Friday, October 5, 2012

SERENGETI BOYS KUVUNJA KAMBI KWA MECHI

    Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) ambayo
imepata tiketi ya kucheza raundi ya tatu ya michuano ya Afrika baada ya Misri
kujitoa itavunja kambi yake kwa mechi ya kirafiki dhidi ya kikosi cha Yanga cha
U20.

     Mechi hiyo itachezwa kesho (Oktoba 6 mwaka huu) Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni. Kiingilio kwenye
mechi hiyo kitakuwa sh. 2,000 tu.

TAFCA YAONGEZA MUDA WA KUCHUKUA FOMU
Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA)
imeongeza muda kwa wagombea kuchukua fomu kwa ajili ya uchaguzi wa chama hicho
utakaofanyika katikati ya mwezi ujao.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati
ya Uchaguzi ya TAFCA, Ramadhan Mambosasa, jana ndiyo ilikuwa mwisho wa kuchukua
fomu lakini mwitikio wa wagombea umekuwa mdogo ambapo ni watano tu
waliojitokeza. Hivyo, amesema wameongeza muda wa kuchukua na kurudisha fomu
ambapo mwisho itakuwa ni Oktoba 9 mwaka huu saa 10 kamili alasiri.

Fomu
zinapatikana ofisi za TAFCA ambazo ziko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es
Salaam. Nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu,
Katibu Msaidizi, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, Mhazini na wajumbe watatu wa
Kamati ya Utendaji.

Boniface Wambura Ofisa Habari Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF

No comments: