.

TUKIO JINGINE LA UTAPELI JIJINI DAR: MATAPELI WAWILI WAKAMATWA MMOJA WAO AKUTWA NA KITAMBULISHO CHA IDARA YA USALAMA WA TAIFA...! PICHA 11 ZA TUKIO ZIMA HIZI HAPA

 Kava ya nje ya Kitambulisho hicho kinaonekana namna hii.
    Watu wawili wanaotuhumiwa kuwa ni wezi a.k.a Wapigaji/Matapeli wamekamatwa usiku huu kwenye hoteli ya Picolo,Kawe jijini Dar es Salaam.

    Watu hao ambao wamekamatwa ni Bw. Takula Mayenga mkazi wa Mbezi Temboni na Bw. Juma Hamis ambaye ni mkazi wa Tabata wakiwa na nyaraka tofauti ikiwemo kitambulisho kinachotaja kuwa ni cha Idara ya Usalama wa Taifa, kadi za benki pamoja na simu zaidi ya kumi,wakiwa katika harakati za kumtapeli mwanadada mmoja aliejitambulisha kwa jina la Rebecca ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo cha Biashara cha CBE,Mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaa .


Akisimulia tukio dada huyo ambaye alipatwa na tukio hilo la kutapeliwa Ijumaa ya wiki iliyopita alisema kuwa, ilikuwa ni Ijumaa iliyopita wakiwa wamekaa katika fukwe wakipunga upepo ndipo alipokuja tapeli huyo na kukaa nao na baadae aliwawekea madawa ya kulevya na kuondoka na dada huyo kwenda kumtupa baharini.About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.