Saturday, August 17, 2013

UNYAMA,MWANAMKE ABAKWA,KISHA KUUAWA KINYAMA HUKO SHINYANGA

         Picture 

           Mwanamke mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 30 amekutwa amekufa katika makaburi ya Majengo katika soko la mjini Kahama mkoani Shinyanga huku mwili wake ukiwa ametobolewa macho na kuonesha kupigwa na kitu kizito usoni.

            Mwanamke huyo ambaye hajatambulika jina lake wala anakotoka, alikuwa amevaa blauzi nyeusi yenye madoa meupe, viatu vyenye urembo wa rangi ya fedha, ni mnene kiasi, mweusi na mwenye nywele ndefu.

           Mwili wa Mwanamke huyo amegunguliwa leo majira ya saa sita mchana baada ya watu waliokuwa wanachimba kaburi kuuona mwili huo pembeni ya eneo hilo na kutoa taarifa kwa Polisi.

           Majirani wanaoishi eneo la makaburi hayo wanahisi unyama huo umefanyika usiku wa kuamkia jana huku, baadhi ya akina mama wakikiri kusikia sauti ya mwanamke akipiga yowe katika eneo la mnadani.

              Jeshi la Polisi wilayani Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku mrakibu msaidizi wa Polisi Aziz Mayunga akitoa wito kwa wananchi kufika katika chumba cha kuhifadhia maiti ili kuutambua mwili huo.HABARI KWA HISANI YA http://sangafesto.blogspot.com/

 KUTOKANA NA MAADILI HA KITANZANIA NA BLOG YENU HATUWEZI KUWEKA PICHA ZOTE ZA MAREHEMU  KAMA UNATAKA KUZITAZAMA ZOTE TIZAMA HAPO http://bundalawilliam.blogspot.com/2013/08/mwanamke-abakwa-na-kuingiziwa-kitu.html

No comments: