Wednesday, December 18, 2013

BREAKING NEWZZ:MV MAGOGONI YANUSURIKA AJALI

Kivuko kikubwa cha Mv Magogoni kinachofanya safari zake kati ya Kivukoni na Kigamboni jijini Dar es Salaam kimekosa muelekeo majini katika bahari ya Hindi kikiwa na abiria na magari baada ya injini zake kushindwa kufanya kazi,Mpaka sasa sababu ya injini kushindwa kufanya kazi hazijatoka.
Shuhuda anasema ‘Tulikua wanatoka Dar kwenda Kigamboni,hatua chache kabla ya kufika Kigamboni injini zilizima,baada ya kuzima zikaja Tag kwa ajili ya kutuvuta mpaka ng’ambo ya pili ambayo ni Kigamboni,na ilituchukua dakika 45 mpaka kuvutwa ng’ambo ya Kigamboni’
Taarifa kamili zinafata endelea kufatilia kupitiaHABARI24 BLOG


No comments: