Tuesday, September 18, 2012

Mh. Pinda alazimika kutumia PIPOZIII.......POWER kumaliza hotuba yake

Jana hapa Mwanza, waziri mkuu alikuwa akihitimisha ziara yake mkoani Mwanza ambayo mbali na kuligarimu taifa kwa matumizi ya hela kutokana na msafara mrefu uliokuwepo, lakini umemalizika kwa fedheha kubwa kwa upande wa waziri mkuu.

Waziri alikuwa na ratiba ya kuhutubia wananchi viwanja vya Sahara, katika kuhutubia kwake, maneno yote ya chama chake hayakupokelewa na wananchi walikusanyika kumsikiliza, ilimbidi atumie maneno ya CHADEMA kumaliza hotuba yake.

CCM OYEE......watu kimya, PIPOZIII......power tena kwa shangwe kubwa.

Na ilikuwa ajbu pale Wenje alipotaka kuhutubia kwani alifikishwa jukwani kwa kubebwa.