Thursday, February 6, 2014

FUJO KATIKA CHAGUZI NDOGO ZA UDIWANI,CHADEMA YAMWANGUSHIA JUMBA BOVU IGP MPYA.YATANGAZA KULIWANIA JIMBO LA MAREHEMU MGIMWA RASMI

MKURUGENZI WA OGANAIZESHEN NA MAFUNZO WA CHADEMA AKIONYESHA BARUA YA TUIME YA UCHAGUZI YA KUTAMNGAZA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA KALENGA WAKATI AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM


Na Karoli Vinsent
          
          SIKU chache kupita baada ya Rais Kikwete kumteua mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu,Chama cha Demokrasia na Maendereo CHADEMA kimeanza kukosa imani naye.
      
       Hayo, yamegundulika leo wakati wa mkutano na Waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam,ambapo Mkuregenzi wa Mafunzo na organaizesheni wa chama hicho Bensoni Singo Kagaila alisema Jeshi la Polisi nchini linashirikiana na Chama cha Mapinduzi CCM katika kukihujumu chama hicho katika mikutano yake inayoenderea.
      ENDELEA=-----------

        “Nasikitika sana fujo zote zinazotokea katika mikutano yetu ya kampeni hizi za  uchaguzi wa madiwani wa kata kumi na sita,zinasababishwa na jeshi la polisi nchini kushirikina na chama cha mapinduzi, kwani wanachama wetu wanapigwa wanakatwa mapanga na watu wa Greengard huku polisi wakiwa kimya na kutochukua hatua yeyote”alisema Kagaila
    
        Kagaila,alishangaa kitendo cha Jeshi la polisi kuwakamata vijana wa Chadema wanaopigwa na Vijana wa Greengard wa CCM na kuwaacha wale wanafanya Vitendo hivyo.
      
        “Leo jeshi la Polisi limekuwa ni la CCM na linatumiwa na chama hicho ,inasikitisha sana pale Mkoani Iringa kijana wetu wa Chadema Kavunjwa Taya lakini waliomvunja taya wameachwa anakuja kukamatwa aliyevunjwa taya huku watu wa CCM Waliofanya unyama huo wameachwa jamani huu ni uonevu   tunaofanyiwa na Jeshi la polisi kushirikina na CCM“alizidi kuongeza Mkurugenzi huyo.
Kuhusu fujo za Iringa
       
       Mkurugenzi huyo alisema kuhusu kitendo cha Jeshi la polisi mkoani Iringa kumkamata Mbunge wa Iringa mjini Piter Misigwa  na kumweka ndani kwa mda wa siku moja ni uonevu.
          
     “Haingii akilini kweli mbunge huyu alikuwa  anahutubia watu jukwaani,leo jeshi la polisi liseme yeye ndie aliyempiga kijana wa CCM,huu ni uongo kwani mbunge huyo akushuka kwenda kumpiga kijana huyu na wala kijana na akupigwa kabisa na mtu yeyote wa chama chetu”
       
        Kwa mujibu wa Kagaila alisema mbunge huyo ameachiwa leo hii kwa dhamana,
          
       Chadema ambacho ni Chama Kikuu cha upinzani nchini,kimemtaka msajiri mpya wa vyama vya kisiasa Nchini kupiga marufuku na pia kuwaonya wanachama wa chama cha Mapinduzi kwa vitendo vyao vya kuingiria kwenye mikutano yao kwani ni kinyume na sheria ya uchaguzi.
         
       Katika hatua nyingine Chama hicho kimetangaza nafasi kwa mtu yeyote anayetaka kugombea nafasi ya Ubunge wa jimbo la Kalenga  uliochwa wazi baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wake.Dkt William Mgimwa kuomba nafasi hiyo kupitia kwenye mtando wa chama hicho au kuandika Sifa au cv na kuzipeleka chadema makao makuu jijini Dar es Salaam au kwenye ofisi za chama hicho mkoani iringa.
        
          Vilevile chama hicho kimesema mda wa kuomba nafasi hiyo ni tarehe 9 mwezi huu.na tarehe 12 kamati kuu ya Chadema itakutana 12  mwezi huu kwa ajili ya kufanya uteuzi wa mwisho wa jina la mgombea wa ubunge wa CHADEMA jimbo la Kalenga.
       
        Kwa mujibu wa Ratiba ya uchaguzi huo ulitolewa na Tume ya uchaguzi Nchini NEC,kampeni zitazinduliwa februali 19 mwaka huu .

No comments: