Thursday, September 19, 2013

BREAKING NEWZZ--POLISI YAPIGA MARUFUKU MAANDAMANO YA WAPINZANI JUMAMOSI

              Jeshi la poisi kanda maalum ya dar es salaam limetangaza asm kuyapiga marufuku maandamano yaliokuwa yafanyike siku ya jmamosi jijini dar es salaam maandamano ambayo yalikuwa yameandaliwa na muunganiko wa vyama vitatu vya upinzxani nchini yenye leo la kupinga mchakato wa katiba nchini

     Akizungumzaa leo jijini dar es salaam kamishna wa kanda hiyo SULEMANI KOVA amesema kua wamefikia hatua hiyo baada ya kukaa na viongozi wa vyma hivyo vitatu na kukubaliana kuwa wasifanye maandamano na badaala yake wafanye mkutano pekee.

         Aamesema kuwa mktano ambao utafanyika siku ya jumamosi uwanja wa jangwani ni halali na utalindwa na jeshi la polisi hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi kabisa katika swala la usalama,katika mkutano huo utawakutanisha CUF,CHADEMA ,pamoja na NCCR-MAGEUZI


            Katika hatua ningine jeshi hilo limefanikiwa kukamata gari la majambazi ambao walikuwa wamehifadhi mabox ya sigara ambayo ni ya wizi jijini dar es salaam
KAMISHNA KOVA AKIONYESHA GARI HILO
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA AMBAZO HAZINA UBORA WA UHAKIKA

No comments: