Friday, September 23, 2016

MANENO YA LOWASA BAADA YA KUTEMBELEA WAHANGA WA TETEMEKO LEO

Ijumaa ya Septemba, 23 aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya CHADEMA, Edward Lowassa amewasili mkoani Kagera kwa ajili ya kuwajulia hali waathirika wa tetemeko la ardhi ambalo lilitokea Septemba, 10 mwaka huu.Baada ya kuona hali ilivyo sasa kwa baadhi ya wakazi wa mkoa huo kupoteza ndugu zao, nyumba na mali zao kuharibika, Lowassa ametumia ukurasa wake wa Twitter kufikisha ujumbe kwa jamii ya watanzania sehemu yoyote walipo duniani kote.
Ujumbe wa kwanza Lowassa aliandika “Poleni ndugu zangu Wa Kagera na mlioathirika na tetemeko, Tupeane nguvu ili tuvuke katika kipindi hiki kigumu pamoja”
Na ujumbe wa pili Lowassa aliandika “Nawasihi watanzania wenzangu tuendelee kujitolea kuwasaidia wahanga kama ilivyo desturi ya umoja wa kitaifa tulionao”lowassa-kagerall


YANGA, JKT RUVU SASA KUCHEZA OKTOBA 26


Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imepanga mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Young Africans dhidi ya JKT Ruvu, sasa utachezwa Oktoba 26, 2016 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar s Salaam.

Pamoja na mchezo huo, imefanya mabadiliko katika baadhi ya ya michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom kama ifuatavyo ambako Mwadui na Azam sasa utachezwa na Novemba 9, 2016 siku ambayo Prisons itaikaribisha Simba kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Novemba 10, kutakuwa na mchezo kati ya Young Africans dhidi ya Ruvu Shooting jijini Dar es Salaam.

KILIMANJARO QUEENS NEEMA TUPU


Ubingwa Kombe la CECAFA Chalenji kwa timu za mpira wa miguu za wanawake katika nchi za Afrika Mashariki, umewavutia wadau wengi kwa kiwango kikubwa hivyo kushusha neema kwa wachezaji hao wa timu ya taifa ya Tanzania Bara maarufu kama Kilimanjaro Queens ambayo imeandika historia ya kutwaa taji hilo ikiwa ni taifa la kwanza katika mashindano hayo mapya.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amefurahishwa na ubingwa wa timu hiyo akisema: “Si ubingwa tu, bali umefuta dhana ya Wakenya ambao siku zote wamekuwa wakitangaza Mlima Kilimanjaro uko kwao Kenya wakati upo hapa Tanzania. Kwa kuifunga Kenya, mmefanya kazi nzuri.”

TSN YADHAMINI MECHI YA BONGO MOVIE NA BONGO FLAVA KUCHANGIA WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI BUKOBA


Mkuu wa kitengo cha Masoko na Biashara TSN, Jahu Mohammed Kessy akiwakabidhi wasanii jezi kwa ajili ya mechi ya kuchangia maafaa ya tetemeko la ardhi Bukoba
Kampuni ya TSN  Kwa kushirikiana na Wasanii wa bongo fleva na bongo Movie wamejitokeza kuwezesha mechi maalum kuchangia wahanga wa Tetemeko la Ardhi lililotokea Bukoba mkoani Kagera.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Biashara Jahu Mohamed Kessy, amesema TSN imejitokeza kudhamini mechi hiyo itayofanyika uwanja wa taifa, jumaapili tarehe 25 september, na hivyo kuwataka wananchi, mashirika na kampuni mengine binafsi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuchangia na kuwezesha misaada kwa wananchi wa Kagera waliopata maafa kutokana na tetemeko hilo la ardhi.


Alisema wao kama TSN wameguswa na janga hili na hivyo mbali na michango yao mingine ya moja kwa moja wameona umuhimu wa kushirikiana na wasanii wa bongo fleva na bongo movie kuhamasisha uchangiaji huo kwa pamoja ilikuweza kuwashirikisha na wengine.


“TSN, Tanzania sisi Nyumbani, tunaunganisha nguvu ya wasanii hawa kutoka katika tasnia hizi mbili tofauti  kwa lengo la kuhamashisha uchangiaji wa pamoja,”

Alisema mechi hiyo inatazamiwa kuchezwa saa tisa mchana katika uwanja huo wa Taif

Tigo yatoa simu 800 zenye thamani ya 120m kusaidia zoezi la kusajili watoto chini ya umri wa miaka mitano katika mikoa ya Njomba na Iringa.


Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Nyanda za juu Kusini Jackson Kiswaga akipeana mkono na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dr Rehema Nchimbi mara baada ya kutoa hotuba wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya zoezi la usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa, uzinduzi huo ulifanyika jana mjini Iringa.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dr Harrison Mwakyembe akionesha mojawapo ya simu 800 zilizotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ili kufanikisha zoezi la usajili na utoaji wa vyeti kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, uzinduzi wa zoezi hilo kwa awamu ya tatu ulifanyika jana mjini Iringa. Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza.

STARTIMES KUWAPAMBANISHA 18 FAINALI ZA SHINDANO LA VIPAJI VYA SAUTI KESHO JIJINI DAR ES SALAAM


Mtengenezaji wa Sauti katika chaneli ya StarTimes Kiswahili, Tracy Luo (katikatio) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza kufanyika kwa fainali za shindano la vipaji vya sauti litakalofanyika kesho katika ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kushoto ni mshiriki wa shindano hilo kutoka Zanzibar,  Safiya Ahmed na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Masoko wa kampuni hiyo, Damien Li. Washiriki 18 kati ya 547 wameingia hatua ya fainali ambapo washindi 10 watajipatia fursa ya kwenda kufanya kazi makao makuu ya StarTimes yaliyopo Beijing, China.

 Mshiriki Safiya Ahmed kutoka Zanzibar (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Mtengenezaji wa Sauti katika chaneli ya StarTimes Kiswahili, Tracy Luo.
Mshiriki Hilda Malecela kutoka Dar es Salaam (kulia), akizungumza na wanahabari katika mkutano huo.
Mshiriki kutoka mkoani Arusha, Mathew Mgeni (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni mshiriki Hilda Malecela kutoka Dar es Salaam.
Taswira meza kuu kwenye mkutano huo.
Washiriki wa shindano hilo. Kutoka kulia ni Safiya  Ahmed kutoka Zanzibar, Mathew Mgeni kutoka Arusha na Hilda Malecela kutoka Dar es Salaam

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU WATAALAMU SABA KWENDA INDIA KUJIFUNZA UPANDIKIZAJI WA KIFAA CHA USIKIVU (COCHLEA IMPLANT)Hospitali ya Taifa Muhimbili inaendelea kutekeleza azma ya Serikali ya kupunguza idadi ya wagonjwa wanaokwenda kutibiwa nje ambao mara nyingi walikuwa wakifuata matibabu yasiyopatikana hapa nchini ama kutokana na kutokuwepo wataalamu au ukosefu wa vifaa vya kutolea huduma husika.

Katika kutekeleza hilo, Septemba 25, 2016, Hospitali ya Taifa Muhimbili itapeleka watalaamu saba nchini India katika Hospitali ya Apollo iliyopo New Delhi ili wakajifunze kwa njia ya vitendo jinsi ya kufanya upasuaji na upandikizaji wa kifaa cha usikivu kwa watu wazima na watoto. 

MEYA WA DAR ISAYA NWITA ASHAURI WATANZANIA KUJENGA UTAMADUNI WA KUTUMIA BIDHAA ZA NGOZI ZA HAPA NCHINI

Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akipata maelekezo kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kemange iliyopo Buhemba Wilayani Tarime Mkoani Mara kwenye darasa ambalo alisoma. Shule hiyo inahitaji ukarabati wa vyumba 9 vya madarasa

Thursday, September 22, 2016

AHADI MPYA-DARAJA LA SALENDA SASA UJENZI KUANZA MWAKANI MARA MOJA,MTIZAME MH RAIS HAPA


Kampuni ya Tigo yaendelea na utoaji wa madawati mikoani

Baadhi ya wananfunzi katika shule ya msingi Mandela wakiwa wameketi katika Madawati mapya yaliyotolea na kampuni ya Mawasiliano ya Tigo.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Saidiki akikabidhi Madawati kwa walimu wakuu,Peggy Staki wa shule ya msingi Mandela (kulia) na Peter Njau wa shule ya msingi Mrumeni wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada huo iliyofanyika katika shule ya msingi Mandela mjini Moshi.

Baadhi ya Wananfunzi katika shule ya Msingi Mandela wakiwa wamekaa kwenye Madawati yaliyotolewa na kampuni ya Tigo ikiwa ni kuiikia wito wa rais John Magufuli katika kutekleza sera ya elimu bure. 

Majengo ya shule ya Msingi Mandela. 

WAZIRI WA UJENZI PROFESA MBARAWA ATAKA WADAU WA UJENZI WALA RUSHWA WAFUTIWE LESENI ZAO

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa, Makame Mbarawa (kushoto), akihutubia wakati akifungua Semina ya 26 ya utoaji elimu endelevu kwa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Dar es Salaam leo asubuhi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Ambwene Mwakyusa akizungumza katika semina hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa, Makame Mbarawa (kushoto), akipeana mkono na Msaji wa Bodi hiyo Jehad Jehad baada ya kumaliza kutoa hutuba yake.
Wadau wa sekta ya ujenzi wakiwa kwenye semina hiyo.

Wadau wa sekta ya ujenzi wakiwa kwenye semina hiyo.

Taswira meza kuu katika semina hiyo.

Picha ya pamoja na mgeni rasmi Waziri Mbarawa.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi, Waziri Mbarawa (aliyekaa katikati), Wengine kutoka kulia waliokaa ni Mkurugenzi wa Huduma na Ufundi kutoka Wizara ya Ujenzi, Profesa Mhandisi William Nshana, Mwenyekiti wa Bodi, Ambwene Mwakyusa, Msajili wa Bodi, Jehad Jehad na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili, Dk.Adelina Kikwasi.

MTAA WA MASAKI JIJINI DAR ES SALAAM WAANZISHA TOVUTI YAKE KWA AJILI YA MAENDELEO

 Mwenyekiti wa Mtaa wa Serikali ya Mtaa wa Masaki jijini Dar es Salaam, Kimweri Mhita (kulia), akizungumza katika na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa Tovuti ya mtaa huo iliyofanyika Hoteli ya Best Western Plus Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Msasani, Benjamin Sitta. 
 Mwenyekiti wa Mtaa wa Serikali ya Mtaa wa Masaki jijini Dar es Salaam, Kimweri Mhita, akitoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya tovuti hiyo.
 Katibu Tarafa ya Magomeni, Fullgence Sakafu (katikati), akikata utepe kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kionondoni, aliyekuwa mgeni rasmi, kuashiria uzinduzi rasmi wa tovuti hiyo. Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Msasani, Benjamin Sitta, Mwenyekiti wa mtaa huo, Kimweri Mhita, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Masaki, Richard Mwakyulu na Mjumbe wa Kamati ya Mtaa huo, Rose Mkisi.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea kabla ya uzinduzi huo.
 Wajumbe wa kamati ya mtaa huo wakishiriki kwenye uzinduzi huo.
 Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo,  Peter Mkongereze akizungumza kwenye hafla hiyo.
 Diwani wa Kata ya Msasani, Benjamin Sitta (kulia), akizungumza katika hafla hiyo.
 Mmoja wa waendeshaji wa tovuti hiyo, Benjamin Chaula (kulia), akielezea jinsi itakavyokuwa ikifanya kazi.Kushoto ni Norbert Baranyikwa.
 Makofi yakipigwa baada ya uzinduzi wa tovuti hiyo.
Katibu Tarafa ya Magomeni, Fullgence Sakafu (kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo.

KILIMANJARO QUEENS KUTUA SAA 12.05 JIONI, SERENGETI BOYS YATUA


Mabingwa wapya wa Kombe la Chalenji la CECAFA, timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania Bara maarufu kwa jina la Kilimanjaro Queens, sasa itatua jijini Dar es Salaam leo Septemba 22, 2016 saa 12.05 jioni (18h05) kwa ndege ya FastJet ikitokea Mwanza.

Hii Ndiyo Agenda inayojadiliwa UN kuhusu Malalamiko ya Maalim Seif wa CUF huko Zanzibar


ZIARA ya kimataifa aliyoifanya Maalim Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Marekani, Ulaya, Canada na Umoja wa Mataifa kulalamikia uvurugaji wa uchaguzi mkuu wa 25 Oktoba mwaka jana, imeanza kuzaa matunda,

Tayari taasisi ya kimataifa ya umoja wa wanaliberali – Liberal International (LI) – imeliandikia Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC) kutaka kutolewa kwa vikwazo dhidi ya Serikali ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana kwenye tovuti ya LI, taasisi hiyo imetaka baraza hilo lenye jukumu la kulinda misingi ya haki za binadamu kwenye mataifa yote wanachama wa UN, kuchukua hatua kali ili kukomesha “uvunjaji mkubwa wa haki za binaadamu na ukandamizaji wa haki za kisiasa na kiraia visiwani Zanzibar.”
ya kupinga walichokiita “uonevu wanaofanyiwa viongozi wa upinzani Zanzibar na wafuasi wao.”

“Tunaitaka serikali ya Zanzibar na Tanzania kuheshimu utawala wa sheria na kuingia katika majadiliano na upinzani ndani ya muda maalum hatua ambayo itawezesha kuundwa serikali ya mpito na kukubali kuitishwa kwa uchaguzi mpya ili kuondoa mgogoro uliojitokeza baada ya kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa 25 Oktoba 2015,” imesema taarifa ya LI

TAMKO RASMI LA LHRC KUHUSU SIKU YA AMANI DUNIANI


ACT-WAZALENDO WASOGEZA MBELE MKUTANO WAKE,HII NDIYO TAREHE RASMI,NA SABABU ZAO

1.    Katika kikao chake cha tarehe 05 Septemba 2016, pamoja na mambo mengine, Kamati Kuu ya Chama cha ACT Wazalendo iliazimia kuwa Chama kifanye Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia (National Democratic Congress) tarehe 24 Septemba 2016 jijini Dar es Salaam.
  2Tangu kutangazwa kwa umma kuhusu mipango ya kufanyika kwa mkutano huu, wanachama wetu wengi na wananchi kwa ujumla, wakiwemo baadhi kutoka mikoani wameonesha nia ya kushiriki. Ili kuwapa fursa viongozi, wanachama na wananchi kushiriki kwenye mkutano huu, Chama kimesogeza mbele tarehe ya kufanyika kwake hadi tarehe 08 Octoba 2016.


3.    Wanachama na wananchi ambao wangependa kushiriki kwenye mkutano huu watume majina yao na majimbo wanayotoka kwa namba  0653619906/0717047574. Ili kutoa muda wa kutengeneza vitambulisho vya washiriki, siku ya mwisho ya kupokea majina ya washiriki ni tarehe 01 Septemba 2016.

4.    Ikumbukwe kuwa mbali na kujadili masuala mbalimbali ya nchi na bara la Afrika, Mkutano wa Kidemokrasia ndiyo fursa pekee ya kikatiba ambapo mwanachama/mwananchi wa kawaida anayeshiriki anapata fursa ya kuwahoji ana kwa ana viongozi  wa kitaifa wa ACT Wazalendo juu ya masuala mbalimbali ya Chama.

Ado Shaibu
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma
Imetolewa leo tarehe 21 Septemba 2016.

Wednesday, September 21, 2016

Kampuni ya Tigo yakabidhi madawati 435 mkoani Tanga leo


Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani, Goodluck Charles akiongea na wanahabari na wanafunzi ya shule ya msingi Mabawa leo, kwenye hafla ya kukabidhi madawati. Kushoto kwake ni mkuu wa wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa, Katibu tawala wilaya ya Tanga Bi. Faidha Salim na kushoto ni Meneja wa Tigo mkoani Tanga, Patricia Sempinge
Katibu tawala wilaya ya Tanga Bi. Faidha Salim akiongea na wanahabari na wanafunzi ya shule ya msingi Mabawa leo, kwenye hafla ya kukabidhi madawati. Kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe. Thobias Mwilapwa, Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani, Goodluck Charles na Meneja wa Tigo mkoani Tanga Patricia Sempinge. Na kushoto kwake mwalimu mkuu Zuwena Msembo.
Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe. Thobias Mwilapwa (kulia)akipokea  dawati toka kwa mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani, Goodluck Charles(kushoto). Katikati ni mwalimu mkuu wa shule ya mabawa, Zuwena Msembo, Jumla ya madawati 435 yenye thamani ya shilingi milioni 72  yalitolewa na kampuni ya Tigo mkoani Tanga kwenye hafla iliyofanyika shule ya msingi Mabawa leo.
Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe. Thobias Mwilapwa (kulia) akiwa ameketi na mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani(mwenye miwani) na wanafunzi  Amir Kibwana na Pili Ali(kushoto) wa shule ya msingi Mabawa, mara baada ya kampuni ya Tigo kukabidhiwa  435 yenye thamani ya shilingi milioni 72 kwa mkoa wa Tanga leo.
Wanafunzi wa shule ya msingi Mabawa mkoani Tanga wakiwa wameketi kwenye madawati .waliyokabidhiwa na kampuni ya Tigo leo