Showing posts with label UCHUMI. Show all posts
Showing posts with label UCHUMI. Show all posts

Tuesday, April 10, 2018

NDANI YA MIEZI TISA TRA YAKUSANYA ZAIDI YA TRILIONI 10.


Katika kipindi cha miezi tisa ya mwaka wa fedha 2017/2018 Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imekusanya kiasi cha shilingi Trilion 11.78 ikilinganishwa na shilingi Trilion 10.86 ambazo zilikusanya kwa mwaka wa fedha 2016/17.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Bw. Richard Kayombo akiongea na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam.

Akiongea na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Huduma kwa Mlipa kodi wa TRA Bw. Richard Kayombo alisema kuwa ongezeko hilo ni sawa na ukuaji wa pato kwa asilimia 8.46

Aidha Mkurugenzi huyo alisema kuwa katika kipindi cha mwezi machi peke yake TRA imekusanya jumla ya shilingi Trilion I.54, ikilinganishwa na makusanyo ya mwezi machi 2017 ambapo ilikusanya jumla ya shilingi Trilion 1.34 ambapo ni ukuaji wa asilimia 14.49.

Kayombo aliendelea kusema kuwa mafanikio yote haya yanatokana na juhudi za walipa kodi, viongozi wa ngazi zote na kampeni kadhaa, pamoja walipa kodi wapya nchi nzima kuwakumbusha kulipa kodi kwa wakati na kusikiliza malalamiko yao pamoja na kuwajengea utaratibu mzuri wa kulipa madeni yao ya nyuma.
Mkutano ukiendelea.

"Katika kipindi hiki tunaendelea na usajili wa walipa kodi wapya wakiwemo wamachinga ambapo kwa wiki hii tupo mkoani Geita, na tunawakaribisha wafanyabiashara wote wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi na kupewa namba ya utambulisho ya mlipa kodi(TIN) na maafisa wa TRA watasikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi" alisema Kayombo


Na mwisho Mkurugenzi huyo alisema kuwa katika kuhakikisha huduma zinazotolewa ni bora, TRA inaendelea kutoa elimu kwa kila anayestahili alipe kodi kwa hiari na kwa wakati na mwenye malalamiko yoyote juu ya makadirio amuone meneja wa eneo husika akiwa na vielelezo vyake vyote.

Tuesday, February 20, 2018

KILICHOMKUTA ASKOFU KAKOBE BAADA YA KAULI YAKE KUWA YEYE ANA FEDHA KUIZIDI SERIKALI YA TANZANIA

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Bw. Charles Kichere akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata la Askofu Zachary Kakobe Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship kufuatia kauli yake kuwa “Yeye ana pesa kuliko Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”. kulia ni Bw. Richard Kayombo Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Walipa Kodi

Kufuatia kauliiliyotolewa na Askofu Zachary Kakobe wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship katika mahubiri ya Ibada ambayo alisema kuwa “Yeye ana pesa kuliko Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilifanya uchunguzi ili kubaini usahihi wa kauli hiyo.

Yafuatayo ni mambo ambayo yalibainika baada ya kufanyika uchunguzi kuhusu kauli ya Askofu Zachary Kakobe;

1.Askofu Zachary Kakobe hana akaunti wala fedha katika taasisi yoyote ya fedha hapa nchini. Aidha uchunguzi ulibaini kuwa Askofu Kakobe ni mmoja wa wasimamizi wakuu wa akaunti za kanisa (signatories) zilizopo katika benki ya NBC zenye jumla ya kiasi cha shilingi 8,132,100,819.00, kiasi hiki cha fedha kimetokana na sadaka, zaka na changizo ambazo zinatolewa na waumini wa kanisa tajwa hapo juu, hivyo kwa mujibu wa Sheria hakitozwi kodi.

2.Kanisa lilikwepa kulipa kodi kiasi cha shilingi 20,834,843.00 ambazo zilitokana na uwekezaji katika makampuni ya kukuza mitaji.Kodi hiyo imelipwa baada ya uchunguzi.

3.Kampuni inayomilikiwa na watoto wa Askofu Zachary Kakobe ilikwepa kulipa kodi kiasi cha shilingi 37,280,030.00 ambazo zimelipwa baada ya uchunguzi. Kwa ujumla, kiasi cha kodi kilicholipwa kutokana na uchunguzi huu ni shilingi 58,114,873.00.

4. Kanisa linatunza kiasi kikubwa cha fedha kwenye ndoo na ‘majaba’ kinyume na taratibu za utunzaji wa fedha, lakini pia uwekaji na utoaji wa fedha nyingi kutoka benki haushirikishi vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya usalama wa fedha zenyewe na wahusika.

5.Pia ilibainika kwamba Kanisa halitengenezi hesabu za Mapato na Matumizi ya Fedha kitu ambacho ni kinyume na Katiba ya Kanisa pamoja na sheria za usimamizi wafedha ambayo imepelekea matumizi mabaya ya fedha za waumini kama vile safari za nje ya nchi ambazo zimedhaminiwa na Kanisa lakini wanaosafiri ni Askofu na familia yake.  Vile vile fedha za Kanisa zinatumika kujenga nyumba ya mke wa Askofu, kwa jina lake na wala si kwa jina la Kanisa, kitu ambacho ni kinyume na taratibu za Kanisa.

Aidha, wakati uchunguzi huo ukiendelea,mnamo tarehe 24.01.2018 Askofu Kakobe aliandika barua kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuomba radhi kutokana na kauli yake ya kebehi pamoja na matamshi yake ya dharau kwamba ana pesa nyingi kuliko Serikali.

WITO:
•  Mamlaka ya Mapato Tanzaniainatoa wito kwa Taasisi zote za dini ambazo zinajihusisha na shughuli zozote za kiuchumi kulipa kodi stahiki na kwa wakati kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za kodi.

• Mamlaka ya Mapato Tanzania inazitaka Taasisi zote za kidini kufuata katiba zao ikiwa ni pamoja na kutengeneza hesabu za mapato na matumizi.

Charles E. Kichere
KAMISHNA MKUU 
MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA

Friday, December 1, 2017

MFUMO WA RAIS WA KUKUSANYA MAPATO KIELEKTRONIKI UMEPEISHA MAPATO YA KODI YA MAKAMPUNI YA SIMU KWA 102%


Mfumo wa Kukusanya Mapato Kielekroniki (eRCS) umeonyesha mafanikio makubwa kwa miezi mitatu ya mwanzo ya Julai, Agosti na Septemba 2017, baada ya Makusanyo ya Kodi kwa Upande wa Zanzibar (ZRB) kupitia eRCS kufikia Shilingi Bilioni.7.2, ukilinganisha na Shilingi Bilioni 3.5, ZRB walizokusanya kipindi Kama hicho mwaka 2016 kabla ya mfumo wa eRCS. Makusanyo hayo yakiwa ni Ongezeko la Shilingi Bilioni 3.6 sawasawa na asilimia102%. Ni zaidi ya Mara mbili ya makusanyo ya mwaka Jana kabla ya mfumo wa eRCS, yanayofikia shilingi Bilioni 7.2 ni majumuisho wa Ushuru wa Bidhaa (Excise Duty) na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) Baada ya kukata Marejesho.
Wakati huo huo Taarifa tulizonazo kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ni kwamba makusanyo ya kodi yanayotokana na kampuni za simu, kwa kutumia eRCS TRA wamefanikiwa kuongeza makusanyo kwa asilimia 21% kwa kukusanya Jumla ya shilingi Bilioni 128.9 kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai, Agosti na Septemba 2017, ukilinganisha na makusanyo ya miezi ya Aprili, Mei na Juni 2017 kabla ya kuanza kutumia mfumo wa eRCS. Aprili, Mei na Juni 2017 kabla ya eRCS, makampuni ya simu saba yalilipa jumla ya kodi ya Shilingi Bilioni 101.7. Julai, Augusti na Septemba 2017, baada ya kuanza kutumika eRCS, Makampuni ya simu yale yale yameweza kulipa Shilingi Bilioni 128.9. Kukiwa na ongezeko la Shilingi Bilioni 27.2 sawa na 21% ambazo ni majumuisho yaliyotokana na kodi ya Ongezeko la thamani (VAT) na Ushuru wa Bidhaa (Excise Duty).
Ukijumuisha makusanyo yanayotokana na Kodi kutoka kampuni za simu saba kuanzia mwezi Aprili 2017 mapaka mwezi Septemba 2017 TRA imekusanya Jumla ya Shilingi Bilioni 230.7. kwa kipindi cha miezi sita tu, ambazo ni wastani wa shilingi Bilioni 38.5 kwa mwezi. Taarifa tulizopata kutoka chanzo chetu ambao hawakutaka majina yao yatajwe wametueleza kwamba Serikali inafuatilia kwa kina udanganyifu unaofanywa na kampuni za simu katika Taarifa zao walizozipeleka TRA za input kwa ajili ya “return” ambazo zinakosa uhalisia kwani zinajumuisha taarifa za miezi iliyopita kwa lengo la kuongeza kiwango cha input tax.
Mfumo eRCS ulizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dkt. Mohamad Shein walipozindua Dirisha la kukusanya kodi Kielekroniki Elecrtronic Revenue Collection System (eRCS) tarehe 1 Juni 2017, ukiwa na lengo la kusaidia Mamlaka zote mbili za Mapato yaani Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRB) kuongeza mapato yanafanyika kupitia njia za kielektroniki. Mpaka Mwezi Novemba 2017, ni kampuni saba za simu ndizo zilizounganishwa katika mfumo wa eRCS, Kampuni hizo ni Vodacom, TTCL, Airtel, tiGO, Halotel, Zantel na Smart. Taarifa hii imeandikwa kutokana na taarifa zinazopatikana IDC, TRA na ZRB Novemba 2017.

Wednesday, November 29, 2017

SERIKALI YA AWAMU YA TANO YA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI YAFANIKIWA KATIKA UKUSANYAJI MAPATO KIELEKTRONIKI

Tangu kuzinduliwa Dirisha la Ukusanyaji Kodi kidigitali June mosi 2017 (Electronic Revenue Collection System - eRCS) ambalo lilizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Makamu wa Rais Mhe. Mama Samia Suluhu Hassani pamoja na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Mohamad Shein,  mawaziri kadhaa wa serikali za Muungano na serikali ya Mapinduzi; Kwa mara ya kwanza serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipatia bila bugudha Ushuru mkubwa wa bidhaa na kodi ya Ongezeko la Thamani zitokanazo na makampuni ya simu.
Mfumo huu uliosukwa na vijana wa Kitanzania wazalendo, umefanikisha kuongeza mapato litokanalo na mtandao (Ciber Space) kwa Zanzibar kwa 51% kwa robo ya tatu ya mwaka 2017 ukilinganisha na miezi kama hiyo 2016. Uchunguzi uliofanyika katika robo hiyo (tatu) ya mwaka 2017 (Julai,August na Septemba 2017), umebaini Zanzibar imelipwa kupitia mfumo wa eRCS Tsh Bil 7.2 ambayo imeongezeka kwa 51% ukilinganisha na miezi kama hiyo mwaka 2016 ambapo makusanyo ya jumla ya kodi yalikuwa  Tsh Bil 3.5 pekee.
Kwa mujibu wa vielelezo vya makusanyo wa TRA, miezi mitatu kabla ya mfumo huu kuzinduliwa rasmi (April,May na June); Makampuni ya simu yalilipa jumla ya kodi ya  Tsh Bil 101.7 lakini baada ya kuzinduliwa rasimi kwa mfumo huu wa eRCS na makampuni ya simu (TTCL, HALOTEL, AIRTEL, VODACOM, ZANTEL, SMART na TIGO) kuugwa ndani ya mfumo; Kwa kipindi cha miezi mitatu pekee ( Julai,Agost na Septemba 2017), yameweza kulipa kwa njia ya kielektroniki Tsh Bil 128.9 kukiwa na ongezeko la Sh Bil 27.2 sawa na 21% huku ongezeko la kodi ya thamani ikipanda kwa 9% yaani Tsh. Bil 4.7 sambamba na ongezeko la Ushuru wa Bidhaa 29% yaani Tsh. Bil 22.
Taarifa za kiuchunguzi zimebaini serikali inafuatilia kwa kina udanganyifu wowote utakao ama uliojitokeza kabla na baada ya mfumo hasa taarifa za makampuni ya simu katika matumizi yaoya kila mwezi.
Mpaka sasa, benk kadhaa nchini zimekamilisha taratibu za kuungwa katika mfumo huu na kuanza kulipa kodi kielectroniki.  Huu ni ushindi mkubwa kwa mkakati wa Rais Magufuli katika kupata njia bora za kukusanya mapato nchini. 
Ikumbukwe wajenzi wa mfumo huu ni vijana wazalendo walioaminiwa na serikali ili kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambazo zingetumika katika ujenzi wa mfumo huo kutumia wataalamu na makampuni ya kigeni.
Hivi ndivyo mapato yanavyoonekana katika Dashibodi ambazo viongozi wakuu wa nchi wanaona mapato yanavyokusanywa kielectroniki kwa kutumia mfumo  wa eRCS kila sekunde.
Jedwali hili linaonyesha  Mabenk yaanza kulipa baada ya yale yaliyokamisha kujiunga na ERCS ambyo ni BANK M na AMANA BANK Tanzania ina Mabenk zaidi  ya 20

Thursday, November 2, 2017

Mkutano wa Sekta ya Uziduaji Madini, Mafuta na Gesi 2017 waanza Mjini Dodoma

Mkutano wa siku mbili wa Sekta ya uziduaji (Madini, Mafuta na Gesi) 2017 umeanza hii leo Mjini Dodoma, ukishirikisha wadau mbalimbali ikiwemo asasi za kiraia, serikali pamoja na wanasheria kutoka ndani na nje ya nchi.

Mkutano huo unaoandaliwa na muunganiko wa asasi za kiraia nchini ambazo zinaangazia utawala bora katika sekta ya uziduaji HakiRasilimali, umelenga kujadili sera, sheria na mifumo ya uendeshaji katika sekta hiyo kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.

Akifungua mkutano huo, Padri Steven Munga alisema sekta ya uziduaji ni chachu ya maendeleo nchini hivyo inapaswa kuangaziwa vyema na hatimaye kuleta matokeo chanya kwa taifa.

Mwenyekiti wa Bodi ya HakiRasilimali, Donald Kasongi alisema mchango wa asasi za kiraia katika sekta ya uziduaji ni mkubwa hivyo asasi hizo zinapaswa kushiriki na kushirikishwa ipasavyo katika kuboresha sekta hiyo.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe alisema mkutano huo ni ishara kwamba suala la kuboresha sekta ya uziduaji si la Rais John Magufuli pekee bali pia asasi za kiraia kwani zina nafasi kubwa ya kuhakikisha rasilimali zilizopo nchini zinabaki kuwa utajiri na siyo laana kwa taifa.

Washiriki wa mkutano huo wametaka mazungumzo zaidi katika kuboresha sekta ya uziduaji nchini ili kuhakikisha inatoa matokeo chanya kwa taifa badala ya kutumia manufaa ya idadi kubwa ya wabunge bungeni kupitisha mikataba mibovu ambayo imeligharimu taifa.
Mgeni Rasmi, Padri Steven Munga akifungua mkutano huo
Mgeni Rasmi Padri Steven Munga (kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya HakiRasilimali, Donald Kasongi (katikati) pamoja na Mwanasheria Veronica Zano kutoka Zimbabwe (kushoto), wakiwa kwenye chumba cha mikutano baada ya ufunguzi wa mkutano wa uziduaji Mjini Dodoma
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe (kushoto) akizungumza na wanahabari kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa Bodi ya HakiRasilimali, Donald Kasongi (kulia) pamoja na Mwanasheria Veronica Zano kutoka Zimbabwe wakiwa kwenye mkutano huo
Mratibu HakiRasilimali, Rachel Chagonja kutoka akiwa kwenye mktano huo
Jenerali Ulimwengu ambaye ni mmoja wa watoa mada kwenye mkutano huo
Profesa Hamudi Majamba ambaye ni miongoni mwa watoa mada kwenye mkutano huo
Amani Mhinda ambaye ni mmoja wa watoa mada
Afisa Miradi kutoka shirika la HAKIZETU Jijini Mwanza, Gervas Evodius akifuatilia mkutano huo
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka Mwanza
Ashraf Omary ambaye ni Mkurugenzi wa shirika la METDO Tanzania akifuatilia mkutano huo
Washiriki mbalimbali wa mkutano huo

Monday, October 30, 2017

JUA KILICHOJIRI KATIKA SOKO LA HISA KWA WIKI ILIYOPITA

Haya ndiyo yaliyojiri kwenye soko la hisa kwa wiki iliyoisha Ijumaa tarehe 27 Oktoba 2017.

Mauzo ya Hisa (Turnover/ Liquidity)
Thamani ya mauzo ya hisa imepungua kutoka Shilingi Billioni 23 ya wiki iliyoishia 20 Oktoba 2017 hadi Shilingi Bilioni 20 kwa wiki iliyoishia 27 Oktoba 2017,
Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imepungua kutoka hisa Mil 2.8 ya wiki iliyoishia 20 Oktoba 2017 hadi hisa Mil 1.6 ya wiki iliyoishia 27 Oktoba 2017.
Kampuni zilizoongoza katika mauzo ya hisa ni kama ifuatavyo:
TBL…………………………………………99%
SWISS………………………………………0.4%
NMB………………………………………….0.2%
Ukubwa Mtaji (Market Capitalization)
Ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika soko umepungua kwa Shilingi Bilioni 432 kutoka Shilingi Trilioni 20.9 wiki iliyopita hadi Shilingi Trilioni 20.5 wiki iliyoishia tarehe 27 Oktoba 2017. Punguzo hilo limetokana na kupungua kwa bei za hisa za ACA(13%), KA (9%), TTP (8%), EABL (2%) na DSE (2%).
Ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umepungua kwa Shilingi Bilioni 2 kutoka Trilioni 10.165 hadi kafika Shilingi Trilioni 10.163 wiki hii. Hii ni kutokana na kupungua kwa bei ya hisa za TTP (8%) na DSE (2%).
Kampuni
27 October 2017            (Shilingi)
20 October 2017            (Shilingi)
Badiliko (%)
CRDB
                                  170
                                  170
0.00%
DCB
                                  385
                                  385
0.00%
DSE PLC
                               1,200
                               1,220
-1.64%
MBP
                                  600
                                  600
0.00%
MCB
                                  500
                                  500
0.00%
MKCB
                                  890
                                  890
0.00%
MUCOBA
                                  400
                                  400
0.00%
NMB
                               2,750
                               2,750
0.00%
PAL
                                  470
                                  470
0.00%
SWALA
                                  500
                                  500
0.00%
SWIS
                               3,500
                               3,500
0.00%
TBL
                             13,900
                             13,900
0.00%
TCC
                             15,600
                             15,600
0.00%
TCCL
                               1,200
                               1,200
0.00%
TOL
                                  780
                                  780
0.00%
TPCC
                               1,520
                               1,520
0.00%
TTP
                                  600
                                  650
-7.69%
VODA
                                  850
                                  850
0.00%
YETU
                                  600
                                  600
0.00%
Kampuni zilirodhodheshwa kutokea Masoko mengine



ACA
                               5,460
                               6,290
-13.20%
EABL
                               5,310
                               5,410
-1.85%
JHL
                             10,490
                             10,500
-0.10%
KA
                                  120
                                  110
9.09%
KCB
                                  820
                                  830
-1.20%
NMG
                               2,380
                               2,360
0.85%
USL
                                    80
                                    80
0.00%




Mtaji Jumla Makampuni yote (Bilioni)
                             20,455
                             20,887
-2.07%
Mtaji Jumla Makampuni ya Ndani (Bilioni)
                             10,163
                             10,165
-0.02%
Kiashiria cha DSEI (pointi)
                               2,124
                               2,172
-2.21%
Kiashiria cha TSI (pointi)
                               3,876
                               3,904
-0.72%

Viashiria (Indices)
Kiashiria cha kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimeshuka kwa pointi 48 kutoka pointi 2,172 hadi 2,124 pointi hii ikiwa ni kutokana na kushuka kwa bei za hisa za Acacia (ACA) kampuni Kenya Airways (KA), Tetepa (TTP) East African Breweries Ltd (EABL) na Dar es Salaam Stock Exchange Plc (DSE).
Pia kishiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimepungua kwa pointi 27 kutoka pointi 3,904 hadi pointi 3,876 kutokana na kushuka kwa bei za hisa za Tatepa na DSE Plc
Kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) kimepungua kwa pointi 1 kutoka pointi 5,380 hadi pointi 5,379
Kiashiria huduma za kibenki na kifedha (BI) kimeshuka kwa pointi 1 kutpka pointi 2,498 hadi pointi 2,497.
Kiashiria cha Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imebaki kama awali kwenye wastani wa pointi 2,462
Hati Fungani (Bonds)

Mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia tarehe 27 Oktoba 2017 yalikuwa Shilingi Milioni 500 kutoka Shilingi Bilioni 13 wiki iliyopita ya 20 Oktoba 2017

Mauzo haya yalitokana na hatifungani saba (7) za serikali na mashirika binafsi zenye jumla ya thamani ya Shilingi Milioni 600 kwa jumla ya gharama ya Shilingi Milioni 500