Thursday, February 27, 2014

MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI KITETO,LHRC YAJA NA TAMKO KALI,SOMA HAPA,BAADHI YA VIONGOZI WAHUSISHWA

WAKILI EMELDA URIO AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI MUDA MCHACHE ULIOPITA HAPA JIJINI DAR ES SALAAM

Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini tanzania leo kimeitaka serikali kuwachukulia hatua kali za kinidhamu  mkuu wa mkoa wa manyara,mkuu wa wilaya ya kiteto pamoja na mkurugunzi wa wilaya ya kiteto baada ya kugundua kuwa wao ndio chanzo kikubwa cha mgogoro wa wakulima na wafugaji uliotokea mapema mwaka huu na kugharimu maisha ya watu.

      Akizungumza na wanahabari jijini dar es salaam wakati akitoa tamko la kituo hiko kuhusu mgogoro huo wakili EMELDA URIO amesema kuwa kituo hiko kimegundua kuwa viongozi hao ndio chanzo kikubwa cha mgogoro huo baada ya kuruhusu ukusanyaji wa fedha usio wa halali kutoka kwa wafugaji ili kulipia gharama za dalali wa kuwaondoa wakulima katika eneo lenye mgogoro jambo ambalo amesema kuwa lilizua taharuki kubwa na baadae mapigano makubwa sana
         Aidha amezitaja sababu nyingine zilizochangia mgogoro huo kuwa ni mfumo mbovu wa matumizi ya ardhi ya kijiji kwani wale ambao wanaonekana ni wavamizi walipata ardhi maeneo hayo kutoka kwa viongozi wa kijiji kwa kutoa kiasi fulani cha fedha.

       Katika hatua nyingine kituo cha sheria na haki za binadamu kimelitaka jeshi la polisi kuhakikisha kinafwatilia kwa makini mgogoro huo na kuhakikisha kuwa linawachukulia hatua kali za kisheria wale wote wanaotajwa kuhusika katika mgogoro huo.


BAADHI YA MADHARA MAKUBWA YALIYOJITOKEZA KATIKA MGOGORO HUO

No comments: