KIKWETE AZINDUA VITAMBULISHO VYA TAIFA


Raisi wa jamhuri wa Tanzania dk JAKAYA MRISHO KIKWETE amewaasa viongozi wanaotumia mchakato wa vitambulisho vya taifa kwa ubinafsi na kwa manufaa yao wenyewe na kusahau kuwa mchakato huo ni kwa wananchi wote wa Tanzania waache mara moja.


 


Raisi KIKWETE ameyasema hayo leo jijini dar es salaam alipokuwa akifanya uzinduzi rasmi wa mchakato wa utoaji wa vitambulisho vya taifa kwa watanzania ambao tayari wamekwisha jiandikisha,amesema kuwa moja kati ya mambo yaliyochelewesha zoezi hilo ni baadhi ya viongozi kutumia zoezi hilo kutaka kujinufaisha wenyewe


 


Raisi KIKWETE amesema changamoto nyingine inayokumba zoezi hilo la utoaji wa vitambulisho vya taifa ni ukosefu wa fedha za kutosha jambo ambalo ameahidi serikali itahakikisha inatoa fedha za kutosha kufanikisha zoezi  hilo kwa wakati.


 


Raisi kikwete amewataka watanzania  kuendelea kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha ili waweze kupata vitambulisho hivyo jambo ambalo ametaja litakuwa na manufaa mengi kwa wananchi.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.