HAYA SASA---DK SLAA NA MAKATIBU WA VYAMA VYA UPINZANI WAUNDA UKAWA NJE YA BUNGE,WATANGAZA KUFANYA MIKUTANO MIKUBWA NCHI NZIMA KUPINGA MCHAKATO WA KATIBA MPYA,KESHO WANAANZIA MWANZA,SOMA HAPA

Makatibu wakuu wa vyama vya CHADEMA,CUF,NA NCCR MAGEUZI wakizungumza na wanahabari jijini dar es salaam baada ya kutangaza muungano wao wa kupinga mambo ambayo yanaendelea bunge maalum la katiba

     Mungano wa vyama vitatu vya upinzani vyenye wabu nge bungen ambao kwa sasa unajiita umoja wa katiba ya wananchi UKAWA leo umetangaza kufanya mikutano ya hadhara kiwa mikoa yote Tanzania kupinga kile ambacho wanakiita kuhujumiwa kwa mchakato wa kupata katiba mpya ambao wanaituhumu moja kwa moja ccm kuwa wanataka kuhujumu mchakakato wa kupata katiba mpya.

              Akitangaza maamuzi hayo ambayo ni ya makatibu wakuu wa vyama vya CUF,NCCR MAGEUZI NA CHADEMA,katibu mkuu wa CHEDEMA dk WILBROD SLAA wakati wa mkutano na wanahabari katika katika makao makuu ya CHADEMA amesema kuwa ukawa imekuwa ikifanya kazi ndani ya bunge na sasa wameunda UKAWA nje ya bunge ili kuwasaidia wale waliopo bungeni kuwaletea watanzania katiba ya wananchi na siyo ya ccm.

          Dk SLAA anasema kuwa UKAWA NJE  wameamua kuwafuata wananchi wa Tanzania kuwaunganisha nguvu zao na kuwaeleza ukweli juu ya mchakato wa katiba mpya unavyotekwa na ccm na kufanya wabunge wa bunge maalum la katiba wanaotaka katiba ya wananchi kuonewa ndani ya bunge na kutokutendewa haki katika bunge hilo.

          Anasema kuwa UKAWA  NJE watafanya mikutano ya hadhara nje na ndani kwa nchi nzima ambapo kampeni hiyo wametangaza kuizindua kesho mkoani mwanza na baadae kufanyika kila mkoa wa Tanzania.

Katibu mkuu wa CHADEMA DK WILBROD SLAA akizungumza kwa niaba ya makatibu wakuu wenzake katika mkutano na wanahabari jijini dar es salaam muda mfupi uliopita

About HABARI24 TV

Post a Comment
Powered by Blogger.