Monday, November 25, 2013

KAMA ULIKOSA HOTUBA YA ZITO NA KITILA MKUMBO JANA ZOTE HIZI HAPA SOMA MWENYEWE USIKUBALI KUSIMULIWA



Na Karoli Vinsent
    
    MBUNGE wa kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ameibuka na kujibu mapigo na kusema haondoki Chadema.
        ENDELEA HAPO CHINI---------

        Hayo aliyasema jana  jijini Dar es salaam wakati akizungumza na Waandishi wa Habari pamoja na Wahariri Zitto alisema kwa sasa hanampango wa kuondoka chadema kama watu wanavyosema na kusema kuwa yeye atakuwa mtu wa mwisho kuondoka
“Nawahakikishia siwezi kuondoka chadema na kama kuondoka mimi nitakuwa mtu wa mwisho kukihama chadema,siwezi nikahama Chadema akati nimejiunga tangu na miaka 16 mimi nimepanda miti ya hiki chama mpaka leo kimestawi harafu nikihame haitowezekana”alisema Kabwe
        
        Kuhusu kufukuzwa uongozi wa Chadema,Zitto Kabwe alisema mpaka sasa hajapata barua kutoka kwa Viongozi wa Chama kuhusu kufukuzwa kwake katika uongozi na kuongeze kuwa yeye anachosubilia ni barua hiyo
“Mimi nichosubili ni barua kutoka kwa viongozi wa Chadema wananiambie wameniengua katika Uongozi na Sababu waziweke hadharani,na mimi nitachukua hatua ya kukata rufaa sehemu zengine”alisema zitto
          
       Vilevile Kabwe alimtaka Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu ambae pia ni Mbunge wa singida Mashariki, atoe ushahidi kama Zitto kabwe anahusika katika Ripoti hiyo ya siri,
     
       Zitto aliongeza na kusema Lissu amevunja kanuni za Chama katika kutoa hukumu hiyo
“Ukisoma vipengere mbalimbali vya katiba ya Chadema inasema wazi kuhusu kumuengua kiongozi pamoja na kumfukuza mwanachama,ni pamoja na kumpa mda wa kujitetea pamoja na kuonyesha ushahidi wa kosa lenyewe lakini leo Chadema hawajafanya hivyo wametoa mahamuzi ambayo yako nje ya Katiba ya chadema”alisema Kabwe
       
        Kwa upande mwingine Zitto Kabwe amefadhaishwa sana hari ya kisiasa ndani ya chama cha Chadema na kusema kuwa hali hiyo haitasaida kujenga chama bali ndio itakuwa inakishusha chama hicho
“Siasa za Majungu ndani ya Chadema haita kisaidia Chama na hari hii Chadema inapitia katika sehemu ngumu sana Chadema si chama Cha kwanza kupitia hali hii ni vyama vingi sana vinapitia katika hali hii,na hali hii ni ishara tosha kabisa kuwa ni kukomaa kwa Demokrasia na kikipa nguvu chama’”alisema kabwe

KUHUSU DK KITILA MKUMBO KUENGULIWA NAFASI YA UONGOZI

Kwa upande wake kitila mkumbo yeye alisema amefadhaishwa na maamuzi ya wajumbe wa mkutano mkuu na kusema hawajafuata haki
“mimi sijakubalina na maamuzi ya wajumbe kwani hawajafuhata haki katika maamuzi haya kwani katiba ya chama hiko wazi katika kuwaengua viongozi lakini leo chadema hawajafata vipengere kama kumpa mwanachama au kiongozi kujitetea pamoja na ushahidi wa kile anachokifanya na huo walaka ambao tunahukumiwa uko sahihi”alisema Mkumbo

Vilevile kuhusu hoja ya kukihama Chama Mkumbo alisema kwa sasa hatokiahama chama  cha chadema na hataendeleo kupigania hati ya watanzania na hatua chama hicho kinapitia ni hatua ya kukijenga chama na chama chochote duniani cha kisiasa  kinapita sehemu hiyo

KUHUSU WALAKA WA  SIRI KUHUSU MABADILIKO YA CHADEMA

    Kuhusu hoja ya walaka  mbunge Zitto Kabwe pamoja na Mhadhiri mwandamizi kutoka chuo kikuu cha mrimani Dokta Kitila Mkumbo wote kwa pamoja waliunga mkono yale yalioandikwa ndani walaka huo na kuongeza kuwa kama mtu anayependa mabadariko lazima haukubali walaka huo

“Mimi sikuwaikusoma walaka huo niliuona mala ya kwanza kwenye mkutano mkuu wa chama juzi na nilipousoma nikaukubari walaka huo na kuvikubali vipengere vyote vilivyoandikwa katika walaka huo”Alisema Zitto Kabwe

Kwa upnde wa Dk Mkumbo alisema walaka huo umeandikwa mahasusi kwa ajiri ya kukijenga chama cha Chadema
“Walaka huu unaonyesha taswira  ya kukijenga chama chetu kukitoa katika mfumo wa kidikteta na kukifanya kiwe chama cha nchi nzima”alesema Mkumbo
Katika hali ya kushangaza Waandishi wa habari walimbana Dk Mkumbo hawataje watu waliohusika katika kuandaa walaka huo lakini Dk huyo aligoma kuwataja wenzake na kusema kuwa kila mtu ajitangaze mwenyewe kwa wakati wake

Mwandishi wa Blogs hii aliushuhudi walaka huo ikiwa pamoja na kuusoma walaka huo huku walaka huo ukionyesha udhaifu mkubwa katika Chama hicho cha siasa chadema na katika suala la uongozi na kuonyesha chama hicho akina uwazi wa mapato na mtumizi ya pesa pamoja na viongozi wa juu wachadema katika kuchezea katiba ya Chama hicho ili waendelee kubaki daima
      
      Taarifa ya chamaAkitangaza uamuzi wa Kamati Kuu jana Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu alisema, Zitto, Dk Mkumbo na Mwenyekiti wa Chadema mkoani Arusha, Samson Mwigamba walikuwa na mtandao wa kukiua  chama hicho, huku wakitengeneza tuhuma za kuwachafua  Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Katibu wake, Dk Willbroad Slaa.

     Alisema kuwa kamati kuu ilibaini kuwapo kwa mkakati mkubwa wa watu hao kutimiza malengo hayo ambao umeandikwa katika waraka unaoitwa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’, ambao umeandaliwa na kikundi kinachojiita ‘Mtandao wa Ushindi’.
“Kikundi hicho vinara wake wapo wanne, Zitto anajulikana kama Mhusika Mkuu (MM), Mkumbo (M1), Mwigamba (M3) na mtu mwingine wa nne hatujamtambua kwa sasa yeye anatumia jina la M2” alisema Lissu.

     Alisema wakati wa kuhojiwa na Kamati Kuu Dk Mkumbo alikiri kuwa mhusika mkuu wa mtandao huo ni Zitto, lakini Zitto alikana kuutambua waraka huo licha ya kueleza unamhusu kwa kuwa umetaja jina lake, kauli ambayo alidai Kamati Kuu haikutaka kuiamini.

      Huku akieleza jinsi watu hao walivyokuwa wakiwasiliana na kupanga mikakati ya kuimaliza Chadema kwa siri chini ya ufadhili wa fedha kutoka kwa Zitto, Lissu alisema Naibu Katibu Mkuu huyo wa zamani alikuwa akitumiwa na Chama Tawala (CCM) kuimaliza Chadema.
“Mkakati wa Mabadiliko 2013 ni mpango haramu na ambao unaichanachana katiba ya chama chetu. Ni mkakati wa vita dhidi ya chama chetu na utaratibu wetu wa kikatiba.
Alisema Kamati Kuu itakutana kwa dharura kwa ajili ya kufanya uamuzi juu ya hatima ya watuhumiwa hao
     
         KUHUSU RIPOTI YA SIRI KUHUSU ZITTO KABWE
          KWA upande wa ripoti ilyosambazwa kwenye mitandao ya kijamiii kuhusu Zitto Kabwe kushirikiana na Viongozi wa Juu wa Usalama wa Taifa katika kukihujuma Chadema Ripoto hiyo iliyojulikana kama “Ripiti ya Siri kuhusu Zitto Kabwe

     Zitti Kabwe alisema yeye alipousoma walaka huo aliwasiriana na viongozi wa chama na kuwauliza wao kama wana utambua walaka huo na wao wakakanusha kile kilichoandikwa kwenye walaka huo
“Mimi nilipousoma ripoti hiyo nikawasiliana na viongozi wachama na kutaka kuja kama wao wanahusika katiaka ripoti hiyo ila wao kwa pamoja wakakanusha kama chama kinahusika kuuandaa walaka huo na kusema ni hila zinazofanywa na CCM pamoja na jkushirikiana na usalama wa Taifa”alisema Zitto Kabwe

    Vilevile  Zitto kabwe aliongeza na kusema kuwa kwa sasa anatawachukulia hatua viongozi wote wa chadema waliohusika katiaka kusambaza walaka huo,ikumbukwe mwandishi wa blog hii aliripoti kuwa walaka huo unasambazwa kwenye blogs ya kiongozi wa Chadema na jina tumeliifadhi

                     KUHUSU POSHO
                             
       KUHUSU posho Kabwe alisema apokei posho toka mwaka 2008 na anafanya hivyo ili kupinga posho zinazotolewa bungeni kwenye vikao vyake pamoja na Shuguli za Kamati na kufafanua kuwa posho hizo zingeenda kwasaidia wa mama wajane wanaojifungulia vichakani kwa kukosa hospitari na zingeelekezwa kwenye kujenga shure.


        Kwa zaidi ya wiki mbili Zitto amekuwa akilumbana na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuhusiana na masuala ya posho.
Vita hiyo ilianzishwa na Lema katika kikao cha wabunge wiki iliyopita aliposema kuwa Zitto anafanya unafiki kukataa posho.
Alimtuhumu mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kwamba anakataa posho za vikao bungeni, lakini anapokea posho nyingi kutoka mashirika mbalimbali ya kijamii nchini.

        Lema aliweka tuhuma hizo kwenye Mtandao wa Jamii Forum huku akisema suala hilo halihitaji vikao vya chama kulijadili isipokuwa vyombo vya habari na hususan, mitandao ya kijamii kwani hata Zitto hutumia mitandao hiyo.

       Zitto alijibu kuwa tangu siku nyingi alikwishapiga marufuku kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kupokea posho kutoka taasisi au mashirika yanayosimamiwa na kamati hiyo.

      Alisema tangu alipokuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), alipiga marufuku posho na pia aliwahi kuwashtaki Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) wabunge wanaochukua posho kutoka taasisi za Serikali.
  
     Zitto pia alipata msukosuko mwingine baada ya kusambazwa ripoti inayoitwa ‘Taarifa ya Siri ya Chadema’ iliyomtuhumu kuwa alikuwa anashirikiana na CCM na viongozi wa Idara ya Usalama wa Taifa kuihujumu Chadema.

      Pia, Zitto aliingia katika malumbano na chama chake baada ya kutuhumu vyama vya siasa kuwa hesabu zake hazikaguliwi na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), huku akitaka ruzuku kwenye vyama hivyo isimamishwe.

     Chadema ilipinga vikali madai hayo na kueleza kuwa imekuwa inatumia taasisi binafsi kufanya kazi hiyo. Vyama vinavyopata ruzuku ya Serikali ni vile vyenye wabunge Chadema, CCM, UDP, TLP, CUF na NCCR-Mageuzi.
MWISHO

No comments: