Thursday, April 30, 2015

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MAY 01.2015 YAKO HAPA

HABARI NYINGINE KUTOKA HAI IKO HAPA


kaika picha ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Ndg Antony Mtaka akizungumza katika uchaguzi wa wajumbe wa bodi ya maji ya Lyamungo Umbwe


myenyekiti mpya wa bodi ya Maji ya Lyamungo Umbwe Michael Sitaki Mmasi
Mhandisi wa maji wilaya ya Hai Eng. Nyakaraita Mwita akizungumza na wajumbe wa mkutano wa bodi ya Maji ya Lyamungo Umbwe.

BODI YA AFYA WILAYA YA HAI YATOA RIPOTI YAKE OKTOBA 2010 HADI 2014 HAI

IMEELEZWA kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zilizopo katika hosipitali ya Wilaya ya Hai Bodi ya Afya wilayani hapo imeweza kufanya kazi ya kuziondoa changamoto hizo ili wananchi waweze kupokea humuda ya afya kwa njia stahiki.

 Hayo yameelezwa hii leo na Mganga Mkuu Wa Hosipitali ya Wilaya Paul Chaote katika mkutano wa Bodi ya Afya ulio ambatana na uteuzi wa Mwenyekiti Mpya wa kuongoza Bodi hiyo kutokana na Mwenyekiti aliye kuwa madarakani kumaliza muda wake kutokana na utaratibu uliowekwa kumalizika.

 Amesema kuwa Bodi ya afya ya Wilaya inayomaliza kipindi chake ilisimikwa na kuanza kazi rasmi mwezi oktoba mwaka 2010 lengo ikiwa ni kufanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu lakini kutokana na kuchelewa mchakato wa uchaguzi wa wajumbe wapya,Bodi hii iliendelea kuwapo madarakani kwa kipindi cha mwaka mmoja zaidi.

Aliongeza kuwa Katika kipindi cha miaka minne bodi kwa kushirikiana na timu ya uendeshaji shughuli za afya pamoja na Menejimenti ya Halmashauri ilifanya mambo mbalimbali ikiwamo Kuongeza wigo wa huduma katika hosipitali ya wilaya kwa kufanya upanuzi kutoka majengo 7 mwaka 2010 hadi majengo 11 mwaka 2014.

Chaote aliongeza kuwa mambo mengine ni pamoja na Kufanya ukarabati katika vituo vya Afya na Zahanati,Kuongeza vituo vya hiduma toka 60hadi 62,Kufanya ziara elekezi za usimamizi katika hosipitali ya Wilaya nay a Machame,Vituo vya Afya na Zahanati na Kuingia mikataba 3 ya kiushirikiano kuendesha vituo vya makanisa ikiwa ni pamoja na hosipitali teule ya Machame.

 Pia tumeweza ku Kufanya uhamasishaji wa mfuko wa afya ya jamii katika mikutano ya wananchi,mikusanyiko ya watu kama masokoni,makanisani na misikitini,katika shule za sekondari na kuongeza wanachama kutoka kaya 854 mwaka 2010 hadi kaya 5,028 mwaka 2014,Kufungua akaunti katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya vya Serikali.

 "Ni jambo la kunivunia kuona kuwa licha ya changamoto nyingi zinazo jitokeza ndani ya hosipitali yetu na vituo vingine fya Afya bado Bodi ya Afya imeweza kutoa huduma kwa wananchi pamoja na kuwaelimisha kuhusu bima za afya ili kila kaya iweze kupokea matibabu yaliyo bora kpitia bima ya Afya."Alisema Chaote.

Alisema kuwa mbali na mafanikio hayo yote pia wameweza kukabiliana na changamoto mbali mbali ikiwemo uchangiaji mdogo wa wananchi katika masuala ya mfuko wa afya ya Jamii ambapo lengo la kitaifa ifikapo disemba 2015 ni 30% wakati wilayaya Hai bado ni 10%tu,uchakavu wa majengo katika baadhi ya vituo,ukosefu wa huduma za maabara katika zahanati za Serikali ukosefu wa baadhi ya huduma muhimu katika Hosipitali ya Wilaya kama nishati mbadala wakati umeme wa Tanesco unapo katika.

 "Tunaamini kwamba Bodi hii iliyo undwa itasimamia kamati zote zilizoko chini yake na itahakikisha kuwa huduma za Afya katika Wilaya yetu zitaboreshwa katika viwango vinavyopendekezwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.Nina kuomba sasa uzindue rasmi Bodi hii ambayo itafanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu."alisema Chaote.

 HABARI KATIKA PICHA WAKATI WA UPIGAJI KURA WA KUCHAGUA MWENYEKITI NA WAJUMBE WA BODI MPYA YA MAJI HAI.

Mganga Mkuu wa Hosipitali ya Wilaya ya hai Paul Chaote aliye simama akizungumza jambo wakati wa kikao cha kuchagua wajumbe wa Bodi ya Afya Wilaya.

Wajumbe wa Bodi ya Afya Wilaya wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Hosipitali ya Wilaya Hai

Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Afya Wilaya  katikati Bw Inocavity Swai akisikiliza maelezo mara baada ya upigaji kura kumalizika.

KIMEELEWEKA--UKAWA WATOKA CHIMBO MUDA HUU,SOMA WALICHOAMUA SASA

Viongozi wakuu wa vyama vikuu vya upinzani UKAWA wakiwasili makao makuu ya CUF kwa ajili ya kuzungumza na wanahabari leo
Hatimaye viongozi wa vyama vikuu vya upinzani vinavyounda  UKAWA wameibuka upya na kutangaza rasmi kutokuwa na kutokuwa na imani na tume ya taifa ya uchaguzi nchini kwa kudai kuwa serikali ya chama cha mapinduzi inaitumia tume hiyo kutaka kusogeza uchaguzi mbele kwa lengo la kujiongezea muda wa kutawala.


Akisoma maadhimio ya umoja huo baada ya kukutana ndani ya siku mbli jijini Dar es salaam mwenyekiti mwenza wa umoja huo ambaye ni mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi mh JAMES MBATIA amesema kuwa kutokana na hali ya hewa inayoendelea kuhusu sintofahamu ya daftari la kupiga kura ni wazi kuwa sasa umoja wao hauna inami hata kidogo na tume ya uchaguzi kwani imeonyesha wazi kuwa inashirikiana na serikali ya chama cha mapinduzi kutaka kuhujumu uchaguzi ujao na kisha kuongeza muda wa uongozi wa serikali hiyo kwa kisingizio cha kutokumalizika kwa uandikishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Amesema kuwa tume ya taifa ya uchaguzi hadi sasa ikiwa imesalia takribani miezi mitatu pekee kuanza kwa kampeni rasmi za uchaguzi haijaanza wala hakuna dalili za maandalizi yoyote ya kufanyika kwa uchaguzi huo jambo ambalo linazidi kuleta wasiwasi kwa watanzania na kuamini kuwa kuna njama za kuahirisha uchaguzi huo kama ilivyofanyika kwa daftari la kudumu la wapiga kura.


“kuna jambo linashangaza sana,hadi sasa hakuna maandalizi yoyote yanayoashiria kuwepo kwa uchaguzi huo ilihali imebaki miezi sita tu kufanyika kwa uchaguzi huo,hakuna utaratibu wa vifaa vya uchaguzi huo,ambapo miaka iliyopita imekuwa ikifanyika maadalizi mwaka mmoja kabla lakini uchaguzi huu hadi leo hakuna maandalizi ya kuonyesha kuwa uchaguzi huo upo japo kuwa mwenyekiti wa tume hiyo anazidi kuwdanganya watanzania kuwa uchaguzi huo upo”.aliseama mh MBATIA.
Naye mwenyekiti wa CHADEMA mh FREMAN MBOWE amesema kuwa hakuna njia yoyote ya kuzia mabadiliko ambayo yanataka kufanywa na ukawa kwa sasa hivyo tume hiyo isikubali kutumika na serikali na badala yake ni lazima uchaguzi ufanyike mwaka huu kwa njiia yoyote.


MGOGORO KUHUSU MAJIMBO

Wednesday, April 29, 2015

TIZAMA ALICHOKIFANYA DC MAKONDA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, wakati akipokea msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 50 kutoka Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN) wa ajili ya mashindano ya Kinondoni Cup yatakayoanza Juni 2015 katika wilaya hiyo.

DK.SHEIN AZINDUA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MKOA WA RUVUMA APRIL 29, 2015.

1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwasha mwenge wa Uhuru Kitaifa katika uwanja wa Majimaji Songea Mkoa wa Ruvuma leo(kushoto) Waziri wa Vijana Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara na Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa jamii vijana wanawwake na watoto Bi Zainab Mohammed.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA DHARURA WA VIONGOZI WA NCHI NA SERIKALI WANACHAMA WA SADC KUHUSU UENDELEZAJI VIWANDA, HARARE ZIMBABWE.

UMESKIA NCCR KUJITOA UKAWA--TAARIFA MPYA HII HAPA

VIONGOZI  wa Vyama Vikuu vya Upinzani vinavyounda (UKAWA) Vimekanusha Uvumi unaoenezwa na Vyombo vya Habari kuwa Miongoni mwa Chama cha siasa kinachounda umoja huo ambacho ni NCCR Mageuzi  kwamba kimetoa hoja ya kujitoa kwenye umoja Huo, na  kusema huo ni upotoshaji Wa Vyombo vya Habari ambavyo vinatumiwa na Chama cha Mapinduzi CCM.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
        
Kauli hiyo ya (UKAWA) inakuja ikiwa ,Gazeti la moja linalotoka kila siku Gazeti la Mtanzania toreo la leo Tarehe 29-mwezi wa nne mwaka huu bila ya kutaja chanzo cha uhakika kimeripoti Habari kwamba Vyama hivyo vikuu vya Upinzania vimeshindwa kufikia muhafaka kwenye ugawaji wa Majimbo  na kudai kwamba Chama cha NCCR mageuzi kimepeleka hoja ya kujitoa kwenye Umoja huo.
         

WAZIRI WA MEMBE AKUTANA NA RAIS MSTAAFU WA MAREKANI BILL CLINTON JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe Membe akimkaribisha Rais Mstaafu wa Marekani Mhe Bill Clinton Ikulu jijini Dar es salaam Aprili 28, 2015. Rais huyo wa 42 wa Marekani yuko nchini kukagua miradi ya maendeleo na afya inayofadhiriwa na taasisi za Clinton Development Initiative (CDI) na Clinto Health Access Initiative (CHAI).

LHRC-SERIKALI IACHE MARA MOJA KUIPIGIA KAMPENI KATIBA PENDEKEZWA

Mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho  Bi HELLEN KIJO BISIMBA Akizngumza na wanahabri leo jijini  Dar es salaam kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu mchakato wa kura y7a maoni juu ya katiba pendekezwa
 Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini LHRC kimesema kuwa kitendo cha serikali kuanza kupiga kampeni na kuwashawishi wananchi kuipigia katiba pendekezwa kura ua ndio ni ukiukwaji  mkubwa wa sheria na na kitendo ambacho kina lengo la kiuvuruga mchakato mzima kwani serikali haina mamlaka ya kufanya hivyo kisheria.
Mratibu wa katiba kutoka kituo hicho Bi ANNA HENGA akizngumzia mambo kadhaa ambayo wamekutana nayo walipokuwa nawazunguka katika mikoa mbalimbali kutoa elimu juu ya katiba pendekezwa
Akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dar es  salaam Mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho  Bi HELLEN KIJO BISIMBA amesema kuwa kituo hicho  kimekuwa kikifwatilia kwa ukaribu kauli mbalimbali za viongozi wa serikali kuanzia kwa Mh Rais KIKWETE pamoja na mawaziri mbalimbali ambapo wamekuwa wakiendelea kupiga kampeni ya kuwahimiza wananchi kupiga kura ya ndio katika katiba inayopendekezwa.

WAISLAM WACHARUKA TENA,SOMA WALICHOKISEMA LEO JUU YA KAMATA KAMATA YA WAISLAM INAYOENDELEA NCHINI

Mwenyekiti wa jumuiya hiyo SHEKH MUSSA KUNDECHA akizngumza wakati wa akitoa tamko hilo leo jijini Dar es salaam 
 Wakati matukio mbalimbali ya kukamatwa kwa viongozi na waislam nchini kwa sababu za kujihusisha na ugaidi yakizidi kutokea Jumuiya ya taasisi za kiislam nchini Tanzania wameibuka na kulaani vitendo hivyo vinavyofanywa na serikali kupitia jeshi la polisi  huku wakiitaka serikali kuwaomba radhi waislaam kwa vitendo hivyo ambavyo wameviita ni vya uonevu na udhalilishaji kwa waislam wote nchini.
Mapema leo akizungumza na wanahabari mwenyekiti wa jumuiya hiyo SHEKH MUSSA KUNDECHA amesema kuwa kumekuwa na matukio ya kamata kamata ambayo kwa viongozi wa kiislam,walimu wa madrasa pamoja na watoto ambao wanasoma katika madrasa hizo vitendo ambavyo amesema kuwa vinakiuka haki za binadamu,haki ya kikatiba,kisheria,na utu wa mwislam huku amesema vitendo hivyo vinazidi kuchochea hasira kwa waialam hao na kuhisi kwamba serikali ina mpango wa kuangamiza uislam nchini.
Amesema kuwa vitendo hivyo vinavyoendelea katika mikoa mingi sasa nchini vinazidi kuwagawa watanzania kwa misingi ya dini,na imani zao jambo ambalo amesema kuwa linaweza kusababisha matatizo makubwa kama halitadhibitiwa huku awali.

Akitaja maeneo ambayo kamata kamata hiyo imewathiri waislam wengi ni pamoja na mkoa wa Kilimanjaro ambapo watoto na walimu wa madrasa wamekamatwa,mtwara,kilombero mkoani morogoro ambapo watu waliingia msikitini saa tisa usiku na baada ya muda mchache polisi wakaingia na kuwakamata jambo ambalo amesema bado linawapa shaka kuwa ulikuwa ni mpango uliosukwa.
Naibu katibu mkuu  wa Jumuiya na taasisi ya kiislam Tanzania, Rajab Katimba (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo
Amesema kuwa hoja inayoenezwa na serilakali kuwa wanazivamia madrasa kwa kuwa zipo kwenye hali duni na hazina usajili  haina maana kwa kuwa hakuna  sheria inayoonyesha jinsi na vigezo vya kuzisajili huku akisema uduni wa madrasa hizo sio hoja kwani zipo shule hadi wanafunzi wanakalia mawe lakini zimekuwa hazifungi wala kuvamiwa na polisi.
Aidha amesema kuwa kumekuwa na ugumu wa viongozi wao pindi wanapokamatwa na polisi kwa makosa kama hayo ambayo ameita ya kusingiziwa ambapo swala la kuwapatia dhamana limekuwa ni gumu sana na kinachofanyika ni kuwahamisha kutoka kituo kimoja kwenda kingine huku wakiendelea kupatiwa mateso bila makosa ya msingi kutajwa.
Katika hatua nyingine jumuiya hiyo imemtaka mkuu wa polisi nchini IGP,DPP,na kila kiongozi anayehusika na utekelezaji wa matendo hayo kuchukua hatua za kujirekebisha na kuacha kutekeleza uonevu huo dhidi ya waislaam.
Aidha amesema kuwa wao kama waislaam wanaotetea waumini wao wamedhamiria kama ifikapo  tarehe 15 mwezi ujao bila majibu sahihi ya tamkio lao wamedhamiria kufanya maandamano ya amani kuishinikiza serikali kuacha mara moja mpango huo ambao hauna tija kwa waislaam wala taifa kwa ujumla.

Tuesday, April 28, 2015

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRIL 29,2015.YOTE YAKO HAPA


VIDEO--HEBU TIZAMA ALICHOSEMA MBOWE KUHUSU HAWA RED BRIGADE NA MALENGO YAO

Kumekuwa na story inaendelea juu ya kikosi ambacho kinapewa mafunzo na chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA,maaarufu kama “Red Brigade” ambapo wadau mbalimbali wamekuwa wakikosoa kikosi hicho wengi wakidai kuwa ni kikundi ambacho kiinaandaliwa kufanya uhalifu wakati wa uchaguzi na mauaji wakati huo.,moja kati ya wada ambao wamekuwa wakilalamikia swala hilo ni msajili wa vyama vya siasa ambapo amekuwa akitishia hata kuwaadhibu CHADEMA kama hawatasitisha mpango huo.sasa hapa  nimekuwekea video ya mwenyekiti MBOWE akizngumzia mafunzo hayo na lengo lake huku akipiga mkwara kwa wale ambao wanaulalamikia mpango huo

WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA TAFFA OFISINI KWAKE,AWAAHIDI KUWAKUTANISHA KWA PAMOJA HIVI KARIBUNI

 Waziri wa ushirikiano wa Africa mashariki mh HARISON MWAKYEMBE amekutana Uongozi wa wakala wa  forodha na uondoshaji shehena Tanzania(TAFFA),kwa lengo la kukaa kwa pamoja na kujadili chamgamoto mbalimbali ambazo zinaikabili secta hiyo katika nchi za Africa mashariki.

Akizungumza katika ,mkutano huo waziri mwakyembe amesema kuwa ameamua kukutana na wakala  hao kutokana na mchango mkubwa walionao katika kuinua uchumi wa nchi na amekuwa na mahusiano ya karibu na wakala hao tangu akiwa waziri wa uchukuzi hadi sasa wizara ya Africa mashariki.
Waziri mwakyembe amesema kuwa amekuwa akipokea kero nyingi za maswala ya uondoshwaji wa shehena kutoka katika nchi za Africa mashariki na kuzitatua lakini ameshangaa kwanini Tanzania wamekuwa wagumu kupeleka kero zao kwa waziri huyo jambo ambalo limemsukuma kukutana na wadau kama hao ili kujua ni changamoto gani zinawakabili na jinsi gani wanaweza kuzitatua kwa pamoja.
Waziri wa ushirikiano wa africa mashariki mh HARSON MWAKYEMBE akizngumza na Uongozi wa wakala wa  forodha na uondoshaji shehena Tanzania(TAFFA) alipokutana nao ofisini kwake jana kwa lengo la kubadilishana mawazo na kujua changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili katika shughuli zao
Wakizungumza na waziri huyo viongozi wa TAFFA wameonyesha kutokuwa na imani na mamlaka ya mapato Tanzania TRA kwa kile walichokiita ukiritimba uliokithiri juu yao wanaofanyiwa na mamlaka  hayo ikiwemo dharau pamoja na kutosikilizwa keri zao jambo ambalo waziri MWAKYEMBE amesikitishwa nalo na kuahidi kulifanyia kazi mara moja


Aidha wakala hao wamelalamikia mfumo mbovu wa utoaji wa leseni kwa ajili ya kufanya kazi zao ambao kwa sasa leseni kwa wakala hao zimekuwa zikitolewa kwa mwaka mmoja jambo ambalo wamedai ni kero kwao kwani wamekuwa wakitumia muda mwingi sana katika kufwatilia leseni kuliko kufanya kazi za kampuni zao jambo ambalo pia waziri mwakyembe ameahidi kulisimamia kwa kina kuhakikishakuwa miaka ya leseni ya kazi zao inaongezwa ili kuwapa unafuu wao katika kufanya kazi zao.

Katika mkutano huo baada ya kuonekana wazi kuwa wakala hao wana changamoto nyingi za kuzungumza waziri MWAKYEMBE aliahirisha mkutano huo na kuahidi kuwakutanisha tena siku za karibuni kujadili kwa kina changamoto zinazowakabili ambapo mkutano huo unatarajiwa kujumuisha wadau wengine wengi akiwemo waziri wa fedha pamoja na wadau kutoka mamlaka ya mapato Tanzania TRA.


NYALANDU -AKUKAGUA VIFAA MBALIMBALI VILIVYONUNULIWA NA TAASISI YA BUFFET FOUNDATION

1
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akikagua gwaride la heshima jana alipowasili Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa jili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.
2
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiangalia moja ya kompyuta maalum zinazotumiwa wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa jili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.

WAZIRI KIVULI WA FEDHA, JAMES MBATIA AZUNGUMZIA KUPOROMOKA KWA THAMANI YA SHILINGI TANZANIA

 Waziri Kivuli wa Fedha, James Mbatia.
 Waziri Kivuli wa Fedha, James Mbatia (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Ofisi Ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam leo, kuhusu kuporomoka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania.

SOMA ORODHA YA VILABU VILIVYOLIMWA FAINI NA TFF LEO,NA WAMUZI WALIOFRUNGIWA HAPA


VILABU VPL VYAPIGWA FAINI, WAAMUZI WAFUNGIWA

Ruvu Shooting imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa kuzingatia Kanuni ya 14(9) ya Ligi Kuu kwa kutoingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo (changing room) katika mechi namba 149 dhidi ya Kagera Sugar iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga

 Pia Ruvu Shooting imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kutoingia vyumbani wakati wa mapumziko kwenye mechi hiyo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu.

Stand United imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya washabiki wake kuwatupia chupa za maji wachezaji wa akiba wa timu ya Polisi Morogoro katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu.

MALINZI AWAPONGEZA YANGA



Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans, Yusuf Manji kufuatia timu yake kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2014/2015.

Katika salamu zake za pongezi, Malinzi amesema kutwaa Ubingwa wa VPL ni jambo muhimu na sasa wanapaswa kuanza maaandalizi kwa ajili ya michuano ya kimataifa barani Afrika mwakani.

Monday, April 27, 2015

MAGAZETI YA LEO JUMANNE APRIL 28,2015

VIDEO--KIMENUKA TENA--ZITTO YALE YALEE YA KULE,ATUHUMIWA KUPORA CHAMA NA KUJIMILIKISHA MWENYEWE.MSIKILIZE HUYU

Katika hali ambayo sio ya kawaida na ya kushangaza mwenyekiti za zamani wa chama cha ACT TANZANIA ameibuka na kusema kuwa kiongozi mkuu wa chama hicho kwa sasa mh ZITTO kabwe amekipora chama hicho mikononi mwake kinyume na sheria na hastahili hata kuwa kiongozi wa chama hicho.mwenyekiti huyo anadai kuwa kitendo cha ZITTO KABWE kubadili jina la chama hicho pamoja na nembo

MABADILIKO HAYO YANAYOLALAMIKIWA YAKO HIVI-----

Wadau kama mnakumbuka Chama cha ACT-Tz kilibadilisha jina na kuwa ACT wazalendo mabadiliko yaliyofanyika machi 28 kwa kupitishwa na mkutano mkuu wa kwanza

Kamati ya mabadiliko ya katiba ilitoa maelezo juu ya taratibu zilizo tumika kufikia mabadiliko na maboresho ya katiba ya cham ikiwa ni pamoja na ufafanuzi ya juu ya mabadiliko yalifanywa kwenye katiba inayopendekezwa kama ifuatavyo

1 Jina la chama litakuwa ACT-WAZALENDO Badala ya ACT-TANZANIA
2 Herufi T katika neno ACT liwe na nembo ya taifa bendera ya Tanzania
3 Alama ya mkono iashirie uwazi na ukweli
4. Makao makuuu ya chama yawe dareesalaam na ofisi ndoga za makao makuuu ziwe mwanza na Zanzibar
5 Kuwepo na misingi kumi ya  chama ambayo imeanishwa katiba katiba ya chama


KAMATA KAMATA DAR-WAZUNGU WAWILI WADAKWA KWA UTAPELI.SOMA HII

  
RAIA WATATU WA KIGENI WAKAMATWA KWA MAKOSA YA WIZI WA MTANDAO KATIKA MABENKI JIJINI DAR ES SALAAM.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa watatu raia wa kigeni kwa makosa yanayohusiana na wizi wa mtandao kwa lengo la kuiba  katika vyombo vya fedha kama mabenki, maduka ya kubadilishia fedha (Bureau de Change) au kuingilia miamala ya fedha zinazosafirishwa na wateja kutoka nje na ndani ya nchi.
Polisi wa kikosi Maalum cha kupambana na wizi wa mtandao (Cyber Crime) walipata taarifa za kuaminika kwamba watu hao watatu walikuwa katika mazingira ya kutiliwa mashaka na ndipo Polisi walienda Mtaa wa Mindu eneo la Upanga na kuwakamata. Watu hao walikutwa katika nyumba namba 416 iliyopo katika ghorofa ya nne na walitambuliwa kwa majina yafuatayo:
1.      FOTIOS S/O VOGIATZIS, Miaka 32, Mfanyabiashara, Mkazi wa Upanga, Raia wa nchini UGIRIKI mwenye Passport namba AK2669977.

2.      ATHANASIOS S/O VOGIATZIS, Miaka 30, Mfanyabiashara, Mkazi wa Upanga, Mkazi wa Ugiriki mwenye Passport namba AK3049876.

3.      PANAGIOTIS S/O ANGELIDIS,           Miaka 25, Mkazi wa Upanga, Raia wa UGIRIKI mwenye Passport namba AK2644930.
Watu hao watatu ambao ni raia wa nchini Ugiriki kumbukumbu zao zinaonyesha kwamba wamekuwa wakiingia na kutoka nchini Tanzania na kwenda nchi mbalimbali za Afrika na Ulaya katika namna ambayo inaonyesha kuwa ni wahalifu wa kimataifa kupitia mitandao.
Katika upekuzi watu hao wamekamatwa na vielelezo mbalimbali vinavyopashiria njama zao kama ifuatavyo:
1.      Muhuri mmoja wa kughushi ulioandikwa “Inspector General of Police DSM”

MALINZI AFUNGUA KOZI YA WAKUFUNZI

Picha na maktaba



Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi leo amefungua kozi ya walimu wakufunzi wa mpira wa miguu chini inayofanyika katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

Malinzi amesema kozi hiyo ni muhimu kwa mustakabali wa soka la Tanzania, walimu wakufunzi watasaidia kuwafundisha walimu wengine wa mpira, ili kuweza kufundisha mpira kwa watoto wadogo ambao ndio hazina ya baadae.

Sunday, April 26, 2015

MAGAZETI LEO JUMATATU APRIL 27,2015, YAKO HAPA

DC MAKONDA AENDELEA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI KATIKA WILAYA YAKE SAFARI HII NI KATA YA WAZO

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiwahutubia wakazi wa Mtaa wa Kilimahewa Juu iliyopo uliopo Kata ya Wazo Dar es Salaam jana, alipofika kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu muda mrefu.
 DC Makonda akizungumza na viongozi wa Manispaa ya Kinondoni na wakata ya Wazo kuhusu mgogoro huo.

VIDEO--NEC WAMJIBU DK SLAA KUHUSU KUIPENDELEA CCM

PICHA --YALIYOJIRI SHEREHE ZA MUUNGANO LEO DAR ES SALAAM

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipunga mkono kuwasalimia wananchi wakati alipokuwa akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam, leo kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Davis Mwamunyange .Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake wa Serikali, wakisimama kutoa heshima wakati ikipigwa mizinga 21, uwanjani hapo. Picha na OMR



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akikagua gwaride la heshima, wakati wa sherehe za Maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR

TIZAMA MBUNGE NASSARI NA SALUM MWALIM WAKIWA MAKAMBAKO WALICHOKIFANYA



Picha mbalimbali zikiwaonesha NKMZ Salum Mwalimu na Mbunge wa Arumeru Magharibi Joshua Nassari wakihutubia wananchi wa Makambako, mkoani Njombe kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana (juzi) kwenye Uwanja wa Azimio, ikiwa ni sehemu ya operesheni ya mafunzo kwa viongozi kukiandaa chama kwenda kushinda dola na kuongoza serikali.

Saturday, April 25, 2015

MBOWE HUKO UKEREWE NI HISTORIA NYINGINE--PICHA ZIKO HAPA

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika  kwenye Uwanja wa Mongella mjini Nansio wilayani Ukerewe mkoani Mwanza.
Mbowe akisalimiana na mlemavu wa viungo alipowasili kwa chopa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mongella mjini Nansio Ukerewe mkoani Mwanza.