Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania
ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi ya 19 kesho (Februari 22 mwaka huu)
kwa mechi tano zitakazochezwa katika miji ya Dar es Salaam, Bukoba, Morogoro,
Tanga na Arusha.
Yanga itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting
ya mkoani Pwani katika mechi itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Nayo Kagera Sugar inaikaribisha Rhino Rangers ya Tabora katika mchezo
utakaofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Uwanja wa Manungu uliopo Turiani
mkoani Morogoro ndiyo utakaotumika kwa mechi kati ya Mtibwa Sugar na Ashanti
United, wakati Coastal Union itaumana na Mbeya City katika mechi itakayooneshwa
moja kwa moja na Azam Tv kutoka Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Maafande wa Oljoro JKT watakuwa
nyumbani kupambana na Mgambo Shooting katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja
wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.
Jumapili (Februari 23 mwaka huu) katika
Uwanja wa Taifa ni Simba dhidi ya JKT Ruvu, mechi ambayo pia itaoneshwa moja
kwa moja na Azam Tv. Mechi kati ya Azam na Tanzania Prisons iliyokuwa ichezwe
kesho (Februari 22 mwaka huu) Uwanja wa Chamazi sasa itachezwa Jumapili
(Februari 23 mwaka huu) ambapo na itakuwa ‘live’.
No comments:
Post a Comment