Wednesday, October 12, 2022

RAIS SAMIA MGENI RASMI KATIKA MJADALA WA KITAIFA WA NISHATI UTAKAOFANYIKA NOVEMBA 1-2, 2022 DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika mjadala wa kitaifa wa utaokuja na suluhu ya namna watanzania watakavyohamasika na matumizi ya Nishati mbadala na kuachana na nishati isiyofaa. 

Mkutano huo utakaofanyika Novemba 1-2, 2022  katika Kituo cha cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam utaratibiwa na Wizara ya Nishati.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Oktoba 12, 2022. Waziri wa Nishati Januari Makamba amesema kuwa mkutano huo utawakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta za Afya, Nishati, Mazingira, Jinsia, Usawa watunga sera pamoja na sheria mbalimbali ili kuweza kujadiliana namna gani wanaweza kupunguza au kuondoa kabisa matumizi ya nishati ya isiyo safi na salama. 

Amesema Sera ya Nishati ya 2015 inayosimamiwa na wizara ya nishati inaelekeza Wizara ya Nishati kuchukua hatua za kuwawezesha watanzania kupata nishati safi na salama na kwa gharama wanayoimudu ili kuboresha ustawi wa watanzania kwa kiasi kikubwa. 

Waziri makamba amesema kuwa Mjadala huo utaratibiwa na wizara ya Nishati ili kupata majibu ya kudumu ya kuondokana na matumizi ya nishati ya kupikia ya Mkaa na kuni nchini pamoja na kupata uelewa wa pamoja juu ya suala nishati ya kupika hapa nchini.

Amesema kuwa katika mkutano huo watangazi katika mlengo wa kiuchumi, Kijinsia afya Usawa na mazingira kwa namna ambavyo tunapika hapa nchini kwa kutumia Nishati safi na Salama. 

Waziri Makamba amesema mjadala huo utapelekea kutambua Changamoto za kutumia kuni na Mkaa, athari zilizipo na kuangalia matokeo yake ni nini. 

Amesema Mifumo ya Kisera Sheria, Kikodi, Kifedha na Utawala itawekwa kwaajili ya kupambana na hali ya namna tunavyopika na kuwaondoa watanzania kutumia nishati inaathiri Afya na Maisha. 

Akizungunzia kuhusiana na madhara yanayojitokeza katika jamii juu ya matumizi ya kuni, Mkaa na nishati nyingine zisizo safi na salama Waziri Makamba amesema Vituo vya afya Nchini vimeelemewa na mzigo Mkubwa wa utoaji huduma za afya za mfumo wa upumuaji zinazotokana na namna tunavyopika.

Amesema Watanzania zaidi ya elfu 33 wanafariki dunia kwa mwaka kutokana na kuvuta moshi wa namna tunavyopika chakula hivyo hii inaendelea kuathiri akina mama na watoto wa kike kwa  kupoteza muda mwingi kwenye kutafuta nishati ya kupikia ya kuni na Mkaa. 

Asilimia 70 ni magonjwa yasiyoambukiza ikiwemwo magonjwa ya mfumo wa upumuaji.

"Wanapokuwa wanatafuta nishati hiyo wanapunguza muda wa kutafuta elimu au kufanya shughuli nyingine za uzalishaji mali huko polini wanakutana na dhahama na matukio ya unyanyasaji wa kijisia.

Pia Nishati  isiyo safi na salama inaleta utofauti au kutokuwa na usawa kati ya wanawake na wanaume, watu wa mjini na vijijini wenye kipato na wasio na kipato." Amesema  Waziri Makamba

Kwa Upande wake Daktari Bingwa wa Magonjwa ya mfumo wa Upumuaji, kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Pauline Chale ameeleza kuwa Matumizi ya Nishati isiyo safi na salama  inasababisha changamoto nyingi hasa katika Afya na matibabu yake ni gharama kubwa 

Dkt. Pauline ameeleza kuwa mgonjwa wa Mfumo wa Upumuaji yanaondoa watu. Pia amesema matumi ya kuni, Mkaa na Mavi ya wanyama yanasumu zaidi ya 200 ndio maana watu wengi wanakuwa na macho mekundu kutokana na sumu hizinazopatikana kwenye moshi.

Wednesday, October 5, 2022

Kamati ya Kutafuta Mdundo wa Taifa yakamilisha kuchukua maoni Katika Mkoa wa Dar es salaam

Na Moshi Saidi Dsm.

Kamati ya Mdundo wa Kitaifa iliyoundwa hivi karibuni na Waziri Tamaduni Sanaa na Michezo  Mohamedi Mchengrwa imepokea maoni  Kutoka kwa Wadau mbalimbali wa muziki ikiwemo watayarishaji wa muziki,watunzi,watangazaji wa vyombo vya habari pamoja wasanii wa ngoma za asili lengo ni kupata vionjo vitakavyotumika kutengeneza Mdundo wa kitaifa.

Wajumbe wa Kamati ya kutafuta Mdundo wa Kitaifa wakiendelea kukusanya maoni.
Wakitoa maoni katika Mdahalo uliofanyika Jijini Dar es salaam Mkurugenzi kikundi cha muziki (Kay wa Mapacha) Levison Kasuhuwa alisema tangu nchi  imepata  uhuru haijawahi kuwa na mdundo wa kulitambulisha Taifa hivyo wasanii wa muziki wameiga Midundo ya za nje kutengeneza muziki yao hivyo sasa kwakuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassani kupitia kamati iliyochaguliwa lazima ije na mdundo utakaokwenda kubadilisha taswira za watu kuondokana na kutumia Midundo isiyo ya asili yao   

"Tunakubali kuwa ukoloni umetuathiri kwa kipindi kirefu kwa kuacha Tamaduni zetu kuna usemi asiyependa kwao ni mtumwa hivyo tumechoka kuwa watumwa kutumia Midundo ya kigeni Sasa ni wakati wa kuwa na mdundo wetu wa asili ambao utatutambulisha "alisema Levision

Sixmondi Mneka kutoka  chama cha muziki wa Reggae dansi nchini amewasihi na kuwaomba Watanzania kuacha  ushabiki wa makabila na badala  yake kushirikiana Kwa pamoja kuunganisha vionjo vya  makabila mbalimbali ili kutengeneza mdundo wa Taifa utakaotambulisha asili ya mtanzsnia katika mataifa mbalimbali Duniani 

"Watanzania wanatabia ya kuibua jambo lakini hatufiki mwisho hivyo tufanye vitu Kwa Makubaliano ambapo naisihi kamati yenu(kamati ya Mdundo wa Taifa) kuendelea kuifanya kazi hiyo iwe endelevu kulingana na mahitaji ya muziki wetu kwasasa ili kuendelea kuulinda Utamaduni wa kitanzania kupitia Sanaa hiyo ya Burudani."amesema Mneka.
Meneja wa Sisi Tambala Bendi Bw. Kibiriti akitoa maoni yake mbele ya wajumbe wa Kamati ya kutafuta Mdundo wa Kitaifa. 
Nae Meneja wa Sisi Tambala Bendi Bw. Kibiriti Nanjuja ameshauri kuwa ngoma za asili za makabila mbalimbali zenye vionjo vya kuvutia ndizo zitumike katika kutengeneza mdundo wa Kitaifa ,nakwama Jamii isipuuzie ngoma za asili kwani ndio utambulisho halisi wa Utamaduni wa Mtanzania kupitia Sanaa hiyo .

Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya mdahalo huo Makamu Mwenyekiti kamati ya Mdundo wa asili Tanzania Masoud Masoudi ambaye ni Manju Muziki amesema kwamba zoezi la kutengeneza mdundo wa Kitaifa unatokana na nia ya Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amenuia kulinda Mila na Tamaduni za Mtanzania kwani zimekuwa zikisahaulika tangu Tanzania ipate uhuru..

" Tumekubali kwa maoni ya wadau ambao wanaonekana wanakubaliana na dhana nzima ya Mdundo wa Taifa,wamekubali kwamba mdundo wa Taifa ni Muhimu,hivyo kuelewa mdundo wa Taifa ni hatua Moja kubwa sana" Amesema Masoud ambaye pia ni Mtangazaji wa TBC