Friday, September 20, 2013

MAJANGA-MCT YABAINI VYUO FEKI VYA UANDISHI WA HABARI NCHINI YAVIPA MIEZI MIWILI KUKIDHI VIGEZO



KATIBU WA BARAZA LA HABARI TANZANIA MH KAJUBI MUKAJANGA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM
           Baraza la habari tanzania MCT limefanya ukaguzi katika vyuo vinavyotoa elimu ya uandishi wa habari nchini tanzania na kugundua kuwa vyuo viwili tuu ndio vilivyokidhi vigezo vya kutoa mafunzo hay hapa nchini

           Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam katibu wa baraza hilo bw KAJUBI MUKAJANGA amesema kuwa ukaguzi huo umefanyika baada ya kugundua kuwa kuna baadhi ya wamiliki wa vyuo wamekuwa wakitoa elimu ambayo haistahili pamoja na kupokea malalamiko mengi kutoka kwa waandishi wa habari kuwa wamekuwa wakipokea wanafunzi ambao hawajui kitu

          Amesema kuwa vyuo viwili tuu ndio vimekidhi vigezo vya kuendelea kutoa elimu kwa kutumia mtaala wa nacte ambavyo amevitaja kuwa ni A3INSTITUTE OF PROFESSIONAL STUDIES cha jijini dar es salaam,pamoja na ARUSHA JOURNALISM TRAINING COLLEGE kilichopo arusha.

          Amesema kuwa vyuo vingine ambavyo havijakidhi vigezo hivyo vimepewa muda hadi mwezo wa 12 kutimizaa masharti huku akuvutaja kuwa ni DSJ,TSJ,ROYAL COLEGE,INSTITUTE OF SOCIAL MEDIA,PAMOJA NA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI ZANZIBAR

Aidha baraza hilo limetoa onyo kali kwa watua ambao wanaanzisha vyuo vya uandishi wa habari kwa lengo la kujipatia fedha na kushindwa kuvisimamia akisema kuwa hatua kali juu yao zitachukuliwa.
MKURUGENZI WA MAFUNZO KUTOKA BARAZA HILO PILI MTAMBALIKE AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI PIA

No comments: