Wednesday, April 3, 2013

WAISLAMU NA WAKRISTO WASABABISHA BALAAA TENA TUNDUMA,,, MABOMU YA MACHOZI YARINDIMA KISA NI SWALA LA UCHINJAJI



 

Taarifa  kutoka
Tunduma mkoani Mbeya zinadai  kuwa hali  si shwari katika eneo hilo kutokana na
kuzuka kwa  vurugu kubwa zinazodaiwa kusababishwa na
masuala ya  kiimani ya nani achinje kati ya mkristo na Muislam
.


Mwandishi   wetu  kutoka Tunduma mkoani Mbeya  anaripoti kuwa 
vurugu  hizo zimeanza  majira ya saa nne asubuhi  kwa makundi  ya vijana 
kuandamana mitaani na kuvutana  kuhusu uamuzi  wa viongozi  wa dini ya kikristo
Tunduma  kuandika barua kwa mkuu  wa wilaya  kutaka  kuruhusiwa kuchinja  wakati
wa pasaka.

Ripota  wetu anaripoti   kuwa kabla ya  ijumaa kuu  viongozi
hao  wa dini ya Kikristo  walikutana na mkuu  wa  wilaya  ya Momba Abuud Saibea
ambae  aliwataka kuwasilisha barua rasmi ya  kutaka  kibali  cha  kuchinja
.

Hata hivyo inaelezwa  kuwa  vurugu  hizo za  leo zina mikanganyiko 
mingi  kwani  wanaoshiriki katika  vurugu  hizo ni vijana  wapiga debe
.....

Vurugu za  uchinjaji  zilifanyika  siku ya Pasaka  na hazikuwa na
mvutano  kwa sababu wakristo  walichinja katika bucha zao na  waislamu nao 
walichinja katika mabucha yao ....

Cha kushangaza leo ni baada ya 
kuibuka  kundi  la  vijana  wanaofanya kazi katika stendi na vijiwe mbali mbali
ambao  ndio walioanzisha  vurugu kiasi cha  polisi  kuingilia kati kwa kutumia
mabomu ya machozi na kuwatawanya  wananchi  waliokuwa wamekusanyika maeneo mbali
mbali .

Kutokana na vurugu  hizo mpaka  wa Tunduma  ambao unaingia nchi 
za kusini  mwa Tanzania  ulifungwa  pamoja na magari yaliyokuwa yakitoka 
Sumbawanga  pia  yalizuiwa  kuendelea na  safari hadi hali  hiyo  ilipotulia
mida ya saa 8 mchana baada ya kamanda wa polisi wa mkoa  wa Mbeya  Diwani
Athuman  kufika  eneo

HABARI KWA HISANI YA MAASINDA BLOG

 

 

No comments: