Wednesday, November 6, 2013

RAIS KIKWETE KUHUTUBIA BUNGE KESHO



Rais Jakaya Kikwete, kesho machana anatarajiwa kulihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma.

Kutokana na tukio hili na zuito unaoambatana nalo, Serikali imewaelekeza Mawaziri na Manaibu Waziri kutotoka nje ya Dodoma hadi hapo Rais atakapokuwa amehutubia Bunge. Kadhalika safari zote za Kamati za Bunge ambazo zilikuwa katika mchakato wa kutekelezwa zimeahirishwa hadi baada ya kesho, ili kutoa fursa kwa wabunge wote kuwapo wakati wa hotuba hiyo.

        Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah amethibitisha kuwapo kwa ratiba ya Rais Kikwete kulihutubia Bunge na kwamba taarifa rasmi ingetolewa Bungeni kama utaratibu unavyoelekeza.

        Hadi saa hakuna anayefahamu Rais anataka kuongea nini na wabunge ingawa wafuatiliaji wa mambo ya kisiasa wanatabiri kuwa anaweza kutumia muda huo kutoa ufafanuzi kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba na pia ushiriki wa Tanzania katika Jumuiya ya Afrika MAshariki.

        inahusiswa Mara ya mwisho Rais Kikwete alilihutubia Bunge wakati akifungua rasmi Bunge la Kumi, Novemba 18, 2010 alipoeleza vipaumbele vya Serikali yake katika awamu ya pili ya uongozi wake. Rais Kikwete analihutubia Bunge wakati likisubiri kujadili mapendekezo ya marekebisho katika Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya 2013 ambayo ilipitishwa katika mkutano uliopita.

No comments: