Thursday, October 11, 2012

MWANZA KUFURIKA NA VIBE KAMA LOTE LA TIGO FIESTA 2018

Mkuu wa Mkoa Wa Mwanza, Mhe. John Mongella akizungumza na waandishi wa habari leo kufungua rasmi pazia la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote litakalofanyika jumamosi hii uwanja wa CCM Kirumba Mkoani humo. Wengine pichani kushoto ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa,Uthman Madati na Msanii Nikki Wa Pili.

Mkuu wa Hifadhi ya Kisiwa cha Saanane kilichopo mkoani Mwanza, Beatrice Kessy akizungumza na waandishi wa habari na Wasanii watakaopanda jukwaa la Tigo Fiesta kesho jumamosi kuhusu umuhimu wa watalii na watanzania kutembelea kisiwa hicho.


Msanii wa Bongo Fleva, Nikki Wa Pili akizungumza na wanahabari jinsi alivyojipanga kutoa burudani kwenye tamasha la Tigo Fiesta kesho Jumamosi.

 Mkuu wa Mkoa Wa Mwanza, Mhe. John Mongella akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tigo na wasanii wataopanda kwenye jukwaa la Tigo Fiesta uwanja wa CCM Kirumba kesho.


Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa, Uthman Madati akizungumza na Waandishi wa habari leo kwenye mkutano wa uzinduzi wa Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote mkoani Mwanza. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella, Msanii Nikki wa Pili na Meneja wa Masoko Tigo Mkoa wa Mwanza, Kassimu Azziz.

Msanii wa Bongo Fleva, Wakazi akizungumza na wanahabari jinsi alivyojipanga kutoa burudani kwenye tamasha la Tigo Fiesta kesho Jumamosi uwanja wa CCM Kirumba.

Wakaazi wa Mwanza kufurahia ofa murua ya Data Kama Lote inayowapa wateja hadi mara mbili ya thamani ya intaneti watakayonunua kutoka Tigo

 Jumamosi hii, jiji la Mwanza linatarajiwa kufurika na vibe kama lote kutoka kwa wasanii 100% wanaokonga nyoyo za mashabiki wa msimu huu wa Tigo Fiesta 2018- Vibe Kama Lote.

Baada ya wiki saba ambazo zimeshuhudia msimu huu mkubwa zaidi wa kitamaduni katika ukanda wa Afrika ya Masahariki na Kati ukizuru miji ya Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Njombe, Mtwara, Songea na Moshi, Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote sasa imetua katika fukwe za Ziwa Victoria na ipo tayari kutifua vumbi katika viwanja vya CCM Kirumba leo Jumamosi tarehe 27 Oktoba.

Waandaaji wa tamasha hilo, kampuni ya Clouds Media group wamesema vibes katika jiji la Mwanza zitaongozwa na msanii Fid-Q ambaye ni mzaliwa wa jiji hilo, akisindikizwa na kundi la Weusi, Rostam, Wakazi na Rich Mavoko. Wasanii wengine watakaopagawisha siku hiyo ni Jux, Barnaba, Whozu, Nandy, Aslay, Country Boy, Nedy Music, Nkunda Star pamoja na Jay Melody. Mwanza pia itashuhudia vibes kutoka kwa Mchama the Best, Jolie, Benson watakaotanguliwa na washindi wa shindano la kusaka vipaji la Tigo Fiesta Supa  Nyota.

Akiashiria kuanza kwa msimu huu wa vibes jijini Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alizungumzia uwepo wa fursa za biashara zinazoambatana na msimu huo. “Wamiliki wa kumbi za starehe, hoteli na nyumba za kulala wageni, mam ntilie, wauza maji na wamiliki wa vyombo vya usafiri ikiwemo bodaboda wote wana fursa kubwa ya kujiongezea kipato kwa sababu tunaratajia maelfu ya wageni kufurika jijini Mwanza katika kipindi hiki,’ alisema.

Hali kadhalika, kampuni ya Tigo imewakumbusha wakaazi wa Mwanza wazikose kufurahia promosheni murwa ya Data Kama Lote itakayowapa bonasi ya hadi mara mbili kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#. ‘Hii itawawezesha wateja wa Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+,’ Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Ziwa, Uthman Madati alisema.

Tigo pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Kwa tamasha la Mwanza litakalofanyika, tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo wa Tigo Pesa Masterpass QR zitagharimu TSH 8,000 pekee badala ya TSH 10,000 kwa watakaonunua kwa pesa taslim, Wateja wanapaswa kupiga *150*01#  na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.

Wateja wa Tigo pia wanaweza kujaribu umahiri wao wa kujibu maswali yanayohusiana na msimu wote wa vibes kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia.  Washindi wanajinyakulia zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya  http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia.

Huu ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ambapo mwaka huu linashirikisha 100% wasanii wa nyumbani wanaozuru mikoa 15 ya nchi. Baada ya Mwanza, tamasha hilo linahamia Musoma kabla ya kutua  Muleba, Kahama, Arusha Singida na Dodoma, huku kilele kikifanyika jijini Dar es Salaam.

No comments: