Friday, May 31, 2013

MGOGORO WA WALIMU NA SERIKALI BADO UPO PALE PALE -CWT


 


        Chama cha walimu tanzania (CWT) kimewataka wabunge kuwa makini wakati wa kujadili bajeti ya wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi , na kutambua kuwa mgogoro kati ya walimu  na serikali kuhusu madai ya nyongeza za mishahara waliyokuwa wanayadai bado haujamalizika.
        Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam raisi wa chama hicho GRATIAN MUKOBA amesema ikumbukwe kuwa mgogoro huo uliotangazwa na chama cha walimu mnamo mwaka jana haukufikia suluhu badala yake serikali ilikimbilia mahakamani kusitisha mgomo huo na kuruhusu mazungumzo ambayo amesema hadi sasa mazungumzo hayo bado hayajaonyesha mafanikio
          Bw MUKOBA Amesema kuwa kumekuwa na maneno mengi ambayo yamekuwa yakisemwa na serikali kuwa mgogoro huo umemalizika jambo ambalo amesema sio kweli na kuwataka wanachama wa CWT kuendelea kuvuta subira wakati majadiliano yanaendelea na kama hayatafikia muafaka watatoa tamko rasmi
          Aidha ameyataja baadhi ya madai ambayo walimu wamekuwa wakiyadai kutoka kwa serikali kuwa ni ongezeko la mishahara asilimia 100,kurudishwa kwa posho ya kufundishia asiilimia 55 kwa walimu wa sayansi na asilimia 50 kwa walimu wa sanaa,pamoja na posho ya asilimia 30 kwa walimu wanaofanya kazi katika mazingira magumu.

picha na maktaba

No comments: