Tuesday, June 25, 2013
kidokezo------JE WAJUA KUWA GHARAMA ZA SIMU ZINAPANDA KUANZIA JULAI MOSI
Kufuatia kuongezwa kwa kodi katika huduma za simu za mkononi , gharama za huduma hizo zinatajiwa pia kuongezeka kuanzia Julai Mosi mwaka huu. Taarifa ya pamoja iliyotolewa jijini Dar es salaam na Umoja wa Makampuni ya Simu za Mkononi Tanzania – MOAT imesema pendekezo la serikali la kuweka kodi ya 14.5 kwenye huduma za simu za mkononi hazitoweza kukwepesha kupanda kwa gharama za simu kwa watumiaji.
MOAT inasema awali kodi ilikuwa ikitozwa asilimia 12.5 katika huduma ya mawasiliano ya simu na kwmaba ongezeko la kufiikia asilimia 14.5 tofauti na nchi za jirani Kenya na Uganda ambazo zimeendelea kutoza viwango vya ushuru vya asilimia 10 na 12.5 tu ni mzigo kwa watumiaji wa huduma za simu za mkononi.
Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2013 unaainisha, huduma za mawasiliano kuwa ni; “huduma yoyote ya maelezo inayotolewa na makampuni ya mawasiliano ya simu kwa njia ya mawasiliano kwa kutoa au kupokea sauti, maandishi, na picha au taarifa ya aina yoyote kupitia mfumo wa kielektronikia,” imesema taarifa hiyo iliyosainiwa na Vodacom, Airtel, Tigo na Zantel
MOAT imesema eneo mojawapo litakaloathirika ni huduma za Intaneti eneo amablo linahitaji kuwekewa mikakati ya kulikuza kutokana na umuhimu wake katika maisha ya sasa kiuchumi na kijamii na wala siyo kulizorotesha kwa kusababisha ongezeko la gharama na hivyo kuendelea kuwa na kiwango cha cha matumizi kilinganishwa na baadhi ya nchi nyengine zikiwemo za Afrika Mashariki. “Hatua hii ya kuongeza kodi itakwenda kinyume na mipango iliyopo yenye lengo la kuibadili jamii kwa kuipatia maarifa ya msingi kupitia huduma ya intaneti sambamba na mawasiliano ya simu.”
Kwa mujibu wa MOAT, Tanzania ni kati ya nchi zenye kiwango cha chini ya matumizi ya huduma ya mtandao wa intaneti katika bara la Afrika ambapo watumiaji wa huduma hiyo ni asilimia 10 pekee ikilinganishwa na nchi jirani ya Kenya ambayo ina zaidi ya watumiaji asilimia 40. Aidha, MOAT imeongeza kuwa, “mawasiliano ya simu si anasa bali ni huduma muhimu katika Tanzania ya leo, sasa tunawezaaje kuwatozakodi mara kwa mara watu hao hao ambao wanaitegemea huduma hiyo ili kuboresha maisha yao? Ilihoji taarifa hiyo ya MOAT.
Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa kwa tozo la kodi ya mapato ya asilimia 35 kwenye sekta hiyo ya mawasiliano ya simu linatosha kiasi ya kwamba sekta hiyo isngeweza kubeba mzigo zaidi wa ongezeko jingine. Hivi sasa, upanuzi wa mawasiliano na miundombinu vijijini ndiyo kipaumbele cha sekta nzima. Tunaamini hapa ndipo ukuaji wa sekta ya mawasiliano ya simu itakapoonekana katika miaka ijayo. Ongezeko lolote la kodi litazorotesha uwezo wetu wa kutanua huduma zetu za mawasiliano na miundombinu maeneo ya vijijini, imesema MOAT.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment