Monday, February 3, 2014

URAIS NA CCM---SITTA ASEMA KAMWE HAWEZI KUMNADI LOWASA JUKWAANI


Na Karoli Vinsent
      WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Samweli Sitta ametangaza msimamo wake kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na kusema ,kamwe awezi kumnadi jukwaani Waziri mkuu aliyejiuzulu,Edward Lowassa endapo atapitishwa na CCM kuwa mgombea wa urais.
endelea----------


    Msimamo huu wa Sitta umekuja kipindi ambacho hali ya kisiasa ndani ya CCM ikiwa imefika katika hatua ya kutisha kutokana na Vita hiyo ya urais.

      Katika kuonyesha hali si swali ndani ya CCM Sitta alisema “Nitakuwa mwendawazimu kumnadi Lowassa jukwaani wakati muda wote msimamo wangu dhidi yake unajulikana”Sita alitoa msimamo wake wakati alipokuwa anazungumza na chazo chetu cha habari,

     Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki kupitia CCM alisema kama chama cha CCM kinataka kuvuka Salama Uchaguzi Mkuu 2015 ni Vema ni vema kikajitathimini na kusimamia misingi iliyoachwa wazi na Baba wa Taifa,Mwalimu Nyerere.

      “Haiwezekani kishindwe kuchukua hatua.mtu anamwaga pesa kanisani ,msikitini na kwengine halafu anaangaliwa tu”alihoji Sitta
Kwa mujibu wa Sitta kitendo cha Lowassa  kutumia pesa nyingi  za harambee ni ishara tosha kwamba ameanza kampeni kabla ya wakati na taratibu za chama

     “Hadi sasa hvi amrfanya harambeeza sh7bilioni.hizi pesa nyingi hanazitoa wapi lakini pia,watu wajiulize kwa nini anatumia fedha hizi”alizidi kuhoji Sitta
     
                           UCHUNGUZI ZAIDI

     Lakini,Duru za  uchunguzi wa mtandao huu umebaini Lowassa alipaswa kukutana na kamati ya maadili ya chama hicho mnamo tarehe 16.

         Hata hivyo Duru hizo zinasema Lowassa hakutokea ofisi ndogo za chama hizo zilizopo Lumumba jijini Dar ws Salaam lakini alikutana na Katibu mkuu wa chama hicho Abdulrahaman Kinana katika chakula cha usiku badala ya kumuita ofisini  ili akutane na kamati hiyo.

    “Jambo la ajabu la ajabu.Kinana badala ya kumuita  Lowassa ofisini ili ahojiwe kwanini ameanza kampeni mapema yeye alimuita katika chakula cha jioni kufanya nae mazungumzo kwa kumbembeleza”kilisema chanzo hicho

        Kwa mujibu wa Duru hizo zinasema katika kikao hicho cha kinana na Lowassa inasemekana Lowassa alikuwa anamuomba katibu mkuu huyo apewe nafasi ya mwisho ya kufanya harambee
            KIKWETE AKEMEA

        Akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya jana, Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, alisema kutoa fedha kunaharibu taswira ya chama hicho na kukiweka katika hatari ya kupoteza ushindi katika chaguzi zinazokuja.

      “Agizo la CCM la miaka mingi iliyopita ni kwamba kila ngazi kuwa na shughuli za kuwaingizia mapato sambamba na kuwa na mfuko wa uchaguzi. Agizo hili bado halijatekelezwa na ndiyo linakiathiri chama,” alisema Rais Kikwete.

        Alisema hali hiyo imekiathiri CCM: “Hivi sasa viongozi wanachukua fedha chafu kutoka kwa watu wenye sifa mbaya na nia chafu. Hata wanaotoa rushwa hupokewa kishujaa.”

     Alisisitiza wanaotoa fedha chafu kwa ajili ya kuimarisha chama lazima wahojiwe akisema wema huo wameutoa wapi ilhali walikuwapo siku zote. Alisema taswira ya chama hicho ikiwa nzuri, kitaungwa mkono na ikiwa mbaya kitachukiwa na watu.

       Aliwataka viongozi na wanachama wa CCM kulipa uzito unaostahili suala la uadilifu na kwamba bila kufanya hivyo chama kinaweza kuwa imara na kutekeleza majukumu yake lakini kisiungwe mkono na wananchi.

     “Tusipoungwa mkono na wananchi tunaweza kupoteza ushindi. Ndiyo maana chama kikaunda Kamati ya Usalama na Maadili kufanya kazi ya kuwabana watu wanaokiuka maadili, naomba kamati hizo zifanye kazi yake ipasavyo,” alisema.

       Alisema kamati hizo zisipokuwa makini zitaathiri hadhi na kukubalika kwa CCM katika jamii.
“Vitendo hivi vibaya lazima tuvikatae na tuvipige vita kwa nguvu zetu zote. Tusiwaache watu wachache wanaotaka uongozi wa gharama yoyote waharibu sifa nzuri ya CCM.”
Alisema watu hao wakiachwa itajengeka dhana potofu kwamba uongozi ndani ya CCM ni wa kununua.

                      WANAOLUMBANA NA LOWASSA
Malumbano kuhusu ‘safari’ ya Lowassa yalianza kwa baadhi ya wenyeviti wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Geita, Joseph Kasheku `Msukuma’ kukana kauli ya Mwenyekiti wa CCM wa Singida, Mgana Msindai kuwa wenyeviti wote wa CCM wa mikoa walikuwa wanamuunga mkono Lowassa. Hata hivyo, Msindai alikanusha suala hilo.  

       Makamu Mwenyekiti wa zamani wa CCM, John Malecela na Mkuu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM, Paul Makonda pia walimtuhumu Lowassa kwamba anakivuruga chama hicho kwa kuanza kampeni mapema za urais.
Hata hivyo, kauli zao zilipingwa vikali na makada wengine wa chama hicho akiwamo Mgeja, Mwenyekiti wa zamani wa CCM wa Dar es Salaam, John Guninita na viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM wa Morogoro.

No comments: