Wednesday, June 26, 2013

SABABU ZILIZOFANYA SUGU KUACHIWA JANA

http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2012/09/Joseph-Mbilinyi-Mr-11.jpg

            KUHUSU Joseph Mbilinyi 'Sugu', Mbunge wa Mbeya Mjini. Ni kweli alikuwa polisi Dodoma, alikoitwa kwa madai ya kutoa lugha ya matusi kwa Ndugu Mizengo Pinda, lakini hajaandikisha maelezo, kwa sababu 3, zifuatazo:

1. Wakili wake, Tundu Lissu, amewaambia kuwa Polisi hawawezi kumkamata na kumhoji Mbunge Sugu, iwe ukumbini, maeneo ya bunge, au nje ya maeneo ya bun
ge, wakati bunge likiendelea, kutokana na parliamentary immunity aliyonayo hadi polisi watakapofuata taratibu zinazotakiwa.

2. Neno hilo wanalotuhumu kuwa ni lugha ya matusi, si tusi kwa sheria za nchi yetu, bali linaweza kutumika kwa vitu au mtu anayefanya matendo au kusema maneno yanayostahili kuitwa hivyo.

3. Wakili wake (Tundu Lissu) kawauliza, nani mlalamikaji katika tuhuma hizo, je wamepokea malalamiko ya Ndugu Pinda mwenyewe ? Majibu yalikuwa ya kigugumizi"

1 comment:

Unknown said...

police wa Tz ni Wagonjwa tu,