Friday, May 31, 2013

SAMAHANI KWA PICHA,VIBAKA WAMFANYIA UNYAMA KIJANA HUYU..MWILI WAKE NUSU UTEKETEEE KWA MOTO


KUMRADHI KWA PICHA HIIKijana Ismai Mayoba(31)anaefanya kazi Bar ya Mangrove, mkaazi wa Jamhuri, Manispaa ya Lindi, akiwa katika ward namba 6 hospital ya Sokoine -Lindi baada ya kuchomwa moto na vibaka

Na Abdulaziz Lindi 

Kijana Ismai Mayoba (31) anaefanya kazi Bar ya Mangrove,Mkazi wa Jamhuri Manispaa ya Lindi ambaye amenusurika kifo baada ya kuvamiwa na kundi la Vijana waliotaka kumpora na hatimae kumchoma moto amelazwa katika Hospital ya Sokoine Mjini humo.

Kufuatia tukio hilo,Jeshi la Polisi wilayani Lindi limefanikiwa kumkamata mmoja kati ya watuhumiwa saba waliohusika na tukio hilo lilitokea katika eneo la Mtaa wa Congo.

  Akithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kukamatwa kwa mtuhumiwa,Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi,Renatha Mzinga alimtaja ndg Ally Manially(22)mkazi wa mtaa wa Kongo kuwa anashikiliwa na Jeshi hilo na atafikishwa mahakamani leo kujibu shitaka la kujeruhi na kujipatia pesa kwa njia ya Udanganyifu ikiwa pamoja na kumchoma mwenzie moto huku akijua ni kosa kisheria.

Aidha Mzinga alieleza kuwa Jeshi la polisi linaendelea kutafuta watuhumiwa wengine 6 waliohusika na tukio hilo Taarifa zaidi tutawaletea kuhusiana na tukio hilo.

No comments: