Friday, January 24, 2014

WAKATI KESHO LIGI KUU TANZANIA IKIANZA,AZAM TV KAMA KWA INARUSHA MECHI ZOTE LIVE ,CHEKI RATIBA HAPA



        Ligi kuu ya Vodacom sasa itarushwa moja kwa moja kupitia Azam TV ili washabiki wa mpira wa miguu Tanzania waweze kujionea mechi kali za ligi kuu muda wowote na mahali popote zitakapochezwa. Ligi hizi zitaonyeshwa katikati na mwisho wa wiki.           

Ratiba za mwisho wa wiki hii:


                       Jumamosi tarehe 25 Januari:

 Ashanti United na Young Africans zitacheza Uwanja wa Taifa (DSM)

Azam FC na Mtibwa Sugar zitacheza Uwanja wa Azam Chamanzi (DSM)


                          Jumapili tarehe 26 Januari:

JKT Ruvu na Mgambo JKT zitacheza Uwanja wa Azam Chamanzi (DSM)

Simba SC na Rhino Ranger zitacheza Uwanja wa Taifa (DSM)

Ratiba za wiki ijayo:


                             Jumatano tarehe 29 Januari:

Azam FC na Rhino Rangers JKT zitacheza Uwanja wa Azam Chamanzi (DSM)

Coastal Union na Young Africans zitacheza Uwanja wa Mkwakwani (Tanga)


                         Alhamis Tarehe 30 Januari:

Ruvu Shooting na Mbeya City zitacheza Uwanja wa Mabatini (PWANI)

Mechi zitaonyeshwa moja kwa moja kuanzia saa kumi kamili jioni.

Katika habari nyingine mpya na za kusisimua, mashabiki sasa watakuwa na uwezo wakuangalia dondoo za mechi zote kupitia simu zao za mkononi, ikiwapa fursa ya kuangalia matukio yaliyopita na kujua yatakoyojiri mechi zijazo.


        “Baada ya kupata kibali cha kuonyesha ligi kuu ya Vodacom, moja kati ya malengo makuu ni kuhakikisha kuwa tunafikia kiwango cha juu cha kimataifa. Katika kufanikisha hili, tumewekeza Zaidi kwenye teknolojia ya kisasa ya matangazo ya nje na mafunzo ya wafanyakazi wetu. Na tumedhihirisha hilo kwamba tumejizatiti katika kutoa matangazo yenye ubora wa hali juu tuliporusha Ligi ya kombe la Mapinduzi lililomalizika hivi karibuni” Amesema Rhys Torrington, mkurugenzi mkuu wa Azam Media.


            Azam Media Ltd waliingia mkataba wa miaka mitatu (3) na TFF wa haki za kutangaza na kuonyesha mechi zote za ligi kuu ya Vodacom wenye thamani ya Tshs 5,560,800,000.

AzamTV tayari inaonyesha chaneli Zaidi ya 50, zinazojumuisha chaneli maarufu za kimataifa na za kitaifa na chaneli tatu maalumu kutoka Azam. Chaneli hizo maalum ni:

·      Azam One – Burudani motomoto kwako na familia kutoka bara la Afrika, ambazo nyingi ni kwa lugha ya Kiswahili.

·      Azam Two – Programu maalum mbalimbali zilizochaguliwa ulimwenguni.

·      Sinema Zetu – Chaneli maalumu inayoonyesha filamu za kitanzania masaa 24.



        Kwa ujumla, chaneli hizi zinawapa fursa wateja wetu kuweza kuangalia kiwango cha juu cha michezo mbalimbali, filamu, vipindi vya watoto, tamthilia, maisha na burudani na mengineyo kwa bei nafuu kabisa ya Tshs 12,500/= tu!


         Kwa sasa Azam TV inapatakana Tanzania tu, lakini kwa wiki chache zijazo itaanza kupatikana Uganda na Kenya, kabla ya kuenea Afrika Mashariki kwa ujumla. Kwa ujumla AzamTV inakupa nafasi yawewe na familia yako kupata burudani mbalimbali kwa bei rahisi na nafuu.



         Azam Media itaendelea kuwekeza kwenye utengenezaji wa programu mpya za ndani ya nchi kupitia kampuni tanzu ya Uhai Productions kwa ushirikiano na watengeneza vipindi wa kitaifa.

Mwisho.


        

No comments: