.

UNYAMA WA KUTISHA .BABA AMZIKA MWANAE CHINI YA MEZA SEBULENI AKIWA HAI.SAMAHANI KWA PICHA HIZI.kwa hisani ya maasinda blog

MKASA wa baba kumuua mwanae kwa kumzika akiwa hai kutokana na mgogoro wa ndoa, umezidi kuibua mapya, baada ya mama mzazi wa marehemu ,Debora Riziki (3), kusimulia mkasa mzima .
Marehemu Debora Riziki miaka 3 enzi za uhai
wake
Riziki Mwangoka
kulia anaetuhumiwa kumzika mtoto wake akiwa hai


Hapa
maiti ya mtoto Debora ikiwa imetolewa nnje mara baada ya kufukuliwa ndani ya
nyumba ya baba yake mzazi


Mwili wa marehemu Debora  ukionyeshwa kwa mzazi na
kudhibitisha kuwa ndiye mwenyewe aliyemfukia
Hatimae sasa Debora anazikwa

mama mzazi wa debora
MKASA wa baba kumuua mwanae kwa kumzika akiwa hai kutokana na mgogoro wa ndoa, umezidi kuibua mapya, baada ya mama mzazi wa marehemu ,Debora Riziki (3), kusimulia mkasa mzima .

 

Akizungumza kwa hisia kali, katika mahojiano maalumu  na Mbeya yetu kijijini kwake Ibula, katika kata ya Kiwira, wilayani Rungwe, Mama mzazi wa Marehemu, Esther Mwambenja, alisema kabla ya tukio hilo kutokea kulikuwa na viashiria vingi vya mumewe kufanya ukatili.

 

Alisema  tukio la mzazi mwenza huyo kumwiba mtoto  na kwenda kumfanyia  ukatili huo wa kinyama lilikuwa la pili, baada ya awali kumuiba akiwa na miaka miwili na miezi mine na alimrudisha kwa maandishi ya serikali ya kijiji.

 

Alisema katika tukio la kwanza la mtalaka wake huyo kumuiba mtoto wao huyo, lilitokea Septemba mwaka 2012, baada ya wiki chache za kumfukuza katika nyumba waliyokuwa wakiishi katika kitongoji cha Iponjola, kijiji cha Asenga, nyumba iliyotumika kuzikwa mtoto huyo.

 

Alitaja sababu za yeye kufukuzwa ni ugomvi uliotokana na yeye kuhoji  sababu za kuficha fedha kiasi cha sh. 120,000 zilizotokana na wao kwa pamoja kufanya  kazi ya kibarua katika mashamba kijijini hapo na baada ya malipo kutolewa mtalaka wake huyo alionesha kiasi kidogo cha sh.80,000.

 

Alisema ugomvi huo ndio ulisababisha  yeye arudishwe kwa wazazi wake, lakini baada ya muda mfupi mwanaume huyo  alimfuata na kumbembeleza ili warudiane na alipogoma aling’ang’ania aondoke na mtoto .

 

“Nakumbuka ilikuwa Novemba mwaka jana baada ya mimi kuondoka nyumbani kwake na kurudi kuishi hapa nyumbani, siku hiyo tukiwa shambani huyo bwana alikuja hapa nyumbani na kumkuta mwanangu wa kwanza (Neema Steven ) niliyezaa na mwanaume mwingine” alisema Mwambenja.

 

Alisema baada ya kufika eneo hilo majira ya saa mbili asubuhi alitumia ujanja na kufanikiwa kumuiba mtoto na kisha kutokomea naye kijijini kwao Asenga, hali ambayo ilisababisha kutoa taarifa kituo cha polisi Kiwira.

 

“Unajua kuwa baada ya kwenda kutoa taarifa polisi walitusaidia kufika kijijini kwao ambapo serikali ya kijiji ilikubali nimchukue mwanangu kwa kuwekeana mkataba wa kisheria kwa mujibu wa sheria, kwani alikuwa chini ya miaka saba”.

 

Aliongeza kuwa  Novemba 15 mwaka 2012 serikali ya kijiji chini ya Mwenyekiti, Lutengano Mwakyoma na mashahidi watano wakiwemo wazazi na ndugu zake, walinikabidhi barua ya kuridhia kuondoka na mwanangu, huku ikimuonya mume wangu kutorudia kosa hili la kumuiba mtoto hadi hapo atakafikisha miaka saba.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.