Showing posts with label TANZIA. Show all posts
Showing posts with label TANZIA. Show all posts

Wednesday, February 14, 2018

KIONGOZI WA CHADEMA AUWAWA NA MWILI WAKE KUTUPWA UFUKWENI MBOWE ATHIBITISHA HAPA.

MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kiongozi wa chama hicho katika Kata ya Hananasif, Daniel John amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Februari 13, 2018, Mbowe alisema John alitoweka siku moja iliyopita. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hana taarifa hizo lakini anawasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni.
 
Amesema baada ya mawasiliano atatoa ufafanuzi leo  Februari 14,2018. Mbowe alisema John ambaye ni katibu kata alitoweka akiwa na Reginald Mallya ambaye alijikuta yupo ufukweni mwa bahari.


Mbowe alisema walitoa taarifa polisi kuhusu kutoweka kwa John na kwamba, walipokwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) walielezwa kuna mwili ulipelekwa na polisi. 

Alisema mwili huo ulitambuliwa na mkewe John na una michubuko inayoashiria alikabwa, una jeraha la panga kichwani na upande mmoja wa kichwa umebonyea kuashiria alipigwa na kitu kizito.

Kuhusu Mallya alisema alipigwa panga kichwani na alivunjwa mkono. Mbowe ametaka polisi kufanya uchunguzi wa tukio hilo. Mallya aliyekuwapo kwenye mkutano huo na waandishi wa habari alisema walikuwa wakitembea na John ndipo waliposimamishwa na kuingizwa ndani ya gari.

Alisema alipigwa hadi kupoteza fahamu na alipozinduka alijikuta ufukweni alikojikokota hadi barabarani ambako alipata msaada wa bajaji na alikwenda Hospitali ya Mwananyamala alikotakiwa kuwa na taarifa ya polisi ambayo aliipata Kituo cha Polisi Oysterbay.

Thursday, January 4, 2018

MKE WA KINGUNGE AFARIKI DUNIA HUKU MUMEWE AKIWA AMELAZWA

Mke wa mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, Peras Kingunge amefariki dunia leo Alhamisi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mtoto wa Kingunge, Kinje Ngombale amethibitisha taarifa hizo na kwamba kifo cha mama yake kimetokea wakati baba yake pia ni mgonjwa.

"Ni kweli mama amefariki na baba amelala kwa sababu ndio kwanza ametoka chumba cha upasuaji aling'atwa na mbwa. Tutamwambia akiamka," amesema

Monday, January 1, 2018

MKE WA NAIBU WAZIRI LUGOLA, MARRY LUGOLA AFARIKI DUNIA

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),  Kangi Lugola amefiwa na mkewe Mary.
Image result for NAIBU WAZIRI LUGOLA
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais imesema Mary amefariki dunia leo Jumatatu Januari Mosi, 2018 jijini Dar es Salaam.

Imeelezwa utaratibu wa mazishi unaendelea kufanyika na taarifa zitatolewa baadaye.

Wakati huohuo, Ofisi ya Bunge katika taarifa kwa umma imesema Spika Job Ndugai amemtumia rambirambi Lugola kutokana na kifo cha mkewe.

Imeelezwa msiba upo Railway Club Gerezani jijini Dar es Salaam.

Ndugai ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa kumpoteza mpendwa wao.

Saturday, December 9, 2017

UMOJA WA MATAIFA HIVI NDIVYO ULIVYOLICHUKULIA TUKIO LA KUFA KWA WANAJESHI WA TANZANIA NCHINI CONGO

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali shambulio lililotekelezwa katika kambi ya walinzi wa amani iliyopo Semuliki, Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kupelekea vifo vya wanajeshi 20 huku wengine 53 wakijeruhiwa.
Image result for wanajeshi wa tanzania waliokufa congo
Kambi ya jeshi hilo la ulinzi wa amani (MONUSCO) ilishambuliwa Disemba 7 jioni na kupelekea vifo vya wanajeshi 15 wa Tanzania na 5 wa DRC.

Wajumbe hao wametuma salamu za pole kwa familia za wafiwa, serikali ya Tanzania na DRC lakini pia MONUSCO huku wakiwatakia majeruhi afya njema na wapone haraka.

Aidha, katika taarifa hiyo wajumbe hao wameeleza kuwa kushambulia kambi za walinzi wa amani ni tukio ambalo linachukuliwa kuwa ni uhalifu wa kivita katika sheria za kimataifa na kwamba wahusika hawawezi kusamehewa kwa matendo hayo.

Serikali ya DRC imetakiwa kuhakikisha kuwa wahusika wa tukio hilo wanakamtwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria na kutaka makundi yote ya kihalifu kusitisha mapigano.

Pia, wamewashukuru wanajeshi na watu mbalimbali ambao wanahatarisha maisha yao kila siku kwa ajili ya kuhakikisha amani inakuwepo duniani, na kwamba tukio kama hilo la kusikitisha linaikumbusha dunia kuwa ni kiasi gani watu hawa wameweka maisha yao hatarini kwa faida ya wengi.

Shambulio hilo la DRC ni kubwa zaidi kuwakumba walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa kwa miaka ya hivi karibuni.

Baraza la Usalama alimesema kwamba litaendelea kushirikiana kwa karibu na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa UN nchini DRC na MONUSCO kuhakikisha kuwa wanatekeleza ipasavyo malengo yao.

Wednesday, November 15, 2017

MUME WA ZAMANI WA UWOYA NDIKUMANA AFARIKI DUNIA JUA SABABU ZA KIFO CHAKE HAPA...

                                 Tokeo la picha la ndikumana
Aliyekuwa  mume wa muigizaji wa filamu nchini, Irene Uwoya, mchezaji Hamad Ndikumana (39) kutoka nchini Rwanda amefariki usiku wa kuamkia leo, chanzo cha kifo chake kikisemekana ni matatizo ya moyo ambapo jana alikuwa akiendelea na kazi zake kama kawaida.

Mpaka anakutwa na umauti alikuwa akicheza katika timu ya APOP Kinyras Peyias FC ya  Cyprus.  Alizaliwa Oktoba 5, 1978 na mpaka anafariki dunia alikuwa ametengana na Uwoya kwa mingi na alikuwa ndiye mkewe waliyefunga naye ndoa katika Kanisa Katoliki na walibahatika kupata mtoto mmoja  ambaye jina lake ni Krish.

Tuesday, October 10, 2017

MKUU WA SHULE AJINYONGA INGIA HAPA KUJUA SABABU ZA KIFO CHAKE

Mkuu wa Shule ya Sekondari Migukulama iliyopo Halmasahauri ya Buchosa wilayani Sengerema, Benerdicto Lweikiza (45) amejinyonga hadi kufa akiwa chumbani kwake.
      Image result for kitanzi
Taarifa za kujinyonga kwa mwalimu huyo zilianza kusambaa wilayani Sengerema na kuthibitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa wa Halmashauri ya Buchosa, Crispin Luanda.

“Ni kweli mwalimu huyo amejinyonga alikuwa mkuu wa Shule ya Sekondari Migukulama na amefikia uamuzi huo majira ya saa tisa mchana wa leo (jana) nyumbani kwake Mtaa wa Kilabela mjini Sengerema,” alisema Luanda.

Mmoja wa wanafamilia wa mwalimu huyo, Martin Kalemera alisema kuwa wao kama familia wanashangazwa na suala hilo na hawaamini kilichotokea ikiwa ni miaka mitano imepita tangu mke wake afariki dunia.

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole alithibitisha kupata taarifa ya kifo cha mwalimu huyo na kusema kuwa hajafahamu chanzo cha kufikia hatua ya kujinyonga na kamba chumbani kwake.

Alisema vyombo vya dola vinafuatilia kwa kina ili kubaini sababu.

Friday, September 29, 2017

KIONGOZI MWINGINE WA CUF AFARIKI DUNIA


Kiongozi wa CUF Mheshimiwa Ali Juma Suleiman ambaye alikuwa Kaimu Mwenyekiti wa (CUF) Jimbo la Mto Pepo na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa (CUF) Wilaya ya Magharibi A. Zanzibar amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Mnazi Mmoja.
Baadhi ya viongozi wa (CUF) na wanachama pamoja na wananchi wakiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja kufuatilia mwili wa Marehemu Ali Juma Suleyman.

Naibu Katibu Mkuu (CUF) Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema kuwa Mheshimiwa Ali Juma alikuwa amelazwa hospitali ya Mnazi Mmoja kufuatia kuvamiwa nyumbani kwake na kupigwa kisha baadaye kutupwa katika maeneo ya Masingini na makundi ya watu yanayoendesha vurugu Zanzibar.
"Nasikitika kutangaza kifo cha Mheshimiwa Ali Juma Suleiman, Kaimu Mwenyekiti wa CUF Jimbo la Mto Pepo na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF Wilaya ya Magharibi A. Amefariki dunia majira ya saa 4 usiku hapa jana hapa Mnazi Mmoja Hospital baada ya kupigwa vibaya na Mazombi juzi usiku" alisema Naibu Katibu Mkuu CUF Nassor Mazrui

Viongozi wa CUF wamesema kuwa mwili wa marehemu umeshafanyiwa uchunguzi tayari na sasa wamekabidhiwa kwa ajili ya kufanya mazishi ambayo yatafanyika leo katika makaburi ya Mwanakwereke, nje kidogo ya mji wa Unguja.  
Inna Lilahi Wa Inna Ilayhi Rajiuun

Saturday, September 2, 2017

BI. HINDU KUZIKWA KESHO MAKABURI YA KISUTU

Naibu Katibu Mkuu wa CUF, upande wa Profesa Ibrahim Lipumba, Magdalena Sakaya amesema chama hicho kimepokea kwa masikitiko kifo cha Mbunge mteule wa Viti Maalum Hindu Mwenda.
Hindu alifariki dunia ghafla jana nyumbani kwake Kibada Kigamboni na anatarajiwa kuzikwa kesho saa 7 mchana katika makaburi ya Kisutu wilayani Ilala,  Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza, leo Jumamosi Septemba 2 Sakaya amesema  Hindu alikuwa ni mpambanaji  na mtu mwenye kukijenga chama hicho  kuanzia miaka ya 90  hivyo ni pigo kubwa kuondoka kwake.

‘’Hata ukifika  Tabora leo hii hakuna mwanachama wa CUF asiyemjua Hindu’ ’amesema Sakaya.
“Sijui niseme nini maana zilikuwa zimebaki siku chache tu aende Dodoma kuapishwa baada ya kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) mwezi uliopita,” amesema Sakaya ambaye pia ni Mbunge wa Kaliua Tabora.

Friday, July 21, 2017

PICHA - MAZISHI YA MAMA YAKE NA ZARI THE BOSS LADY









Waombolezaji wakiswali msibani.
Mama mzazi wa Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’Halima Hassan aliyefariki dunia jana asubuhi, baada ya kuugua kwa wiki kadhaa na kulazwa hospitali alitarajiwa kuzikwa leo katika Kitongoji cha Munyonyo, Kampala.


Kina mama wakiomboleza.
Alhamisi iliyopita Gazeti la Amani liliripoti hali ya ugonjwa ya mama huyo kutokuwa nzuri baada ya kudaiwa kupumulia mashine ya oksijeni kwenye Kitengo cha Wagonjwa Mahututi (ICU) katika Hospitali ya Nakaseroiliyopo nchini Uganda akisumbuliwa na maradhi ya moyo na figo ambayo yamekuwa yakimsumbua tangu kufariki kwa mkwe wake, Ivan Ssemwanga.



Hali ilivyokuwa nyumbani kwa mama Zari.
Kwa mujibu wa chanzo ndani ya familia hiyo, mama Zari alipata matatizo ya moyo na figo baada ya kuanguka ghafla na kichwa chake kujigonga, hali iliyosababisha akimbizwe hospitalini haraka.



Kaburi ambamo mwili wa marehemu utazikwa.
Kifo cha mama Zari ambaye alizaliwa Mei 15, 1959, kimekuja ikiwa ni takribani miezi miwili tu tangu mkwe wake, Ivan Semwanga, aliyeaga dunia Mei 25 mwaka huu huko Steve Biko Academic Hospital nchini Pretoria, Afrika Kusini.



Maombolezo yakiendelea.
Waombolezaji wamefurika nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya kushiriki mazishi ya mama huyo ambaye amekuwa maarufu Afrika Mashariki na Kati kupitia kwa mwanaye Zari.


Chakula kikipakuliwa.



Dada wa Zari, Zuleha Hassan akiomboleza kifo cha mama yake.



Jeneza lenye mwili wa marehemu likishushwa kwenye gari.



Jeneza likipelekwa eneo maalum kwa ajili ya kuagwa na kufanya taratibu za mazishi.



Ndugu wa marehemu wakilia kwa uchungu.



Swala kwa ajili ya marehemu.



Kundi la matajiri lijulikanalo kama Rich Gang wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu.



Mmoja wa waombolezaji akigonga pilau.