JJI LA DAR LAACHANA NA UDA


 

Meya wa jiji la dar es salaam mh didas masaburi leo ametangaza rasmi kwa serikali kujiondoa rasmi katika saka a uda na kuuza hisa zake zote ilizokuwa nazo katika shirika hilo.

akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam mh masaburi amesema kuwa uamuzi huo umetokana na sababu nyingi ikiwemo kushindwa kumudu deni kubwa ambalo shirika hilo linadaiwa kwa sasa
aidha amesema kuwa sababu nyingine ni kuwa hakuna sababu ya kuwa na shirika hilo kwani tayari serikali inaendesha mradi mkubwa wa mabasi yaendayo kwa kasi

uamuzi huo umetolewa katika kikao ambacho kimewakutanisha viongozi wa jiji na kuamua kuwa jiji liuze hisa zake 51 ilizokuwa nazo katika shirika hilo na kujiondoa rasmi katika mgogoro huo

katika hatua nyingine jiji limeagiza mwekezaji simon group alipe hisa zisizogawiwa kwa bei ya soko yani 1618.

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.