Sunday, April 14, 2013

HAWA NI KATI YA WATU MAARUFU WACHACHE WALIOUWAWA


jikumbushe kidogo





Rapper Tupac Hip Hop msanii aliyotokea kupendwa sana na vijana hata watu wenye umri mkubwa kwa jinsi alivyokuwa akitetea watu wenye hali ya chini. Tupac alishambuliwa kwa risasi Septemba 7, 1996 akiwa ndani ya gari, alikuwa na umri wa miaka 25, Tupac alikufa siku sita mbele toka aliposhutiwa. Mwili wake ulichomwa na washkaji wa waliokuwa wakiunda kundi la OutLwaz baadae wakavuta bangi iliyochanganywa na majivu ya mwili wa Tupac  Marvin Gaye muimbaji bora kabisa wa RnB ambae ameshafanya ngoma kali kama “I heard it through the grapevine” “You are all I need to get by” na “Let’s get it on”. Muimbaji huyu mahiri wa RnB alifariki tarehe 1 Aprili 1984 baada ya milongo miwili akifanya vizuri katika muziki wake uliokuwa unapendwa sana. Kifo chake haikuwa ajali, ila alipigwa risasi mara mbili na baba yake na bundiki ambayo alipewa na baba yake kama zawdi ya Krisimasi.



            Alizaliwa akiitwa Christopher George Latore Wallace katika gemu la muziki alifahamika kamaThe Notorious B.I.G Big Smalls, alifariki kwa kupigwa risasi tarehe 9 Machi, 1997 miezi sita tu baada ya kifo cha Tupac Amar Shakur, watu walidhani labda kifo chake alihusika Tupac lakini Polisi walisema hawadhani kama kuna hali ya Tupac kuhusika, alipigwa risasi huko Los Angeles. Hawa ni wachache kati ya celebrities wengi waliouwawa.




No comments: