Saturday, February 28, 2015

MAUAJI YA ALBINO NCHINI YAMGUSA MWANAMITINDO TAUSI LIKOKOLA,AUTUMIA USIKU WA JANA KUCHANGISHA FEDHA ZA KUWASAIDIA

Mwanamitindo mkongwe kutoka nchini tanzania TAUSI LIKOKOLA akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla yta chakula cha jioni iliyoandaliwa rasmi kwa ajili ya kuchangisha fedha ziweze kuwasaidia watu wenye uhitaji maalum ikiwemo watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na watu wanaoishi na virusi vya ukimwi

 Baada ya kukaa nje ya Tanzania kwa zaidi ya maika kumi na hivi majuzi kurejea kwa kipindi kifupi nchini  mwanamitindo maarufu na mkongwe TAUSI LIKOKOLA usiku wa kamkia leo ameendesha shughuli ya kuchangia fedha kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye matatizo ya ulemavu wa ngozi pamoja na waathirika wa ugonjwa wa ukimwi nchini ikiwa ni sehemu ya mwanamitindo huyo kurudisha shukrani kwa watanzania kwa kumpokea tena nchini.


Shughuli hiyo ambayo imeendeshwa jijini Dar es salaam imeshughudia watu mbalimbali kujitokeza kwa wingi kumpa saport ili kufanikisha lengo lake hilo ambalo ni jambo ambalo limepongezwa na watanzania wengi kwani kuna watu wengi wenye uhitaji na inahitajika watu kama TAUSI wengi ili kuwasaidia watanzania.
Akizungumza na mtandao huu katika hafla hiyo ya chakula cha jioni iliyokwenda sambamba na harambee hiyo mwanamitindo TAUSI LIKOKOLA amesema kuwa ni miaka mingi amekuwa nje ya Tanzania na baada ya kurejea kwake amesikitishwa sana baada ya kukuta tatizo ambalo limeanza kuwa sugu la mauaji ya watu ambao wana ulemavu wa ngozi jambo ambalo amesema kuwa limemsukuma kuanza kuwasaidia watu hao kwani kwa sasa wanaishi katika mazingira yasiyo sala sana.

Mmoja kati ya waandishi nguli  na wasomi nchini Tanzania GENERALI ULIMWENGU alikuwa ni mmoja kati wa wageni waalikwa katika shughuli nhiyo ambapo amempongeza TAUSI kwa wazo lake hilo la kuwasaidia watu wenye uhitaji kwani ni baraka hata kwa mwenyezi mungu

Amesema kuwa ni jambo la kutisha sana kuona au kusikia mambo ambayo wanakutana nayo walemavu wa ngozi nchini Tanzania na hata ukisikiliza story zao jinsi wanavyoishi bila amani lazima itakugusa ambapo amesema kuwa ni wakati sasa wa watanzania kukemea kwa lugha moja tatizo hilo ili likome na lisijirudie tena.

Alikuwepo pia,aliyekuwa miss Tanzania mwaka 2014 SITTI MTEMVU akiwa anashughudia hafla hiyo kwa ukaribu kabisa
Aidha katika hatua nyingine mwanamitindo TAUSI LIKOKOLA ameitumia hafla hiyo kuzindua manukato yake mapya pamoja na vitabu ambavyo ameviandika mwenyewe aambapo alitumia bidhaa hizo katika kupiga mnada ili kupata fedha aweze kuwasaidia watu wenye uhitaji maalum nchini tanzania.
Mbunifu wa mavazi maarufu nchini TANZANIA MUSTAFA HASANALI ambaye usiku huo ndiye aliyemvalisha TAUSI LIKOKOLA naye alikuwepo katika hafla hiyo

Tupige na sisi picha utotue kwenye blog--sawa nikawapiga
ENDELEA KUANGALIA PICHA NYINGI ZA TUKIO HILO HAPO CHINI

UNDANI NA UKWELI WA KIFO CHA CAPTAIN KOMBA HUU HAPA

...Komba enzi za uhai wake.
MBUNGE wa Mbinga Magharibi, Kapten John Komba amefariki dunia jioni hii jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, hata hivyo hakuwa tayari kuelezea kwa undani kwa madai kuwa taarifa hizo zimemfikia sasa hivi.
Mmoja wa watoto wa Komba ambaye aliyejitambulisha kwa jina la Herman amethibitisha kutokea kwa msiba huo na akasema, huku akilia, msiba wa baba yake upo nyumbani kwake Mbezi Tangi Bovu, Dar.
Habari zinasema asubuhi ya leo Komba alikwenda kwenye shughuli zake za kikazi kama kawaida lakini baadaye akajisikia vibaya, hivyo akaamua kurudi nyumbani ambako alizidiwa ndipo familia yake ilipoamua kumkimbiza Hospitali ya TMJ lakini alipopimwa na madaktari ikathibitika kuwa alikuwa tayari ameaga dunia. habari zaidi zinasema kuwa hivi sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo.
Kapteni Komba ambaye pia ni Mkurugugenzi wa Kikundi cha Maigizo cha Tanzania One Theatre (TOT),  ambacho kina kikundi cha taarabu na bendi  inayokwenda na mtindo wa Achimenengule, amekuwa akikisaidia sana chama chake, Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kampeni zake wakati wa uchaguzi kwa kutunga nyimbo za kuhamasisha wapiga kura na kushiriki kupiga live kwenye majukwaa ya kisiasa.
 .
..alipokuwa bungeni
Enzi za uhai wake alitamani  sana na kufanya juhudi kubwa ili mtindo wa Achimenengule uwe wa kitaifa lakini ikashindikana,  na badala yake Watanzania sasa tuna muziki wa Mduara ambao umekuwa kama mtindo wa muziki wetu kwa sababu zifuatazo.
Kwanza, ni mtindo halisi wa Kitanzania uliochipuka kutoka mahadhi ya kimwambao ya Tanzania. Pili, ndiyo mtindo pekee uliowahi kutumiwa na bendi nyingi baada ya kuasisiwa na ‘mabingwa’ wa muziki wetu, wana Njenje, The Kilimanjaro Band.
Baada ya bendi hiyo kuuasisi, mtindo huo, tayari umepigwa na bendi kama TOT Plus, Chuchu Sound, Pamo Sound, Inafrika Band, wana mipasho kadhaa na mwanamuziki mahiri lakini asiyethamini kiwango chake kikubwa cha muziki, Bob Haisa.
Sababu ya tatu ni kwamba mtindo huo umekuwa wa kupigwa na bendi nyingi, vikundi vingi na wanamuziki wengi si kwa kulazimisha bali kwa mapenzi tu ya mashabiki wa muziki wa Tanzania.
Kapteni Komba awali alikuwa mwalimu wa shule ya msingi kabla ya kuingia jeshini na kuwa kiongozi wa kikundi cha maonesho cha jeshi na baadaye Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akamshawishi aachane na jeshi na kujiunga na CCM wakati wa mfumo wa vyama mingi ulipoingizwa mwaka 1992.
“Mzee Mwinyi ndiye aliyenifanya niache jeshi wakati huo nikiwa na cheo cha ukapteni. Aliniomba nikisaidie chama kwa kuanzisha kikundi ambacho lengo lake lilikuwa kukipigia debe CCM,” aliwahi kusema hivyo Kapteni Komba.
Ameshiriki kampenzi za marais Ally Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa na aliye madarakani hivi sasa, Jakaya Mrisho Kikwete. Alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi hadi kifo kinamchukua.
Licha ya siasa Kapteni Komba alikuwa anamiliki shule na pia alikuwa na biashara kadhaa.

Mwaka 2012 Komba aliwahi kupelekwa India kwa matibabu ambapo alifanyiwa upasuaji wa nyonga baada ya kupata ugonjwa uliosababisha mifupa kusagana sehemu hiyo ya nyonga.
Baada ya kurejea nchini alisema upasuaji huo ulichukua saa tano na ulifanyika katika Hospitali ya Apollo, India na alikanusha kuwa alikuwa na ugonjwa wa figo.Ugonjwa uliomuua ni shinikizo la damu ambalo lilikuwa likimsumbua kwa muda mrefu.
..marehemu Komba akiongea na wanahabari nyumbani kwake Mbezi tangi Bovu akielezea kuimarika kwa afya yake aliporejea kutoka India kwenye matibabu, Julai 27, 2012.
MALI ZAKE ZATISHIWA KUUZWA
Mapema mwezi uliyopita mwaka huu, mali za Kapteni John Komba zilitangazwa kupigwa mnada kutokana na kushindwa kulipa deni analodaiwa na Benki ya CRDB.
Mali hizo zilihusisha eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 2,214 lililopo Mbezi Tangi Bovu, Dar es Salaam, kiwanja namba 1030 kilichosajiliwa kwa jina la John Damiano Komba na Salome Komba.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa kwenye vyombo vya habari, Kampuni ya Uwakili ya Mpoki & Associates Advocates inayoiwakilisha CRDB ilitangaza kuuza eneo hilo la kibiashara lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya mafuta, maduka makubwa, benki, sehemu ya kufanyia mazoezi, hospitali na huduma nyingine za kijamii.

Marehemu Komba ameacha mjane, Bi Salome, ambaye ni mwalimu kitaalumu na watoto kadhaa. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi- ameen!

Friday, February 27, 2015

TIZAMA KAULI YA ZITTO KABWE KUHUSU WAKINA TIBAIJUKA KUPANDISHWA KWENYE KAMATI YA MAADILI



Kazi inayofanyika katika Baraza la Maadili ni kazi nyeti sana ambayo inajenga 'misingi madhubuti ya uwajibikaji' ili kupambana na rushwa kwa viongozi wa umma. Iwapo Baraza hili lingekuwa limeanza kufanya kazi namna hii tangu mwaka 1995 sheria ya Maadili ilipotungwa, (Sheria hii ilitokana na Muswada binafsi wa Mbunge Jenerali Ulimwengu ), angalau tungekuwa tumeondosha 'impunity' iliyokita mizizi nchini kwetu.
Moja ya adhabu kwa mujibu wa Katiba kwa mtu aliyekiuka maadili ya Viongozi wa Umma ni kupoteza nafasi ya Uongozi aliyonayo. Wananchi tushinikize kwamba Tangazo la Mali na Madeni ya Viongozi wa Umma liwe wazi bila masharti ili kwanza kuwaumbua wanaodanganya mali zao na pili kuwaburuza kwenye Baraza la Maadili kueleza wamepataje Mali walizonazo na za wenza wao.
Taasisi za Uwajibikaji zipo, tatizo hazifanyi kazi inavyotakiwa. Sakata la Escrow limeibua taasisi hizi. Tusiishie hapa

BLOGGERS KUKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM KESHO KATIKA PATI YA KIHISTORIA

 Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network  na mmiliki wa Blog ya The Habari.com Joachim Mushi (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi. Kutoka kushoto ni  Mkala Fundikira,Shafia Mpanja wa AM,Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale na Khadija Kalili.
 Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale akifafanua jambo wakati wa mkutano.
 Mmiliki wa Blog ya Bongoweekeend Khadija Kalili akizungumza wakati wa mkutano.

TIGO YATOA UDHAMINI KWA WASHINDI WA TIGO NGORONGORO RUN KUSHIRIKI TIGO KILI HALF MARATHON 2015

WAKI1Mwanariadha Alphonce Felix akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati kampuni ya Tigo ilipotangaza udhamini kwa wanariadha ambao walishinda mbio za mwaka jana za Tigo Ngorongoro Run Marathon kushirki kwenye mbio za mwaka huu za Tigo Kili Half Marathon. Pembeni kulia ni .Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Kanda ya Kaskazini, David Charles na Meneja wa Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha.WAKI2Mwanariadha Mary Naali akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati kampuni ya Tigo ilipotangaza udhamini kwa wanariadha ambao walishinda mbio za mwaka jana za Tigo Ngorongoro Run Marathon kushirki kwenye mbio za mwaka huu za Tigo Kili Half Marathon. Pembeni kulia ni .Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Kanda ya Kaskazini, David Charles na Meneja wa Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha na kushoto ni Meta Petro Mjumbe toka riadha Tanzania pia ni kocha wa wanariadha hao.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI KUAGA MWILI WA MAMA MZAZI WA DKT. EDWARD HOSEA, JIJINI DAR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu mama mzazi wa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Ewdard Hose, Mama Esther Gigwa, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika nyumbani kwa Mkurugenzi huyo, Masaki jijini Dar es Salaam, leo Feb 27, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kwenye Kitabu cha maombolezo ya marehemu Esther Gigwa, Mama mzazi wa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Edward Hosea, wakati alipofika kushiriki kuaga mwili huo nyumbani kwa mkurugenzi huyo, Masaki jijini Dar es Salaam, leo Feb 27, 2015. Picha na OMR
Wanafamilia wafiwa wakiwa katika shughuli hiyo ya maziko




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Edward Hosea, wakati alipofika kushiriki kuaga mwili wa marehemu mama mzazi wa Mkuruenzi huyo nyumbani kwake, Masaki jijini Dar es Salaam, leo Feb 27, 2015. Picha na OMR

WATU 14 MBARONI KWA UTEKAJI WA ALBINO TANZANIA

Watu wenye ulemavu wa ngozi waendelea kuishi kwa hofu nchini Tanzania.
Watu wenye ulemavu wa ngozi waendelea kuishi kwa hofu nchini Tanzania.

Mwanza, Jeshi la polisi mkoani Mwanza, linawashikilia watu 14 kwa tuhuma za kuhusika na tukio la utekaji nyara wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Pendo Emanuel wa kijiji cha ndami wilayani kwimba tukio  lililotokea Desemba 27 mwaka jana.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaapisha wakuu wapya wa wilaya za Misungwi, Kwimba na Sengerema Mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa mulongo  amesema kuwa miongoni mwa watuhumiwa hao wamo waliohusika kwenye utekaji wa mtoto huyo pamoja na wale waliomuhifadhi kwenye hoteli moja jijini Mwanza kabla ya kumsafirisha kwenda kusikojulikana.

Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi mkoa wa Mwanza Alfred Kapole pamoja na katibu wa chama hicho mkoani humo Enos Tuju wameendelea kukemea  ukatili dhidi watu wenye ulemavu wa ngozi Albino  pamoja na  kuiomba serikali kudhibiti vitendo vya mauaji  ya albino yanayo  endelea kutokea mkoani Mwanza.

MAPYAA---DC MAKONDA KUPANDISHWA KIZIMBANI RASMI


Katika hali isiyokuwa ya kawaida aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa dare s salaam bwana JOHN GUNINITA leo ametangaza kumpandisha mahakamani mkuu wa wilaya ya kinondoni  DC PAUL MAKONDA kwa kila elichokiita kuwa ni kudhalilishshwa na kutupiwa maneno ya kashfa.VIDEO IKIONYESHA SIKU MAKONDA ALIPOTOA MANENO HAYO
Akizungumza na wanahabari mapema leo jijini Dare s salaam mh GUNINITA amesema kuwa kitendo alichokifanya DC MAKONDA cha kuitisha mkutano wa wanahabari na kuwatukana viongozi wastaafu wa chama cha mapinduizi ni kitendo ambacho hakivumiliki na mtu yoyote na kwa kuwa chama kimeshindwa kumshughulikia sasa njia pekee anayoiona inafa kumwadhibu ni kwenda mahakani ili haki ipatikane.


Amesema kuwa sio mara ya kwanza kwa kiongozi huyo aliyewahi kuwa kiongozi wa umoja wa vijana CCM kulalamikiwa kwa kitendo chake cha utomvu wa nidhamu mbele ya viongozi wenzake wa ndani ya chama hivyo sasa ni wakati muafaka wa kuhakikisha kuwa wanamfundisha adabu kwa kutumia sheria za Tanzania.

Ameongeza kuwa chama cha mapinduzi kina utaratibu wake wa kuwaonya wanachama wake pale wanapokwenda kinyume na utaratibu wa chama hicho lakini kitendo cha kijana huyo kutoka nje mbele ya wanahabari kuwatukana viongozi wa chama hicho ambao mbali na uongozi ni baba zake ni kitendo ambacho sio utaratibu wa chama na hakina wa kuvumilia kitendo hicho

Thursday, February 26, 2015

MAGAZETINI LEO IJUMAA TAREHE 27,FEBRUARY 2015


TAIFA STARS KUSHIRIKI COSAFA CUP.



Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imethibitisha kushiriki michuano ya kombe la COSAFA nchini Afrika Kusini kufuatia mwaliko wa Baraza la vyama vya soka Kusini mwa Afrika (COSAFA).
Michuano ya kombe la COSAFA inatrajiwa kuanza kutimua vumbi katikati ya mwezi Mei mwaka huu nchini Afrika Kusini, na ratiba ya hatua ya awali ya makundi inatarajiwa kutangazwa leo jioni saa 1:00 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki moja kwa moja na kituo cha Luninga cha Supersport 4.
Taifa Stars itakuwa juu (seeded) katika hatua ya makundi, ambapo nchi nane zitagawanya katika makundi mawili na washindi wa kila kundi wataingia hatua ya robo fainali, nchi  nyingine zitakazoanzia kwenye makundi ni Lesotho, Madagascar, Marutius, Namibia, Seychelles, Swaziland.
Katika kila kundi, timu zote zitacheza michezo mitatu na mshindi wa kila kundi ataingia katika hatua inayofuata ya robo fainali itakayozijumuisha nchi za  Afrika Kusini, Botswana, Ghana, Malawi, Msumbuji na Zambia ambazo zimeingia katika hatua ya pili kutokana na nafasi zao kwenye msimamo wa viwango vya FIFA.

breaking newzz--MSANII CHID BENZ ATUPWA JELA MIAKA MIWILI KOSA LA MADAWA YA KULEVYA

Breaking News:Chidi Benzi atupwa jela Miaka miwili kwa makosa ya kukutwa na Dawa za kulevya aina ya Heroin wakati alipokuwa akienda kufanya tamasha la muziki Oktoba 24 Mwaka jana.



PICHA 5:;HATIMAYE KINYESI CHA MWALIMU KILICHOKUWA KWENYE CHUMBA CHAKE CHATEKETEZWA



Mfanyakazi wa Manispaa ya Temeke Kitengo cha Usafishaji,

Ramadhani Athuman akiweka dawa katika vyombo alivyokuwa akitumia kuhifadhia
kinyesi mwalimu Gaudensia Albert wa Shule ya Sekondari Kibasila jijini Dar es
Salaam, kabla vyombo hivyo havijaenda kutupwa dampo. (Picha na Francis Dande)

 Mlango ukivunjwa ili maofisa wa afya waweze kuingia ndani ya chumba cha mwalimu.


 Umati wa watu ukiwa nje ya nyumba wakati zoezi la kuteketeza                                       kinyesi likiendelea.



 Kinyesi kikiwa kimehifadhiwa ndani ya chumba cha mwalimu.

 Wafanyakazi wa Manispaa ya Temeke wakiondoa kinyesi katika nyumba ya mwalimu Gaudensia.

MASWALI 10 ALIYOYAJIBU JOHN MNYIKA KUTOKA KWA WAPIGA KURA WAKE,TIZAMA HAPA




1. Mengi Athman (30), Machinga; mkazi wa Mburahati.
Ulituahidi kuondoa kero ya machinga kabla ya kupata kura yangu, leo hii tunaishi kama popo mitaani umefanya jitihada gani mpaka sasa?
Jibu: Nimetekeleza ahadi hii kwa namna mbalimbali mwaka 2011, 2012, 2013 na 2014. Nimefanya mkutano wa kikazi na Machinga na kupokea kero zilizopewa  kipaumbele.
2. Omary Sebea (33), Fundi Seremala; mkazi wa Kimara King’ong’o
Miaka mitano imekwisha na kilio kikubwa cha maji bado hakijamalizika, ninanunua ndoo Sh500, kwa nini nikupe kura yangu 2015? Kwanini eneo la King’ong’o maji hayapatikani wakati kuanzia Kimara mpaka Msikitini na Matosa yanapatikana?
Jibu: Miaka mitano haijaisha na tayari kuna maeneo ambayo hakuna kilio cha maji. Nashukuru Omary Sebea ametambua kwamba maji yanafika Kimara mpaka Msikitini na Matosa. Juu ya eneo la King’ong’o na eneo lingine ambalo hajalitaja la Michungwani maji hayafiki na nilifuatilia Dawasa na Dawasco toka mwaka 2010 na 2011 na nikaelezwa kwamba kwa mwinuko uliopo hayawezi kufika kwa urahisi kutokana na mlima. Sikuridhika na majibu hayo hivyo nitaendelea kuisimamia Serikali.
3. Hamad Hussein (27), Dereva Bajaji; Mkazi wa Makoka

Wednesday, February 25, 2015

TUKIO LA KWANZA ALILOFANYA RAIS KIKWETE HUKO ZAMBIA

unnamed
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Rais wa Zambia Michael Sata aliyefariki mwaka jana katika eneo la maziko ya viongozi wa kitaifa jijini Lusaka Zambia leo.Rais Kikwete alitumia  wasaa huo pia kuweka shada la maua katika marais wa Zambia waliofariki Marehemu Frederick Chiluba na Levy Mwanawasa.
(picha na Freddy Maro)

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS TAREHE 26 FEBRUARY 2015 YAKO HAPA

RAIS JAKAYA KIKWETE AWASILI ZAMBIA

ZAM2
ZAM1Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wawasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka Zambia na kupokewa na mwenyeji wao Rais Edgar Lungu wa Zambia leo asubuhi kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.(PICHA NA FREDDY MARO WA IKULU)

VODACOM NA TIGO SASA KITU KIMOJA UTOAJI HUDUMA ZA KIFEDHA

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutia saini makubaliano ya kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha na miamala mbalimbali ya malipo zinazotolewa na kampuni yake kupitia huduma ya M-Pesa na Tigo kupitia huduma yake ya Tigopesa. Anayeshuhudia kulia ni Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez.
Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutia saini makubaliano ya kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha na miamala mbalimbali ya malipo zinazotolewa na kampuni yake kupitia huduma ya Tigopesa na Vodacom kupitia huduma yake ya M-Pesa. Anaeshuhudia kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (kushoto, aliyekaa) na Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez (kulia, aliyekaa), wakitia saini mkataba wa makubaliano ya kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha na miamala mbalimbali ya malipo zinazotolewa na makampuni yao kupitia huduma ya M-Pesa na Tigopesa. Wanaoshuhudia kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Vodacom Tanzania, Ngayama Matongo na kulia ni Meneja wa Chapa ya Tigo, William Mpinga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza (wa pili toka kushoto) na Meneja Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez, wakibadilishana nakala za mkataba wa makubaliano ya kutoa huduma za kutuma na kupokea fedha na miamala mbalimbali ya malipo zinazotolewa na makampuni yao kupitia huduma ya M-Pesa na Tigopesa, wanaoshuhudia kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria wa Vodacom Tanzania, Ngayama Matongo na kulia ni Meneja wa Chapa ya Tigo, William Mpinga.

MICHEZO24--TIZAMA KOCHA JULIO NDANI YA TIMU YAKE MPYA

 Kocha Msaidizi wa Coastal Union,Jamhuri
Kiwelu "Julio"kulia akisisitiza jambo mazoezini jana mara baada ya
kuwasilia mkoani Tanga kuifundisha timu hiyo kushoto ni Kocha Mkuu
James Nandwa ,Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Coastal Union,Albert
Peter,Katibu Mkuu Coastal Union,Kassim El Siagi na Meneja wa Coastal
Union Akida Machai.

Kocha Msaidizi wa Coastal Union ,Jamhuri
Kiwelu "Julio"akizungumza na viongozi wa Coastal Union mara baada ya
kuwasili mazoezini jana ,Picha kwa Hisani ya Coastal Union




HII NI KALI LEO KUTOKA KWA CHENGE NA ESCROW LEO

Pichani ni Mbunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi ,
Andrew Chenge akitoka kwenye Kamati ya Maadili leo Jiji Dar Es Salaa

MBUNGE wa Jimbo la Bariadi Magharibi,Andrew Chenge amesema anataka muongozo wa kujadiliwa yeye katika Tume ya Maadili kutokana na suala la Akaunti ya Tegeta Escrow liko Mahakamani hivyo shitaka lake haliko msingi wa kisheria ,Anaripoti KAROLI VINSENT ,Endelea nayo ..

Kugoma kwa chenge kwa shitaka lake kutosikilizwa na  kutaka Tume ya Maadili itolee ufafanuzi juu ya kuwepo kwa Shauri kwenye Makama kuu ya Tanzania linalozuia kujadiliwa kesi nje ya Mahakama hivyo kuhusu sakata la Akaunt ya Tegeta Escrow kumetokea mda huu jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa anasomewa mashtaka yake kwenye tume hiyo ambapo---..
                
Chenge ambaye ni Mwanasheria Mkuu  wa zamani wa Serikali anashatakiwa na tume ya maadili kutokana na kitendo chake che kupokea pesa ya zaidi Bilioni 1.6.8 kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engineering bwana James Rugimalira wakati akiwa mtumisha wa umma na bila kuitangaza kama zinavyodai sheria za tume hiyo.
             
  Mbunge huyo alipandishwa Mahakama ya Baraza la maadili mda huu Jijini Dar es Salaam mbele ya Mwenyekiti wa Baraza hilo maadili Jaji Mstaafu Hamis Msumi -
           
 Ambapo amesomewa mashtaka yake na Wakili wa Baraza Maadili Hassan Mayunga  alidaiwa Mbunge huyo wakati akiwa mwanasheria mkuu wa serikali mwaka 2006  alivunja sheria ya maadili ya viongozi wa umma kwa kuipa mkataba wa Miaka 20 kampuni ya kufua Umeme ya IPTL.
           
Wakili huyo amesema kitendo iko cha Chenge kuipa mkataba kampuni hiyo kinaonekana wazi alikuwa anamaslahi yake binafsi kwenye kampuni hiyo  na kupelekea kuingiziwa pesa na Mbia wa Kampuni ya IPTL ambayo ni VIP Engineering na kupata mgao wa bilioni 1.6.8 kama zawadi ya kuingizia hasara serikali kwenye mataba hao.
Mbunge Chenge akimgomea mwandishi wa habari wa
 Itv na Radio One Ufoo  asimuulize swali lolote
    Mabishano ya Sheria yatokea
Mara baada ya kusomewa mashtaka hayo na Wakili huyo wa Baraza hilo ndipo Chenge akaliomba Baraza hilo lisijadili kesi hiyo kutokana na kuwepo kwa kesi mahakama kuu linalokataza Vyombo vyovyote vya Serikali visijadili suala linalohusu Mihamala ya Akaunt ya Tegeta Escrow mpaka pale hukumu itakapotolewa.
Baada ya kusema hivyo Mwenyekiti wa Baraza hilo JajiHamis Msumi

Alimtaka Wakili wa Baraza hilo kuhakiki hati ya Staka ya mahakama kuu na Wakili huyo akajitetea na kusema hakuna kipengere kwenye kesi hiyo iliyoko mahakama kuu kinachozuia vyombo vingine kuzungumzia.
Baada ya kusema hivyo Jaji Hamis Msumi h akahahirisha kesi hiyo mpaka kesho ili apate mda wa kusoma hati hiyo ya mahakama kuu kama kutakuwa na kipengele hicho kwenye kesi na endapo kitakuwepo basi Tume hiyo haiwezi kulizungumzia suala hilo