.

TAARIFA YA IKULU 
     Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa dokta JAKAYA MRISHO KIKWETE amewapandisha vyeo maafisa kadhaa wa jeshi la polisi kuwa makamishna wa polisi(CP) na manaibu kamishna wa polisi (DCP)
            
       Katika taarifa iliyotolewa leo ikulu jijini dar es salaam imewataja waliopandishwa kuwa makamishna ni ISAYA  MUNGULU na SULEMAN KOVA ambao kabla ya vyeo vyao vipya walikuwa manaibu kamishna wa pilisi

    Aidha waliopandishwa kuwa manaibu kamishna wa polisi ni  ELICE MAPUNDA,BROWN LEKEY,HAMDAN OMAR MAKAME,KENETH KASSEKE,ABDUL RAHMAN KANIK,THOBIAS ANDENGENYE,ADRIAN MAGAYANGE,SOSPETER KONDELA,SIMON SIRO NA ERNEST MANGU.ambapo kabla ya uteuzi huo maafisa hao walikuwa makamishna wasaidizi waandamizi wa polisi
 
     Katika taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi huo unaanza mara moja

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.