Tuesday, September 10, 2013

WALIMU TANZANIA WAUPINGA MPANGO WA BIG RESULT NOW,WASEMA HAUWASAIDII WALIMU,WAPENDEKEZA PIA SERKALI TATU KATIKA KATIBAra

RAISI WA CWT AKIFAFANUA JAMBO WAKATI AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI
        Chama cha walimu tanzania CWT kimesema kuwa mpango wa serikali wa big result now ulioanzishwa na serikali hauna tija kwa walimu na hauwezi kufanikiwa kwani walimu hawajashirikishwa na serikali katika mpango huo.

       Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar  es salaam raisi wa chama hicho GRASIAN MUKOBA amesema kuwa katika mpango huo walimu ndio watekelezaji wakubwa japo hawakushirikishwa katika mpango huo

     Aidha amesema kuwa madai ya walimu ambayo wamekuwa wakiidai serikali tangu muda mrefu ni lazima wasikilizwe ili mpango huo uweze kutekelezwa.ambapo amesema hadi ufikia sasa walimu wanaidai serikali zaidi ya bilion 39 jambo ambalo amesema kuwa linawakatisha tamaa walimu katika kutekelezza maujkum yao.

Hata hivyo pia bw MUKOBA amesema kuwa chama cha walimu bado kipo katika mazungumzo na serikali kuhusu madai yao na kama hawatasikilizwa itabidi watumie njia nyingine katika kudai.

MUKOBA AKIZIDI KUTIRIRIKA

       Aidha katika hatua nyingine chama cha walimu kimetoa maoni yao juu ya rasimu ya katiba mpya huku katika aswala la muungano wakipendekeza serikali tatu.

No comments: