Showing posts with label HABARI MPYA. Show all posts
Showing posts with label HABARI MPYA. Show all posts

Tuesday, September 20, 2022

Viongozi wa Siasa Wakumbushwa Kuacha Kuwagawa Wananchi Kwa Maslahi yao Binafsi.

Na Vicent Macha

Wito umetolewa kwa Wanasiasa nchini kuacha tabia ya kuwagawa wananchi nabadala yake waendeleze misingi ya Aamani,Umoja na Maendeleo iliyoachwa na Muasisi wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Wito huo umetolewa leo Dar es salaam na Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba kwenye kikao cha kubadilishana Uzoefu na Ujuzi kilichoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere nakuwakutanisha wadau mbalimbali ikiwemo viongozi wa vyama vya siasa,lengo likiwa  ni kujadili misingi iliyoachwa na viongozi wa Taifa tangu kupata uhuru mwaka 1961.

Amesema kuwa viongozi wa kitaifa walifanya imani kuwa wananchi wote ni sawa ,nakwamba baada ya kupata uhuru viongozi hao  hawakuona umuhimu wa nchi kuwa huru huku wananchi wakiwa hawako huru,hivyo walihakikisha wanasimamia misingi ya Amani,Umoja na Maendeleo ili kulifanya Taifa la Tanzaia kuwa na Umoja.

"Tusiwagawe wananchi,tuhakikishe tunalinda misingi ya amani,umoja na maendeleo iliyoachwa na Viongozi wetu wa kitaifa waliopambana hadi tukapata uhuru,hivyo tunapaswa kuwa na nchi huru yenye watanzania huru."amesema Jaji Warioba.

Awali Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Joseph Butiku amesema kwamba Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi ya uhai wake amekuwa akisimamia misingi ya Amani,Umoja na Maendeleo hivyo viongozi wa vyama vya siasa hawana budi kushirikiana kwa pamoja kuondoa changamoto zinazowakwaza watanzania katika kuwaletea maendeleo.

Kwa upande wake kadhalika Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Bara Christina Mndeme amewambia waandishi wa habari kuwa mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere umewasaidia kupata mawazo ya namna yakuendeleza  misingi ya amani,Umoja na Maendeleo iliyoachwa na Hayat baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
\
                                                                   Habari Picha.
Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba akiongea na Baadhi ya Wajumbe kutoka vyama mbalimbali katika Kongamano liliandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere mapema leo Mkoani Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku akiongea katika Kongamano lililoandaliwa na Taasisi hiyo.
Baadhi ya Viongozi wa dini wakifuatilia matukio katika Kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere mapema leo mkoani Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Bara Christina Mndeme akiongea katika kongamano la kubadilishana uwezo kati ya Viongozi wa vyama mbalimbali vya Siasa na Asasi za Kijamii.
Kongamano likiendelea.




\



Wednesday, July 13, 2022

MAKAMU WA RAIS AKIFUNGA MAONESHO YA SABASABA

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) mhandisi Prof. Fredrick Kahimba juu ya mtambo maalum wa kuchakata zao la Chikichi ili kuweza kupata mafuta ya Mawese wakati Makamu wa Rais alipotembelea Banda la Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Sabasaba. Julai 13 ,2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisiliza maelezo kutoka kwa washiriki mbalimbali katika Banda Maalum la Zanzibar wakati alipotembelea na kufunga Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Sabasaba Jijini Dar es salaam tarehe 13 Julai 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akisiliza maelezo kutoka kwa washiriki mbalimbali katika Banda Maalum la wajasiriamali wanawake la Mama Anna Mkapa wakati alipotembelea na kufunga Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Sabasaba Jijini Dar es salaam tarehe 13 Julai 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa kilele cha Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Sabasaba Jijini Dar es salaam tarehe 13 Julai 2022.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akikabidhi zawadi kwa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kuwa kinara wa Banda bora la Maonesho ya Sabasaba kwa mwaka 2022 wakati wa kilele cha Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Sabasaba Jijini Dar es salaam tarehe 13 Julai 2022.

Mwenyekiti wa Bodi wa Tantrade Dkt. Ng’wanza Soko akimkabidhi zawadi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango kwa ushiriki wake katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Sabasaba Jijini Dar es salaam  wakati wa ufungaji wa maonesho hayo leo tarehe 13 Julai 2022.

Sunday, July 3, 2022

Makinda atinga kwenye Mnada wa Old Shinyanga Akihamasisha Wananchi kushiriki Sensa

 





Makinda ametembelea katika Mnada huo leo Julai 3,2022 akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na wananchi kwenye mnada huo, amewasihi siku hiyo ya zoezi la kuhesabiwa Sensa ya Watu na Makazi Agosti 23 mwaka huu, washiriki kikamilifu , ili Serikali ipate idadi ya watu wake kamili kwa kila eneo kuanzia ngazi ya chini.

“Tunaendesha zoezi la Sensa ya watu na makazi ili tujue Tanzania tuko watu wangapi, na itaisaidia Serikali katika upangaji wa mipango ya maendeleo kwa wananchi wote kulingana na idadi yao,” amesema Makinda.

“Rais Samia Suluhu Hassani amekuwa akitafuta fedha za maendeleo kwa wananachi wake, na anataka kujua ni maeneo gani ambayo wananchi bado hawana maendeleo kwa uwiano sawa na idadi yao, hivyo nawasihi jitokezeni kuhesabiwa Sensa,” ameongeza.

Aidha, amewataka pia wananchi watoe ushirikiano kwa Makarani wakati wa Sensa pamoja na kutoa taarifa za kweli na usahihi na siyo kudanganya ili siku huduma zikianza kutolewa na Serikali katika eneo husika kusiwepo na mapungufu.

“Kama wewe una ng’ombe 100 wataje wote usiseme una ng’ombe 10, ili siku madawa yakija kulingana na idadi ya mifugo mlioitaja msianze kugombania na kulalamika madawa hayatoshi na wakati awali nyie ndiyo mlitoa taarifa siyo sahihi,” amesema Makinda.

Katika hatua nyingine, amewataka wananchi wasiwafiche ndani watu wenye ulemavu pamoja na wazee, bali wawape fursa nao ya kuhesabiwa katika zoezi hilo la Sensa.

Nao baadhi ya wananchi waliokuwa kwenye mnada huo pamoja na wafanyabiashara, wameshukuru kupatiwa elimu hiyo kuhusu Sensa ya Watu na Makazi.

Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi Mhe. Anne Makinda akizungumza katika Mnada wa Old Shinyanga na kutoa elimu ya Sensa ya watu na makazi kwa wananchi na kuwahamasisha washiriki kikamilifu kuhesabiwa katika zoezi hilo la Sensa Agosti 23 mwaka huu.

Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi Anne Makinda akizungumza katika Mnada wa Old Shinyanga na kutoa elimu ya Sensa kwa wananchi na kuwahamasisha washiriki kikamilifu kuhesabiwa katika zoezi hilo la Sensa Agost 23 mwaka huu.

Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu NBS Pastory Ulimali akizungumza kwenye Mnada huo wa Old Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza na wananchi kwenye Mnada huo wa Old Shinyanga wakati wa utolewaji wa elimu ya Sensa.

Wananchi wakisikiliza elimu ya Sensa na kuhamasishwa washiriki kuhesabiwa Agosti 23 mwaka huu.

Wananchi wakiendelea kusikiliza elimu ya Sensa.

Elimu ya Sensa ikiendelea.

Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Mhe. Anne Makinda akiwa katika Mnada wa Olshinyanga kutoa elimu ya Sensa na kuhamasisha wananchi washiriki kikamilifu kuhesabiwa Sensa Agosti 23 mwaka huu.

Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi Anne Makinda akiwa katika Mnada wa Old Shinyanga kutoa elimu ya Sensa na kuhamasisha wananchi washiriki kikamilifu kuhesabiwa Sensa Agosti 23 mwaka huu.

Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi Mhe. Anne Makinda akiwa katika Mnada wa Old Shinyanga kutoa elimu ya Sensa na kuhamasisha wananchi washiriki kikamilifu kuhesabiwa Sensa Agosti 23 mwaka huu.


Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi  Mhe. Anne Makinda akiwasili katika Mnada wa Old  Shinyanga kutoa elimu ya kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa  ya watu na makazi Agosti 23 mwaka huu.

Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi Anne Makinda akiwa katika Mnada wa Old Shinyanga kutoa elimu ya Sensa na kuhamasisha wananchi washiriki kikamilifu kuhesabiwa Sensa Agosti 23 mwaka huu.
Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi Anne Makinda akiwa katika Mnada wa Old Shinyanga kutoa elimu ya Sensa na kuhamasisha wananchi washiriki kikamilifu kuhesabiwa Sensa Agost 23 mwaka huu.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Saturday, June 25, 2022

Mpendekezo ya ACT - Wazalendo Kuhusiana na Ajali ya Treni iliyotokea Mkoani Tabora.

Juzi, Jumatano 21, 2022 tulitoa taarifa ya awali kupitia akaunti za mitanao ya kijamii ya Msemaji wa sekta ya Habari na Uchukuzi wa ACT Wazalendo Ndg. Ally Saleh kwa kutoa pole kwa wananchi waliopata ajali ya Treni iliyotokea siku hiyo katika eneo la Malolo Mkoani Tabora. 

Ajali hiyo ilihusisha treni iliyokuwa ikifanya safari kati ya Kigoma na Dar es Salaam na chanzo chake kikielezwa ni kuwa hitilafu za miundombinu ya reli kutokana na uchakavu. Treni iliyopata ajali iliondoka stesheni ya Kigoma saa mbili usiku Jumanne Juni 21, 2022 kuelekea Dar es Salaam ikiwa na behewa nane zilizobeba abiria 930.

ACT Wazalendo pamoja na mambo mengine kwenye suala hili tumeona Takwimu za waathirika wa ajali hii zimekuwa na mkanganyiko mkubwa kati ya taarifa kutoka Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Shirika la Reli, Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Wahudumu wa Hospitali ya Kitete. Vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti kuwa ajali hiyo imesababisha vifo vya watu wanne (4) na majeruhi wapatao 205. 

Aidha, chanzo cha ajali hii haikijawekwa wazi na kutolewa maelezo ya kutosha na mapendekezo ya namna ya kukomesha tena kutokea kwa ajali kwa wakati mwingine. Tunafahamu umuhimu na mchango wa Usafiri wa reli nchini hususani kwenye Mikoa ambayo reli hii inahudumia kama vile Morogoro, Dodoma, Singida, Shinyinga, Mwanza na Kigoma kwa upande wa reli ya kati. 

Shirika la Reli, linasimamia Miundombinu ya Reli na uendeshaji mzima wa usafirishaji wa mizigo na watu kupitia usafiri huu, hivyo ilitarajiwa kuona shirika linashtushwa na kuguswa zaidi kutokea kwa ajali ambayo imeleta athari kubwa kwa wananchi kwa kutoa maelezo ya kutosha na hatua Madhubuti zitakazo rejesha Imani ya wananchi kuhusu usafiri huu.

Kinyume chake, Shirika la reli halijaipa uzito na kutoa hatua madhubuti za kushughulikia waathirika, kutoa taarifa za aendeleo yao, uchunguzi wa chanzo halisi cha ajali na kuimarisha kwa Miundombinu na nyenzo za usafiri wa reli. Kama tulivyotangulia kusema awali; taarifa yetu ya mwanzo ilikusudia kutoa pole, hivyo kutokana na taarifa ya sasa, 

ACT Wazalendo tunatoa mapendekezo yafuatayo ili kushughulikia waathirika na kuimarisha uendeshaji wa huduma ya reli nchini: 

i. Serikali isiwe inaficha takwimu halisi zinapotokea ajali kama hizi ili kuondoa mkanganyiko na kujulisha umma ukubwa wa ajali. 

ii. Serikali ilisimamie Shirika la Reli kuhakikisha kuongezeka kwa ubora wa huduma na usalama wa usafiri huo usioweza kukwepeka na wananchi wengi. 

iii. Abiria wote waliojeruhiwa wapatiwe matibabu bure kadri ambayo watayahitaji ili wapone kabisa na warudi katika kazi na maisha yao ya kawaida.

 iv. Serikali iandae utaratibu wa kutoa fidia kwa majeruhi watakao pata ulemavu wa kudumu na fidia kwa familia kwa wale waliopoteza maisha kutokana na ajali hii. 

v. Uchunguzi wa tukio hilo ufanywe kwa haraka na uweledi ili taarifa sahihi itolewe kwa umma. 

Imetolewa na; Ndugu Ally Saleh 

asaleh@actwazalendo.or.tz 

Msemaji wa Sekta ya Habari, Teknolojia ya Habari na Uchukuzi ACT Wazalendo

Saturday, April 14, 2018

SUMBAWANGA KUONJA VIBE KAMA LOTE LA TIGO FIESTA 2018

Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa, Bernard Makali(katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo kuelekea Tamasha la Tigo Fiesta litakalofanyika siku ya Ijumaa mkoani humo, Wengine kwenye picha ni Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Juu Kusini , Henry Kinabo (kushoto) na Msanii wa Bongo Fleva Nandy.

Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za Juu Kusini , Henry Kinabo akizungumza na waandishi wa habari leo kuelekea Tamasha la Tigo Fiesta litakalofanyika siku ya Ijumaa uwanja wa Nelson Mandela wilaya Sumbawanga. Wengine kwenye picha kulia  ni Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa, Bernard Makali, Msanii  Msanii wa Bongo Fleva Nandy na Mwisho kulia ni Katibu Tawala Msaidizi Idara ya Utawala, Winnie Kijazi  na kushoto Msanii, Nikki wa Pili 

Katibu Tawala wa mkoa wa Rukwa, Bernard Makali(katikati)akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wwafanyakazi wa Tigo na wasnii wataopanda leo kwenye jukwaa la Tigo Fiesta uwanja wa Nelson Mandela

Baada ya mafanikio ya ufunguzi wa msimu wa Tigo Fiesta 2018- Vibe Kama Lote mjini Morogoro, sasa ni zamu ya Sumbawanga na viunga vyake kufurahia vibe lote katika msimu mkubwa zaidi wa muziki na utamaduni nchini uliowasili mjini hapo na promosheni tatu kabambe, fursa za kibiashara kwa wakaazi wote pamoja na ahadi ya vibes moto moto kutoka kwa 100% wasanii wa nyumbani.  

Pazia la onesho hilo litakalofanyika katika viwanja vya Mandela mjini Sumbawanga litafunguliwa na wasaanii wanaochiopuka waliofanya vizuri katika shindano la kusaka vipaji la Tigo Fiesta 2018 – Supa Nyota. Wasanii wa kike Nandy na Maua Sama pia watakuwepo kukongo nyoyo za mashabiki, wakati wasanii wa hip-hop Fid Q, Bil Nas na kundi la Weusi linaloundwa na Joh Makini, Niki wa Pili pamoja na G-Nako nao watafunika onesho hilo. Mashabiki wa muziki pia wategemee kupata vibes za uhakika kutoka kwa wasanii wa bongo fleva Chegge, Jux, Whozu, Nedy Music, Barnaba na Marioo..
Mdhamini mkuu wa msimu huu, kampuni ya Tigo imewakumbusha mashabiki wote wa muziki mjini Sumbawanga kufurahia promosheni zake tatu murwa katika msimu hii wa vibes. ‘Data Kam Lote inawapa wateja hadi mara mbili ya vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#. Hii itawawezesha wateja wa Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+,’ Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Kusini Henry Kinabo alisema.

Tigo pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Kwa Sumbawanga, tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo wa Tigo Pesa Masterpass QR zitagharimu TSH 5,000 pekee badala ya TSH 7,000 kwa watakaonunua kwa pesa taslim, Wateja wanapaswa kupiga *150*01#  na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.

Wateja wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za kila wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya  http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia.

Katibu Tawala mkoa wa Rukwa, Bernard  Makali alielezea shukrani zake kwa waandaji kutoa fursa ya kuuitangaza wilaya hiyo akisema kuwa itaibua fursa nyingi zaidi za biashara na kujiongezea kipato kwa wakaazi.

Huu ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ambapo mwaka huu linashirikisha 100% wasanii wa nyumbani watakaozuru mikoa 15 ya nchi ikiwemo; Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku kilele kikifanyika Dar es Salaam.

Tuesday, April 3, 2018

AGNES MASOGANGE YAMEMKUTA-HII NDIO HUKUMU YAKE KUTOKA MAHAKAMANI LEO


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu video queen, Agnes Gerald ‘Masogange’ kulipa faini ya Shilingi Milioni 1.5 ama kwenda jela miaka 3 baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam. 


Kutokana na hukumu hiyo, Wakili wa utetezi Nehemiah Nkoko amesema kuwa watalipa faini. 

Thursday, March 15, 2018

VITUO MWENDO SITA VYAZINDULIWA DAR ES SALAAM NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI

Moja ya Vituo Mwendo vya Polisi vilivyozinduliwa leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), ambavyo vitatumika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kipolisi Kinondoni katika kuzuia na kupambana na uhalifu. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akisikiliza maelezo ya Kituo Mwendo cha polisi kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Jumanne Muliro (katikati), baada ya kuzindua moja ya vituo hivyo ambavyo idadi yake ni sita, lengo ikiwa vitumike katika maeneo ya mkoa huo kudhibiti uhalifu. Kulia ni Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Vituo Mwendo sita vya polisi ambavyo vimegawiwa kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuweza kuzuia na kupambana na uhalifu huku akiwaasa wananchi kujikita kwenye shughuli za maendeleo. Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Vituo Mwendo sita vya polisi ambavyo vimegawiwa kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuweza kuzuia na kupambana na uhalifu . Tukio hilo limefanyika leo, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


Thursday, March 8, 2018

MWENYEKITI WA MTANDAO WA WANAFUNZI ABDUL NONDO AOKOTWA IRINGA BAADA YA KUPOTEA KWA SIKU KADHAA

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) aliyekuwa hajulikani alipo tangu usiku wa kuamkia jana na kuacha ujumbe usemao “I AM AT HIGH RISK”, amepatikana Mafinga mkoani Iringa.
 Tokeo la picha la ABDUL NONDO
Mkurugenzi wa Idara ya Sheria ya Mtandao wa Wanafunzi Tanzania, Paul Kisabo amesema  kwamba Abdul Nondo amepatikana mkoani Iringa katika wilaya ya Mafinga jana jioni baada ya kuzinduka na kujikuta ametupwa barabarani.

“Nondo amepatikana Mafinga katika Kituo cha Polisi hivi punde, amezinduka na kujikuta akiwa ametupwa, akauliza watu eneo alipo ndipo wakamwambia yupo Mafinga, amejikokota na kuelekea kituo cha polisi kuripoti.

“Kilichomsaidia alikuwa anakumbuka namba mojaya dada yake ambayo alikuwa ameikariri kichwani, ikabidi aombe simu polisi, kumpigia dada yake ambaye naye alijulisha baba yake mdogo aliyepo Dar es Salaam kuwa ndugu yao amepatikana.

“Nondo ameongea na baba yake mdogo kupitia simu ya polisi na kudai kuwa laini zake zote za simu lakini simu yake bado anayo na yupo salama,” -Paul Kisabo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire amethibitisha kupatikana kwa mwanafunzi huyo, Abdul Nondo na kusema sasa bado yupo katika Kituo cha Polisi Mafinga akitoa maelezo.

Friday, March 2, 2018

TUNATAKA KATIBA YENYE KUWEZA KUPINGA MATOKEO YA URAIS - PROF. BAREGU

                    

Tuesday, February 27, 2018

ANGALIA HAPA KUJUA KILICHOTOKEA KATIKA KONGAMANO LA WANAWAKE NA UONGOZI

Wanawake kote nchini wametakiwa kuacha tofauti zao, wakae pamoja na kuangalia changamoto zinazowakabili na watafute namna ya kuzitatua ili waweze kusonga mbele.
Mbunge wa Hanang Mkoani Manyara Dkt. Marry Nagu akiongea na wanawake kutoka mikoa mbalimbali walioudhuria kongamano la wanawake na uongozi lililoandaliwa na TGNP Mtandao Mapema leo jijini Dar es salaam.
Hayo yamesemwa mapema leo jijini Dar es salaam na Mh. Merry Nagu alipokuwa akifugua kongamano la siku moja la wanawake na uongozi lililoandaliwa na Mtandao wa jinsia TGNP.

Kongamano hilo lililofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam liliudhuliwa na watu wengi mashuhuri na wenye mchango mkubwa kwa taifa kama Mama Anna Makinda, Marry Rusimbi, Ester Bulaya Prof. Ruth Meena nk.

Katika kongamano hilo Marry Nagu alipenda kuwashauri kwa wale wanawake waliopata nafasi nzuri waweze kuzitumia nafasi hizo katika kuwanufaisha wanawake wenzao kama alivyofanya yeye.

“Wanawake wenye nafasi nzuri katika uongozi mnatakiwa kuzitumia nafasi hizo kuwakomboa wanawake wenzenu kama nilivyofanya mimi nilipokuwa Waziri wa Utumishi kwa kuweza kubadilisha sharia ya utumishi kutoka sharia ya serikali mchakato kwenda serikali matokeo” alisema Marry Nagu

“Katika ushiriki wa wanawake kwenye uongozi bado kuna changamoto katika kuchaguliwa au kupigiwa kura lakini wanawake tunatakiwa kuonyesha kwamba tunaweza na tuweze kutiana moyo wenyewe kwa wenyewe, kwani hii itawapa msukumo hata wanaume kuweza kutupigia kura kwa kuona umoja wetu” alisema Marry Nagu

Aidha Marry Nagu alipenda kuwashauri wanawake kuwa haitoshi kwa kusema wao ni wachakalikaji au wabangaizaji kwani mwisho wa siku wanakuwa hawana chochote wanachokipata na hivyo wanatakiwa kuwa wajasiliamari ili kujiongezea kipato katika maisha yao ya kila siku.

Na mwisho kabisa alipenda kumpongeza Rais Magufuri kwa kuona mchango na umuhimu wa wanawake katika serikali yake hata kumchagua Mama Samia Suluhu Hassan kuwa makamu wake, hii inaonyesha kwa kiasi gani rais anasogeza mbele harakati za wanawake.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mapema leo katika Kongamano la Wanawake na Uongozi lililoandaliwa na Mtandao huo Mlimani City jijini  Dar es salaam.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi alisema kuwa lengo la Kongamano hilo ni kujumuika, kushauriana/ kuelimishana kuhusu changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake kote nchini.

Mkurugenzi huyo aliendelea kusema kuwa bado wanawake hawapewi nafasi ipasavyo kwani takwimu zinaonyesha kuwa hadi kufika oktoba 11 2017 wanawake waliyoweza kushika madaraka kama wakuu wa nchi ni 11 kati ya 178 na kwa afrika ni mwanamke mmoja tu ndio kiongozi wa juu yaani Rais.

Lakini pia Rwanda imekuwa ya kwanza kwa afrika mashariki na kidunia kwa asilimia 61.3 na Tanzania imekuwa ya pili kwa Afrika Mashariki lakini ya 25 kidunia kwa kuwa na asilimia 36.9 hivyo hali bado siyo nzuri katika usawa wa kijinsia.

Aidha Mkurugenzi huyo aliendelea kusisitiza swala la wanawake kuwezeshwa kiuchumi hii ikiwa ni pamoja na kazi za huduma ambazo zimekuwa ni kama majukumumu ya kawaida kwao bila kupata kipato chochote, wakati muda huo wangeutumia kutafuta kipato wengeweza kujenga uchumi wa nchi.

Na mwisho Lilian alipenda kushauri kuwa wanawake wapewe nafasi katika uongozi na maamuzi ili waweze kuonyesha uwezo wao katika Nyanja hizo kwani ushiriki wao umekuwa ni mdogo sana ukilinganishwa na wanaume kama wakuu wa Wilaya, Wabunge, Mawaziri na Wakuu wa Mikoa.

Mwenyekiti wa bodi wa TGNP Mtandao Visencia Shule akimkalibisha Mgeni rasmi ambaye pia ni Mbunge wa Hanang mkoani Manyara  Mama Marry Nagu mapema leo katika kongamano la wanawake na uongozi lililofanyika Mlimani City jijini Dar es salaam.
Waziri mstaafu ambaye pia Mbunge wa jimbo la Hanang mkoani Manyara Marry Nagu akijaribu kuwatia moyo wanawake wanaotamani kuwa kama yeye au watu wengine wakubwa ndani na nje ya Tanzania katika kongamano la wanawake na uongozi mapema leo jijini Dar es salaam .

Wageni mbalimbali waliofika katika Kongamano la Wanawake na uongozi lililoandaliwa na TGNP Mtandao mapema leo jijini Dar es salaam




                            ANGALIA HAPA KUJUA MENGI ZAIDI..
                   

Sunday, February 25, 2018

TGNP MTANDAO KUFANYA KONGAMANO KUBWA LA WANAWAKE NA UONGOZI FEBRUARY 27 MWAKA HUU

NA VICENT MACHA - DAR ES SALAAM

SERIKALI imetakiwa kuzitambua kazi za kutoa huduma zinazotekelezwa na wanawake na kuziingiza katika Mipango ya Taifa kwani zinaweza kusaidia kuongeza pato la Taifa.

Hayo yamesemwa mapema leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia (TGNP) Bi. Lilian Liundi alipokuwa akitoa Mhuktasari wa Kongamano la Wanawake na Uongozi.

Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika siku ya jumanne ya tarehe 27 Mlimani City jijini Dar es salaam, likihudhuliwa wanawake mbalimbali walio katika nafasi za uongozi na waliostafu.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa kuna haja ya serikali kuzitambua shughuli mbalimbali zinazotolewa na wanawake kama huduma kwa lengo la kujipatia kipato kwani uchunguzi umebaini kuwa wanawake hutumia muda wa masaa 10 mpaka 15 kwa siku kwa shughuli hizo hivyo wanakosa muda wa kufanya shughuli za kujipatia kipato.

Aidha Mkurugenzi huyo aliendelea kusema kuwa lengo kuu la Kongamano hilo ni wanawake kwa pamoja kuweza kujadili namna gani wataweza kuongeza nafasi za uongozi na maamuzi kwani bado hawajaweza kufikia lengo ambalo ni 50 kwa 50.

Lakini pia kuweza kusherekea, kupongezana na kuajadili changamoto mbalimbali anazokutana nazo mwanamke katika Nyanja ya elimu, afya na umiliki wa ardhi swala ambalo bado ni changamoto kubwa kwa wanawake wengi hivi sasa.

Bi. Lilian aliendelea kusema kuwa kutakuwa na kuenzi na kukumbuka mchango uliotolewa na wanawake ambao walikuwa katika ngazi za uongozi maamuzi kuanzia ngazi ya jamii mpaka taifa.

Mgeni Rasmi katika Kongamano hilo anatarajiwa kuwa Waziri msataafu Mama Marry Nagu, lakini pia kutakuwa na wadau zaidi ya 250 wanawake kwa wanaume viongozi wa sasa na wastaafu katika kuhakikisha kongamano hilo linaleta tija kwa jamii yetu.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mapema leo jijini Dar es salaam katika mkutano na waandishi kuhusu kongamano la Wanawake Uongozi.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao Lilian Liundi wa katikati akiwa na jopo la wafanyakazi wa shirika hilo pamoja na wadau mbalimbali walioshiriki katika kuandaa Kongamano la Wanawake na Uongozi.
Waandishi wa habari wakiendelea na kazi yao.

ANGALIA HAPA KUJUA MENGI ZAIDI KUHUSU KONGAMANO HILO....
                         

Thursday, February 22, 2018

MSIBA WA AKWELINA WAOMBOLEZAJI WAJA JUU KUSHINIKIZA WAZIRI MWIGULU NA IGP SIRRO KUACHIA NGAZI

Baadhi ya waombolezaji katika ibada ya kuaga mwili wa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, yakiwamo ya kumtaka waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro kujiuzulu.

Ibada hiyo imefanyika leo Februari 22, 2018 katika viwanja vya NIT, Mabibo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu, wakiwamo viongozi mbalimbali wa Serikali.

Waombolezaji hao walinyanyua mabango hayo baada ya waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako aliponyanyuka kutoa salamu kwa wafiwa kama walivyofanya viongozi wengine, akiwamo mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Baadhi ya ujumbe katika mabango hayo ni; “muuaji hawezi kujichunguza na Mwigulu, Sirro kwa mauaji haya bado mko ofisini.”

Juhudi za kuwataka waombolezaji hao kushusha mabango ziligonga mwamba kutokana na baadhi ya watu waliokuwa karibu yao kuja juu, wakitaka waachwe kwa maelezo kuwa wana haki ya kufanya hivyo.
Katika salamu zake za rambirambi, Profesa Ndalichako alisema: “Rais Magufuli ameshaagiza uchunguzi ufanyike na mimi kama waziri nasisitiza vyombo vinavyohusika vifanye uchunguzi haraka.

“Matukio ya aina hii hayapaswi kuendelea, nimehuzunika kwa msiba huu na naomba Watanzania waungane kuiombea familia.”