Wednesday, May 29, 2013

UTAFITI WANGU.HAWA NDIO WASANII WALIOWAHI KUTAJWA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYIA,YUMPO MAREHEMU NGWEAR



           Kifo cha malkia wa muziki wa Pop, RnB na Soul wa Marekani, Whitney Elizabeth Houston kilichochangiwa na matumizi ya madawa ya kulevya, chaibua mchakato mpya ambapo imepelekea kutolewa kwa orodha ya wasanii wa bongo flavaz wanaodaiwa kwa watumizi wa Mihadarati. Mihadarati iliyotajwa ikiwa ‘unga’, bangi, miraa na aina nyengine.

         Habari za chini kwa chini zinadai kuwa kwa sasa mastaa kibao wanatumia madawa ya kulevya huku majina makubwa kama Msafiri Sayai ‘Diouf’, Albert Mangwair, Langa Kileo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, Waziri Makuto ‘Lord Eyez’, Fareed Kubanda ‘Fid Q’, Aisha Mbegu ‘Madinda’, Khaleed Mohamed ‘TID’, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’, Abas Kinzasa ‘20%’, David Nyika ‘Daz Baba’, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Happiness Thadei ‘Sister P’ na Rose Ndauka yakitajwa.

           Katika orodha hii Fid Q ndiye msanii wa pekee aliyejitokeza wazi wazi kukana madai haya.huku langa akikiri kutumia na kusema ameacha

            Huku sanaa ya bongo flavaz ikiimarisha juhudi za kukabiliana na tabia ya utumizi wa Mihadarati miongoni mwa wasanii wa Bongo, wakereketwa wa mziki wa Mombasani pia wahimizwa kuiga juhudi hizi ili kumaliza tabia hii miongoni mwa wasanii wa mkoa wa pwani.

Niwazi kwamba kuna baadhi ya wasanii wa pwani ambao wameonekana wazi wazi wakitumia madawa mbali mbali katika sehemu za burudani hususan kabla ya kufanya performance.

No comments: