Na Karoli Vinsent
SIKU chache
kupita baada ya Gazeti la “This Day” la Tanzania kuishutumu Idara ya Uhamiaji
nchini kuhusika katika kutoa vibali kwa wadada wenye asili ya Kihindi ambao
wanajihusisha na Biashara ya uchangudoa hapa nchini, Idara hiyo ya Uhamiaji
imekuja juu na imekanusha taarifa hiyo na kusema hawahusiki katika kutoa
vibali hivyo.
Hayo,
Yalisemwa leo Jijini Dar es Salaam,na Kamishna wa Idara ya uhamija nchini
Abbasi Mussa,wakati wa mkutano na Waandishi Habari,ambapo alisema Idara
hiyo ya uhamiaji ni Idara kama ilivyo kwa watumishi wengine,na kwamba
wana wajibu kama wa kusimamia sheria.
“Napenda
kutoa taarifa kwa umma ya kwamba ni vyema ikaeleweka bayana kuwa
watumishiwa idara ya uhamiaji kama walivyo watumishi wengi wa Serikali
,wanafanya kazi kwa mujibu wa kusimamia sheria mbalimbali zinazohusu uhamiaji
kwa uhadilfu mkubwa”\
“Kwa msingi
huu,Afisa yoyote wa uhamiaji anaejihusisha na vitendo vya kupokea rushwa akiwa
katika majukumu yake ya Kazi atakuwa amekiuka sheria za nchi na anatakiwa
kustakiwa”alisema Mussa
Taarifa
hii ya uhamiaji imekuja baada ya Gazeti la This Day katika toleo lake la Tarehe
16 machi 2014,ukurasa wa kwanza,lilitoa taarifa,yenye kichwa cha Habari “Asian
Girls in Dar Sex Trade”_Police,immigration official blamed for allowing
human Trafficials,prostitution Activities in Mujra Clubs”
Katika
taarifa hiyo ilidaiwa kuwa rushwa na kukosa umakini “Laxity” kwa upande wa
maofisa polisi na maofisa uhamiaji kumechangia kuwepo na mtandao
unaowazesha kushamiri kwa biashara ya ngono zinazofanyika katika “MUJRA CLUBS”
ikihusisha wasichana kutoka nchi za India,Nepal,Pakistan na Bangladesh .
Taarifa hiyo
ilizidi kusema Maofisa hao wamedaiwa kupokea Rushwa kutoka kwa Baadhi ya
wafanya biashara wenye asili wa kihindi ili kuwa sili ya kihindi ili kuwaruhusu
kufanya biashara hiyo ya ukahaba.
No comments:
Post a Comment