabia za dereva ambao pia unatoa kifaa cha ufahamu wa dereva (Driver Awareness tool) kinachobadilisha jinsi mafunzo ya mereva yanavyofanyika wakati wa kuendesha kwa kutoa maelekezo ya sauti ya hapo kwa hapo kwa dereva. Zaidi ya eneo halisi gari liliko, taarifa za kasi ya gari idadi ya tripu na umbali ambao tayari ameshasafiri, utendaji wa dereva kama vile kufunga breki kwa haraka, kukata kona na takwimu za utulivu wa kupita kiasi pia zinapatikana.  Mfumo huu umetengenezwa kusimamia na kufuatilia utendaji wa gari, tabia za dereva na kuboresha mifumo ya usalama.'
Vilevile alisema kwamba, ‘The Sentinel Perimeter Protection kutoka Afrika ya Kusini ni mfumo wa masafa marefu wa kutambua uvunjaji na kuzuia ambao unatoa ishara ya kengele unapokuwa umekiukwa na kutuma video za tukio kwa kutumia Wi-Fi wakati pia ikiwa inatuma ishara ya tahadhari kwenye Control room yetu na katika simu yako ya mkononi masaa 24/7 Ina uwezo wa kusimamia eneo la mita 150 na vipengele vya ziada vinaweza kuongezwa kwenye mfumo huu kutoa ulinzi wa asilimia 100% katika eneo husika. 
Akiongea kuhusu mfumo wa ulinzi kwa kutimia video ulioko katika ofa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa ZONITH, Kristian H Stiesmark amesema kwamba 'Ishara ya Kengele ya Hofu Binafsi (Personal Panic Alarms) iliyoundwa na ZONITH, kampuni ya teknolijia ya kiwango cha juu ya watu wa Denmark inatoa kifaa cha kutolea ishara ya kengele ya hofu binafsi cha kufunga mahali na cha kutembea nacho ambacho kinamruhusu mtumiaji kuita msaada kutoka katika kikosi cha kuitikia matukio cha G4S panapotokea vitisho vya kiusalama au huduma ya kimatibabu au dharura ya moto. Zonith inatoa teknolojia ya kuchagua inayotumia Bluetooth ambayo inaruhusu ishara ya kengele na sehemu ulipo kutumwa kutokea sehemu yoyote  ambako mtandao wa GSM unapatikana.'

No comments: