Saturday, December 14, 2013

SAKATA LA KUFUNGIWA MWANAHALISI LAIBUKA BUNGENI,NAIBU WAZIRI MAKALA AMPINGA RAIS JK WAZI WAZI


Na Karoli Vinsent

  NAIBU Waziri wa Habari na Michezo Amosi Makala amepingana hadharani  Rais Jakaya kikwete kuhusu sakata la kulifungia Gazeti la mwanahalisi.

      Hayo yaligundulika wiki hii katika vikao vya bunge vinavyoendelea mkoani Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu,ambapo mbunge wa Mbinga Mashariki kapteini John Komba(CCM) alipokuwa anauliza swali kuhusu utaratibu  uliotumiwa na serikali katika kuyafungia magazeti ya mtanzania pamoja  mwanahalisi.

  “kwanini Serikali ilitumia nguvu katika kuyafungia magazeti ya Mwanahalisi pamoja na Mtanzania wakati tayari serikali ilikuwa imeshawaonya  wahariri hao na hao wahariri wa magazeti hayo wakakubali kosa na kuomba Radhi”aliuliza Komba
ENDELEA HAPO--------

    Naibu Waziri  wa Habari na Michezo Amosi Makala alipokuwa anajibu swali hilo ambalo likuwa tofauti na mkubwa wake wa kazi Rais Kikwete ambapo alisema Serikali haiku kurupuka  katika  kulifungia Gazeti la Mwanahalisi kwani Makala nyingi zilizokuwa zimeandikwa kwenge hili gazeti hilo zilikuwa za kichochezi.

   “Serikali haikukurupuka kufungia gazeti hilo kwani makala nyingi zilikuwa za kichochozezi kwa mfano makala ilyokuwa inasema Waziri Sophia Simba ni Muhuni na nyingine Zilikuwa zinawashutumu baadhi Maofisa wa Serikali kuhusika na utekaji unaoendelea hapa nchini”alizidi kufafanua Makala

   Uchunguzi uliofanywa na Habari24 umegundua majibu ya  Naibu Waziri huyo ni Tofauti na majibu aliyatoa  Rais Jakaya Kikwete alipokuwa kwenye Mkutano na waandishi Nchini Ethopia ambapo, alisema watu wanahoji na kuishutumu Serikali yake kulifungia gazeti la mwanahalisi wakati wamesahau Gazeti hilo lilikuwa linaandika Habari ambazo zinawataka wanajeshi watanzania kuhasi  serikali yao habari hiyo iliandikwa na Gazeti la Serikali .

    Wachambuzi wa Masuala ya Habari waliozungumza na Habari24 walisema utofauti huo wa majibu hayo. Unaonyesha kuwa Serikali haikuwa na hoja wala mantiki yeyote katika kulifungua Gazeti hilo kwani hakuna uthibitisho wa ukweli wowote kuwa Gazeti hilo lilikuwa limeandika habari za jeshi kuasi Serikali,bali ni ubabe ambao umekuwa unafanywa serikali katika kuyafungia magazeti hilo.

   Ripoti mbalimbali Duniani ikiwemo ya Shirikisho la waandishi habari Duniani (CPJ)ililiweka Tanzania sio Sehemu Salama kwa waandishi wa Habari, katika ripoti hiyo kuna vipengele ambavyo vinaishutumu serikali  ya Tanzania kwa kushindwa kuwapa ulinzi Waandishi wa Habari katika majukumu yao ya kila siku na ripoti hiyo ikaonyesha waandishi wa habari wa Tanzania wameacha kuandika habari za uchunguzi kwa kuhofia kufungiwa gazeti magazeti yao pamoja na usalama wa maisha yao.


No comments: