Friday, February 28, 2014

TAARIFA MUHIMU KUTOKA AZAM TV JUU YA KUONYESHA MECHI YA YANGA LEO



1377169_224621101037472_893234737_nTumepokea maswali na simu nyingi sana zikiuliza kama Azam TV itaonesha mechi kati ya Yanga na Al Ahal leo, jibu ni kwamba HAPANA...           Ukweli ni kwamba tulipokea maombi toka kwa agent aliyenunua pambano kwa niaba ya Watu wa Misri ambaye aliomba Azam TV impe gharama za kuzalisha ili kuweza kupeleka feed yenye ubora wa kimataifa North Africa & Middle East na ikiwezekana kuonesha nchini Tanzania. Katika vikao vyote na Agent Azam TV iliweka wazi kuwa ipo tayari kuzalisha bure na hata kama ikibidi kuonesha delayed sawa kwa kuwa Yanga walionesha wazi kuzuia Live Coverage nchinikwa kuhofia mapato kupungua.
 
      Bahati mbaya Yanga waliikataa Azam TV na kuamua kutoa pesa waliyolipwa kukilipa kituo kimoja nchini ambacho ndicho kilichopewa kandarasi kwa malipo licha ya kutokidhi vigezo vya watu wa Egypt ambao walitaka angala 8 Camera OB na Azam TV iliwapa 10 Camera OB with HD Feed
 
         Kwa taarifa hii tungependa kuwaarifu wateja wetu kuwa Azam TV ilikuwa tayari kuwapa Yanga na Agent ushirikiano wote ili pesa yote waliyopewa na Watu wa Misri iingie klabuni lakini wao wameamua kuitumia kulipia production iliyo sub-standard ili mradi tuu kuinyima fursa Azam TV
 
       Pamoja na haya yote Azam TV inaitakia kila la kheri klabu ya Yanga kwenye mchezo wake wa leo, na inaamini matatizo hayapo kati ya Azam na Yanga kama taasisi bali mtu mmoja mwenye nguvu ndani ya Yanga

No comments: