Saturday, December 7, 2013

samahani sana kwa picha hizi JAMBAZI SUGU LAPIGWA RISASI KICHWANI NA KUUWAWA WILAYANI KAHAMA, KAMA NI MWOGA USIFUNGUE.



Mwili wa jambazi hilo ukiwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama

Kijana mmoja ambaye hajatambulika jina lake mwenye umri kati ya miaka 26 hadi 30 ameuawa kwa kupigwa risasi wakati akiwa na wenzake wakijaribu kuvunja duka maeneo ya Shunu, kata ya Nyahanga wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Tukio hilo limetokea majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo ambapo jambazi hilo likiwa na wenzake watatu liliuawa kwa kupigwa risasi kichwani na Wilson Masolwa (63) mkazi wa mtaa huo ambaye alijeruhiwa kwa mapanga.
ENDELA NA PICHA HAPO CHINI---------------
Mtu huyo ameuawa kwa Bunduki aina ya Shortgun ambayo hata hivyo wenzake waliipora baada ya kumkata mapanga Masolwa na kupoteza fahamu.
Akizungumzia tukio hilo mmiliki wa nyumba hiyo Yasinta Patrick (32) amesema mtu huyo na wenzake walivamia katika nyumba yake, ambayo ameipangisha kwa wafanyabiashara wawili wa kutoa na kutuma fedha kwa njia ya mtandao.
Mmiliki wa nyumba iliyovamiwa Bi Yasinya Patrick
Yasinta ambaye pia amejeruhiwa kiasi amesema lengo la majambazi hao lilikuwa ni kuiba pesa katika maduka hayo baada ya kumfuata katika chumba kingine alichokuwa amelala na kumpiga huku wakimtaka atoe pesa za biashara hiyo.
Kwa upande wake Masolwa amesema baada  kusikia kelele alifika katika eneo la tukio na ndipo majambazi hao walianza kumkata mapanga kabla ya yeye kumpiga risasi ya kichwa mmoja wao na kufariki dunia papo hapo.
Mzee Masolwa alivyojeruhiwa wakati akipambana na majambazi hayo
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Kihenya Kihenya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na  kwamba Masolwa amefikishwa katika Hospitali ya wilaya ya Kahama kupatiwa matibabu na kuruhusiwa na kwamba hali yake inaendelea vizuri.
 
Kaimu kamanda wa polisi mkoni Shinyanga, Kihenya Kihenya
Kamanda Kihenya mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Kahamaa na kwamba jeshi la polisi linaendelea na msako wa kuwabaini na kuwakamata wahusika watatu waliotoroka ikiwa ni pamoja na bunduki waliyoipora.
Maduka yaliyokuwa yakifanyiwa uhalifu na majambazi hayo
Mtangazaji wa Redio Kahama FM Faraji Mfinanga akimuhoji Mzee Masolwa
CREDIT BY http://www.tuangaze.blogspot.com

No comments: