Na Karoli Vinsent
RAIS Jakaya Kikwete Ameeanza kumuiga
Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa kile kinachodaiwa ameanza kurithisha
uongozi Famili ya yake ndani ya Chama cha Mapinduz CCMi ,.
Haya yamegundulika Baada ya Mtoto wa Rais,
Ridhiwani Kikwete Kupitishwa na Wajumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha
Mapindzu CCM, yaani NEC kugombania Ubunge wa Katika Jimbo la Chalinze.
Kupitishwa kwa Ridhiwani na NEC, imekuja
ikiwa Tayari Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
Taifa (NEC) ya Chama hicho ambapo alichaguliwa Kupitia Wilaya ya Lindi Mjini
Huku naye Mtoto wake wa kiume Ridhiwani ni
Mjumbe wa NEC kupitia Wilaya ya Bagamoyo .Ikumbukwe wote hao walipita bila
kupingwa.
Duru za kisiasa zinasema Rais Kikwete
ameanza kumiga Rais Musevini kutokana Rais huyo wa Uganda kwenye utawala wake
amewaweka Ndugu zake kwenye Nafasi za juu za Jeshi la Uganda hadi kwenye
utawala Wa serikali.
Museveni,ambaye aliweka Rekodi Barani
Afrika kwa kitendo cha kumteua Mkewe kuwa Waziri wa Masuala ya Karamoja
Nchini humo,bali pia amegawa madaraka ya umma kwa ndugu zake wa Kuzaliwa.
Mdogo wake,Salim Saleh,kuwa mshauri
Mwandamizi wa Rais akiwa amemuhamishia kutoka Waziri wa Fedha wa Uganda.Mwanae
wa Kumzaa Bregedia Muhoozi ni mkuu wa Vikosi maalum vinavyomlinda
Museveni.
Duru hizo zinasema licha ya kuwa tofauti na anavyoanza Rais
Kikwete,lakini Rais Kikwete ameweka Rekodi ambazo azikufikiwa na Watangulizi
wake kwa kitendo chake cha kuidumbukiza Familiya yake kwenye Siasa.
Wachambuzi Mbalimbali waliozungumzia
hili,akiwemo Mwandishi na Mhariri Mwandamizi wa Gazeti la Tanzania Daima
Edsoni Kamukara katika moja ya Makala yake alishangaa kwa hatua taifa letu
inayofikia ya Viongozi Kuanza kupandikisha viongozi watoto wao kwenye Utawala
huku wakiwa hawana uwezo.
“Tutakuja kujikuta siku moja tuna
serikali inayoundwa na ‘family friends’. Ni kweli inatokea sehemu nyingi
duniani ambako watoto wanawarithi wazee wao. Lakini karibu mara zote
ukifuatilia tabia hiyo ya serikali za ‘kifamilia’ utakuta uporaji
au matumizi mabaya ya mali za umma.
Ikumbukwe kwamba jimbo analotaka kugombea
Ridhiwani ni jimbo ambalo baba yake pia alikuwa mbunge kabla ya kupaa hadi kuwa
rais. Uteuzi huu hata kama ulifuata vigezo vya wagombea unaweza kufanya
watu wakaanza kujiuliza tena ile tambo maarufu ya Chama Cha Mapinduzi
kwamba CCM ina wenyewe! Je, wenyewe ndio baba na watoto wao au
inahusisha pia kila aliye na kadi ya chama hicho?ilisema makala hiyo ya
Kamukala.
Ridhiwani kikwete alikaliliwa na Vyombo
vya Habari wiki hii alisema jina la Kikwete alina mashiko yoyote kwake
katika kushinda ujumbe kwenye baraza kuu la vijana la CCM,pia alina mvuto
kupata U_NEC na hata sasa nafasi ya yeye kugombania ubunge wa chalinze.
Duru za Kisiasa zilipinga kauli hiyo ya
Mtoto wa Rais kikwete mwenye miaka 30-40 na kusema yeye ni
mtu anayeangalia jua angani mchana saa sita wakati jua kali na kusema
kwanini jua alingai.
Yeye anatamka hivyo amekuwa kipofu
asiyejua chochote kinachoendelea,Ridhiwani anatoa kauli hiyo akiaamini kila
mtanzania ni Juha na hajui kupambuna mambo,Jina la Baba yake Tangu anakuwa
Waziri mpaka leo Rais wa Nchi haijaweza kumsaidia mpaka yeye kufika hapo.
Udhaifu mkubwa wa Mtoto huyo wa Rais
kujenga hoja,anaonyesha Taswira moja kwamba kijana huyo asemi ukweli na
anajitahidi kusema uongo kwa nguvu sana ili kubadilisha uongo kuwa
ukweli,ukweli ni Kwamba kikwete Ndiyo gia yake kubwa la kufanikiwa.
Huu ni mwenderezo wa Rais
Kikwete kutuhadaa Watanzania,
No comments:
Post a Comment