Tuesday, December 17, 2013

TAARIFA MUHIMU KUTOKA TIGO,YAWATANGAZIA NEEMA WATEJA WAKE

Na Karoli Vinsent

     KAMPUNI ya Simu za mkononi Nchini ya Tigo  imewatangazia Neema wateja wake baada ya kuzindua promosheni kabambe iitwayo “Cheza kwa Furaha Unaposhinda kitita”itakayowawezesha watumiaji wa huduma ya Tigo pesa kujishindia zawadi mbalimbali za fedha taslim  zenye jumla ya shilling bilioni moja.  

      Akizungumza na waandishi wa habari leo,Meneja Mawasiliano wa Tigo Bw.John Wanyacha amesema kwamba promesheni hii mpya inatokana na kampuni  hiyo kuweka kipaumbele kuwapa wateja wake sababu ya kutabasamu na fursa ya kuweza kubadilisha maisha yao  kupitia huduma za kutuma na kupokea pesa.

      “Jumla ya shilingi milioni 150 itashindaniwa.Kutakuwa na zawadi na fedha taslim milioni10 kila mwezi kwa wateja 10 kila mmoja,fedha taslim shiling milioni mbili kila wiki kwa wateja 20 kila mmoja na fedha taslimu shilingi laki mbili  kwa wateja   50 kila mmoja”alisema Wanyancha
ENDELEA HAPO CHINI--------



    “Aliongeza ,shindano hili ni njia mojawapo ya kuwafurahisha wateja wetu hususan msimu huu wa sikukuu.Tunaamini kwamba hii itakuwa kama zawadi ya kipekee krismasi hii na tunapoanza Mwaka mpya”

     Kupitia promesheni hii ya Tigo pesa “cheza kwa furaha unashinda kitita”wateja waliosajiliwa na huduma ya tigo pesa  na kufanya  miamala ya kiasi chochote cha fedha wataingizwa maja kwa moja  kwenye droo itakayowapa nafasi ya kushinda  zawadi xs fedha taslimu.

  Vilevile Wanyancha, alizidi kufafanua kwa kusema wateja waliosajiliwa na Tigo pesa wataweza kushiriki katika promosheni hii kwa kutuma Fedha ,kununua muda wa maongezi au kulipa Huduma mbalimbali kupitia tigo pesa

       Katika hatua nyingine Afisa huyo wa mawasiliano wa kampuni ya Tigo akaitaja miamala amabayo haitaruhusiwa kuingia kwenye droo ya shindani hilo ni pamoja na kuangalia salio ,kubadilisha pini,kuangalia taharifa fupi ya akaunti,kubadilisha lugha na kununua Kabaang.

     Huu ni mwendelezo wa kampuni ya tigo kuwapa raha wateja wake na kuonyesha kuwajali kwa kuzidi kuwazawadia mapesa,promesheni hii itaisha mwezi Februari 12 Mwaka 2014

No comments: