Wednesday, December 18, 2013

BREAKING NEWS:WATU 200 WALIOKUWA WAKISAFIRI KWA NDEGE YA ETHIOPIAN AIRLINE WANUSURIKA KUFA BAADA YA KUTUA DHARURA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA ARUSHA




Taswira ya picha eneo la tukio
             Habari iliyoifikia hivi punde toka jijini Arusha, inaeleza kuwa Ndege ya abiria aina ya Boeing 787 ya shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines) mchana huu imeshindwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kutoka na hitilafu iliyokuwepo Uwanjani hapo na kulazimika kutua kwa dharula kwenye Uwanja wa Mdogo wa Arusha,hali iliyopelekea Ndege hiyo kusimama nje kabisa ya uwanja huo huku abiria zaidi ya 200 wakiwa ndani ya ndege hiyo mpaka sasa bila ya kushuka.
 
Wataalam wa Ndege wapo eneo la tukio hivi sasa kutafakari namna watakavyoweza kuwashusha abiria hao na kutafuta namna ya kuweka sawa mambo ili Ndege hiyo iweze kuruka.
 
Globu ya Jamii inaendelea kufatilia kwa ukaribu tukio hilo,na tutaendelea kufahamishana kadri taarifa itakavyokuwa ikitufikia.  PICHA NA MDAU WETU KUTOKA ARUSHA
CHANZO: BLOG YA PAPARAZI

No comments: