Thursday, October 10, 2013

MGOMO WA MALORI BANDARINI HATARI,TANI 23165 ZA MIZIGO ZAKWAMA KWENDA ZAMBIA,MELI 15 ZIPO BAHARINI,BANDARI KWA SASA IMEJAA

KAIMU MENEJA WA MAWASILIANO MAMLAKA YA BANDARI TANZANIA BI JANETH RUZANGI AKIZUNGUMZA NA WAANDIAHI WA HABARI MAPEMA LEO
      Mamlaka ya bandari tanzania imekiri kuwa mgomo unaondelea sasa wa malori nchini umewaletea madhara makubwa sana katika utendaji wao wa kazi ambapo zaidi ya tani 23165 za mzigo aina ya molea ambao kiasi kikubwa ulikuwa usafirishwe kwenda zambia umekwamba bandarini hadi sasa.

       Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam kaimu meneja wa mawasiliano kutoka TPA  JANETH RUZANGI amesema kuwa hadi sasa meli 15 zipo baharini zikisubiri kupakuliwa huku bandari hiyo ikiwa imejaa kutokana na mizigo ambayo ingetakiwa kuondolewa na malori kutkuondolewa hapo.

   Bi RUZANGI amesema kuwa kama hali itaendelea hivyo ya mgomo basi hali itakuwa mbaya sana kwa watumiaji wa mizigo hiyo na wamiliki wa meli hizo kwani wataanza kutozwa faini

No comments: