Thursday, March 21, 2013

WAGUNDUZI watakiwa kugundua VITU VITAKAVYOWASAIDIA WANANCHI KATIKA JAMII: DK. MWERU

 




 

Watafiti nawanasayansi nchini Tanzania wametakiwa kufanya tafiti za kiungunduzi ambazozitaleta manufaa na kusaidia jamaii ya watanzania .

Hayo yamesemana leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dr. Mwele Malecela(pichani juu)wakatiwa semina ya siku moja ya wagunduzi mbalimbali iliyoandaliwa kwa pamoja kati yaNIMR na Shirika la Grand Challenges la




nchini Canada.

Dkt. Malecela amesema umefika wakati sasa kwa wagunduzi mbalimbali wa Kitanzaniakuanza kungundua njia mbalimbali za kuweza kutatua matatizo yaliyopo katika jamii hasa katika sekta ya afya.

Semina hiyo ya siku moja ilikuwa na lengo la kuhamasisha wangunduzi sekta ya afyaambapo baadhi ya wanasayansi wagunduzi kadhaa walitoa taarifa zao za awali za namna ya kukabiliana na matizo kadha hasa kwa Mama na mtoto.

Wagunduzikadhaa waliweza kuzungumzia gunduzi zao katika semina hiyo na miongini mwa hizoni pamoja na ile ya hali ya Utapiamlo unaofanywa na Dkt. Magreth Kagashe kutokaTaasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Bianadamu Ifakara ambayo inafanyika katika Vijiji vya Kilombero.

Ugunduzimwingine ni wa namna ya kusafisha maji na kuyaweka katika hali salama kupitianjia ya Takasa maji, na kuyaweka taika hali salama nay a usafi ugunduzi unaofanyana Kijakazi Mashoto na Ugunduzi mwingine ni matumizi ya Maua ya Rosella katika kukabiliana na Upungufu wa damu kwa mama na mtoto.

Dkt.Malecela amesema ya kuwa ugunduzi unaofanyika sasa na kupewa fedha na GrandChallenge ya Canada unatakiwa uwe ugunduzi ambao utaleta mabadiliko na kubadili maisha ya wananchi.

“Maranyingi wanasayansi wamekuwa wakifanya tafiti mbalimbali na kugundua matatizomengi katika jamii lakini mara chache watafiti hawa wametafuta suluhisho yahayo matatizo au magonjwa katika jamii hizo …kwahiyo hivi sasa wanasayansi wagunduziwa kitanzania umefikia hatua ya kugundua vitu ambavyo vitasaidia jamii,” alisemaDkt.Malecela.

Aidha nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Grand Challenge Canada, Peter Singer alisema kuwa
jumlya ya miradi 16 ya ugunduzi inayofanywa na wanasayansi wa kitanzania
itapatiwa fedha kupitia taasisi hiyo.




Afisa
Mtendaji Mkuu wa Grand Challenge Canada, Peter Singer akizungumza na waandishi
wa habari mara baada ya semina hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya NIMR jijini Dar
es Salaam leo.



Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dr. Mwele Malecela
akipiga picha na Afisa Mtendaji Mkuu wa Grand
Challenge Canada, Peter Singer mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari Makao
Makuu ya NIMR jijini Dar es Salaam leo.






No comments: