Thursday, July 25, 2013

WIZI WA MIZANI ZA MADUKA NA MABUCHA WAKIDHIRI WATANZANIA WATAHADHARISHWA

MENEJA WA VIPIMO WA WAKALA WA VIPIMO BW MESHAKI KADEGE AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM


             WAKALA WA VIPIMO TANZANIA IMEWATAHADHARISHA WATANZANIA NA WATU WANAOTUMIA MEZANI ZA MADUKA ZA KUPIMIA VITU MBALI MBALI KWA KUWAIBIA WATANZANIA KWA KUZIHARIBU MASHINE HIZO ILI ZIPIME NA KUTOA VIPIMO AMBAVYO SIO VYA KWELI


               AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DA ES SALAAM MENEJA WA WA SEHEMU ZA UPIMAJI WA WAKALA HAO BW MESHACK KADEGE  AMESEMA KUWA SASA HALI HIYO IMESHAMIRI SANA KATIKA MADUKA MENGI HAPA TANZANIA KWA WENYE MADUKA NA WALE WA MABUCHA YA NYAMA WANAOTUMIA MIZANI KUPIA MIZIGO YAO KUFANYA HIVYO


A MESEMA KUWA WATU HAO HUARIBU KWA MAKUSUDI MIZANI HIZO AMA KUTUMIA MAWE YA KIPIMA AMBAYO HAYANA UZITO SAHIHI HIVYO KWA WATEJA WENYE HARAKA NA WASIOELEWA KUIBIWA KILA SIKU. 


              WAKALA HAO WAMEWATAKA WATANZANIA KUWA MAKINI PINDI WAENDAPO DUKANI KUKAGUA KWANZA MIZANI HIZO KABLA YA KIPIMIWA BIDHAA NA MUUZAJI KWANI WEZI NI WENGI NA KILA SIKU WANAONGEZEKA KATIKA MIJI YETU

BW MESHAK AKIONYESHA MOJA KATI YA JIWE AMBALO LIMEKAMATWA MTAANI LIKIWA NA MUUNDO KAMA WA MAWE YA KILO MBILI KUMBE NI KILO MOJA NA NUSU

No comments: