Thursday, May 30, 2013

VURUGU ZA BUNGENI CHANZO HIKI HAPA


Kufuatia hotuba ya Wenje bungeni kutuhumu chama cha cuf kuwa ni chama cha kishoga, mbunge wa CUF amesimama na kuwaita chadema ni wehu, wahuni, wazushi, mashoga na kwamba wameidhalilisha cuf...


           Mbunge huyo wa CUF ameomba spika achukue hatua za dhidi ya chadema asipofanya hivyo cuf watachukua hatua dhidi ya Chadema na bunge..

Kumetokea vurugu bungeni ambapo spika ameliahirisha bunge hadi jioni.

Hiki ni Kipande cha hutuba hiyo ambacho nimekitoa Jamii Forums:
"Mheshimiwa Spika, kwa upande wa chama cha CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo wa Kiliberali ambazo miongoni mwa misingi yake mikuu ni pamoja na “kupigania haki za ndoa ya jinsia moja, usagaji na ushoga”. Hii ni kwa mujibu wa tangazo lao kwenye mtandao wao wa umoja wa maliberali ulimwenguni, likiungwa mkono na Waziri wa Haki na Usawa wa Uingereza, Lynn Featherstone kutoka chama cha Liberal Democrats wakati chama hicho(www.liberal-international.org) kilipokuwa kinapitisha azimio la kuruhusu ndoa za jinsia moja kama haki ya mtu mmoja mmoja, wanashirikiana na vyama kama vile LPC ya Canada, Det Radikale Venstre cha Norway, FDP cha Ujerumani, Israel Liberal Group cha Israel,PDS cha Senegal na Liberal Democrats cha Uingereza. 

        Kutokana na umoja huo, CUF wamekuwa wakipata msaada wa kifedha na nyenzo nyingine mbalimbali kutoka kwa vyama hivyo vya mrengo wa Kiliberali na msaada wa mwisho ni hivi majuzi mwezi Machi 2013 waliposaini makubaliano na chama cha Kiliberali kutoka Norway. 

          Mheshimiwa Spika, kwa upande wa CHADEMA, wapo kwenye Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia Ulimwenguni (International Democratic Union - IDU). Huu ni umoja wa vyama ambavyo vipo kwenye mrengo wa kati na ambavyo msingi wake mkuu ni pamoja na kuwa na familia, kama taasisi muhimu katika jamii, ikimaanisha kwamba: “tunapinga vitendo vyote vya ushoga na usagaji”. Tunatetea demokrasia, haki za binadamu na kupambana na ufisadi katika serikali. Vyama wanachama wa umoja huu ni pamoja na Conservative Party cha UK, CPP cha Norway, Republican cha Marekani na vingine vinavyofuata mrengo huo. 


             Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, inavitaka vyama vyote ambavyo vimekuwa na mahusiano na vyama vya nje viweke wazi mikataba yao na malengo ya mahusiano hayo ikiwa ni pamoja na misaada ambayo vimekuwa vikipokea kutoka kwenye nchi hizo "

No comments: