Sunday, July 28, 2013

KONGAMANO LA AMANI DAR--JESHI LATUHUMIWA KUWABAKA KINAMAMA WA MTWARA



     


         WAKATI LEO KUKIWA KUMEFANYIKA KONGAMANO KUBWA SANA LA AMANI JIJINI DAR ES SALAAM KATIKA CHUO KIKUU KATIKA UKUMBI WA NKURUMA,KONGAMANO HILO LIMEIBUA MAMBO AMBAYO MENGINE KAMA NI KWELI YAMETOKEA BASI NI AIBU KATIKA TAIFA

         AKIZUNGUMZA WAKATI AKICHANGIA KATIKA KONGAMANO HILO NAIBU KATIBU MKUU WA CHAMA CHA WANANCHI CUF  JULIUS MTATIRO  AMELISHUTUMU JESHI LA TANZANIA LILILOKWENDA MTWARA KUIMARISHA ULINZI WAKATI ULE WA MVUTANO WA GESI NA KUDAI KUWA JESHI HILO LIMEENDESHA ZOEZI LA UBAKAJI KWA KINAMAMA WA MKOA HUO KIPINDI KILE CHA VURUGU

         AMESEMA KUWA ANATAMBUA KUWA JESHI LA TANZANIA LINA SIRI NYINGI SANA JUU YA HAYO ILA ANA USHAHIDI WA KUTOSHA KUWA JESHI HILO LILIFANYA UCHAFU HUO NA CHAMA CHAKE KILIKUTANA NA MAMA AMBAYE ALIFANYIWA KITENDO HICHO NA DACTARI KUDHIBITISHA KUBAKWA KWA MAMA HUYO JAMBO AMBALO LIMEPINGWA VIKALI NA MWAKILISHI WA JESHI HILO ALIYEHUDHURIA KATIKA KONGAMANO HILO

          AIDHA KABLA YA BW MTATIRO KUTOA TUHUMA HIZO NAYE KATIBU MKUU WA CHADEMA MH DK SLAA AMBAYE NAYE ALIHUDHURIA WAKATI AKICHANGIA AMELITUPIA LAWAMA JESHI LA POLISI NA MAJESHI MENGINE KWA KUENDESHA VITENDO VYA KIHUNI KATIKA VURUGU ZA MTWARA NA KUWAASA KUACHAMARAMOJA MAMBO HAYO KWANI NI UONEVU WA WAZI KWA WANANCHI,HUKU AKISEMA   KUWA ANA USHAHIDI WA MAMBO AMBAYO ANAYAZUNGUMZA.

KATIKA KONGAMANO HILO LILIHUDHURIWA NA VIONGOZI MBALIMBALI WA KISIASA PAMOJA NA WA SERIKALI AMBAPO KATIKA SERIKALI ILIWAKILISHWA NA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MH NCHIMBI AMBAPO WAKATI AKIFUNGA KONGAMANO HILO AMEKANUSHA TAARIFA HIZO ZA JESHI KUWABAKA BAADHI YA WANAWAKE WA MTWARA NA KUSEMA KUWA YEYE NDIYE WAZIRI HUSIKA NA HANA TAARIFA KAMA HIZO NA HAJAWAHI KUSEMA KITU HICHO NA KUWATAKA WATANZANIA KUTISIKILIZA MAMBO YANAYOSEMWA BALI WAFANYE UTAFITI WA MAMBO HAYO

MH  NCHIMBI AMEUPONGEZA UONGOZI WA UDASA KWA KUANDAA MDAHALO HUO AMBAO PIA AMESEMA USIWE MWISHO BALI UWE NI MWANZO ILI WATANZANIA WAPATE NAFASI YA KUIJADILI AMANI YAO MIAKA HAMSINI IJAYO

No comments: